Kila nikimtazama 20 Percent natokwa na machozi

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,427
21,118
Niseme tu wazi miongoni mwa wanamuziki wenye vipaji tofauti tofauti vya hali ya juu ila hawajielewi basi mmoja wapo ni huyu ndugu yetu Abasi Kinzasa (20 Percent).

20 Percent ni msanii wa hali ya juu mwenye uwezo wa hali ya juu wa kuandika na kuimba nyimbo zinazoteka hisia za watu kwa kiasi kikubwa mno ila marafiki wa hovyo waliokuwa wakimzunguka ndio waliochangia anguko lake la kimuziki.

Ikumbukwe msanii twenty percent ndiye msanii wa kwanza kihistoria kubeba tuzo nyingi za Kilimanjaro Music Awards kwa mara moja baada ya kufanikiwa kubeba tuzo 5 za Kilimanjaro Music Awards mwaka 2011 katika vipengele sita alivyokuwa anawania kabla historia hiyo haijavunjwa na Diamond Platnumz mwaka 2014 baada ya Diamond kuweka rekodi ya kuchukua tuzo 7 za Kilimanjaro Music Awards rekodi ambayo haijavunjwa mpaka leo.

Sasa kilichomponza 20 ni hizi tuzo maana zilimvimbisha kichwa sana nakuona ameshamaliza kila kitu akawa ni mtu wa starehe starehe na yeye badala ya kuumiza kichwa kutoa kazi zingine kali zaidi.

Na alizidi kupotea zaidi baada ya yeye na producer wake ambao chemistry zao mara nyingi zinaendana (Man Walter) maana hapa kila mmoja alijiona yupo juu ya mwenzie.
20 Percent alivuka mipaka kwa kumtusi mpaka Diamond Platnumz kwamba eti si lolote si chochote hapa ndipo alipozidi kujiharibia.

Na kama hiyo haitoshi juzi kati hapa alipoenda kuhusu ishu ya Juma Nature na kusema "Achilia mbali Juma Nature kutaka kulipwa laki 5 kwa show, Mimi kwa hadhi yangu sifanyi show hata kwa milioni moja" .

Tuachane na mambo ya muziki turudi kwenye upande wa kuigiza.

Kwa upande wa kuigiza 20 Percent amewaacha mbali sana waigizaji wengi sana hapa bongo kiasi kwamba alikuwa tishio mpaka kwa marehemu Steven Kanumba ila tu jamaa hakuwa serious na Sanaa ya maigizo.

Kupitia filamu ya Furaha Ipo wapi jamaa aliuonesha ulimwengu upande wake wa pili wa vipaji alivyojaliwa na Mwenyezi Mungu. 20 alizidi kujizolea mashabiki lukuki na hapo akajisahau tena na kuvimba kichwa kwa kutaka dau kubwa ili aje kuigiza kwenye filamu yako ,alikuwa anataka kucheza filamu kwa milioni 4 kama sikosei wakati kwa kipindi hicho hata akina Kanumba wenyewe dau lao lilikiwa halifiki huko.

Yote kwa yote muda bado upo ,kurudi kwenye muziki kwa Sasa na kuwika ni ngumu ila arudi kwenye kuigiza atang'aa sana hilo halina ubishi kabisa.

download.jpeg



2011 winnersEdit

Main article: 2011 Tanzania Music Awards
CategoryArtistTrack
Best Male Artist20 Percent
Best Female ArtistLady Jaydee
Best Male Singer20 Percent
Best Female SingerLinah Sanga
Best Song Writer20 Percent
Best Upcoming ArtistLinah Sanga
Best Hip Hop ArtistJoh Makini
Best Rapper (from a Band)Khalid Chokoraa
Best Song20 Percent'Tamaa Mbaya'[6]
Best music videoCPWAA ft Ms. Triniti, Albert Mangwea & Dully Sykes'Action'
Best Afro Pop Song20 Percent'Ya Nini Malumbano'
Best R&B SongBen Pol'Nikikupata'
Best Zouk/Rumba SongBarnaba Classic'Nabembelezwa'
Best Hip Hop SongJCB ft Fid Q & Chidi Benz'Ukisikia Paah'
Best Collaboration SongJCB ft Fid Q & Chidi Benz & Jay Moe'Ukisikia Paah'
Best Swahili Song (from a Band)Mapacha Watatu ft Mzee Yusuph'Shika Ushikapo'
Best Ragga/Dancehall SongCPWAA ft Ms. Triniti, Albert Mangwea & Dully Sykes'Action'
Best Reggae SongHardmad ft Enika & BNV'Ujio Mpya'
Best Taarab SongJahazi Modern Taarab'My Valentine'
Best East African SongKidum & Lady Jaydee'Nitafanya'
Best Traditional SongMpoki Mjuni ft Cassim'Shangazi'
Best ProducerLamar (Fish Crab)
Hall of Fame trophy
  • to an individual: Said Mabera
  • to an institution: Tanzania Broadcasting Radio (TBC)

 
Diamond Platnumz amethibitisha kuwa ndiye msanii namba moja kwa sasa nchini Tanzania baada ya usiku wa Jumamosi kunyakua vipengele vyote zote saba alivyokuwa ametajwa kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro, KTMA.


IMG_9370.jpg
 
Laki 5 dau la underground artists.
Dharau kwa legend wa bongo flavor ziishe.
 
Enzi zao walikuwa wanalipwa bia tu hao
Laki tano yoote hiyo
Sasa siyo enzi hizo.
Enzi za utoto wako ulikuwa unatembea na nguo ya ndani tu, Je, sasa unaweza kutembea na hizo nguo za ndani pekee?

Kilo ya sukari ilikuwa 1600/- Sasa 3000/-
Sembe 900/- Sasa 2000/-
Soda 500/- Sasa 600/-
Cement mfuko 9500/ Hadi 12,000/-
Hospital ya wilaya kufungia jalada 6000 Sasa .....
Simu hakuna Tozo ...
Bank hakuna kodi za miamala...
Petrol Lita moja 2000/- Sasa 3300/-
Nyama kilo 5000/- Sasa 8000/-
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom