Mzee Yusuph: Walio na nyimbo zangu kwenye simu zao wafute

chiefnyumbanitu

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
906
426
Aliyekuwa mfalme wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuph amefunguka na kueleza kuwa watu wote walio na nyimbo zake kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza ili kuepuka dhambi.

Katika mahojihano na kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha Times Fm, Mzee Yusuph ameelezea maisha yake ya ndoa, kidini na kiuchmi yalivyo kwa sasa ukilinganisha na hapo awali.

“Mimi nikikubali watu wacheze nyimbo zangu ina maana nimeruhusu dhambi tena ni bora nirudi kuimba muziki tena hivyo, watu wote waliokuwa na nyimbo zangu kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza kuepuka dhambi,” amesema Mzee Yussufu.

Mzee Yussufu amesema yeye hayupo kwenye kundi lake la ‘Jahazi Modern Taarab’ kama baadhi ya watu wanavyodhani na wala hafuatilii kabisa kundi hilo.

“Nilitaka kulivunja Kundi la Jahazi lakini sheria za nchi haziruhusu nikaliacha na haya niliambiwa na Basata wenyewe. Vyombo vya bendi ya Jahazi havikuwa vya kwangu tulikuwa tunasaidiana na mabosi,” amesema.

Katika hatua nyingine Mzee Yusuph amesema maisha ya kiuchumi kwa sasa ni toufauti na kipindi alichokuwa anafanya muziki kwani hapo awali kwa wiki alikuwa anaweza kutengeneza milioni moja na nusu mpaka mbili ila sasa kushika laki tano au milioni inaweza kumchukua miezi miwili.

Ameongeza kuwa wake zake wanne bado anaendelea kuishi nao kama kawaida, na kuwa na wake ni jambo ambalo amehimizwa na sio amri, na kwa sasa wanamjua ni mtu wa namna gani na mambo yote yanaenda sawa hakuna hata mmoja anayefanya sivyo.

d28c79aae0e581a8717129ee818cf03a.jpg
 
We kaa hapo kumsengenya mwenzio, wakati mwenzako anafanya toba. Mwisho wa siku wewe dhambi zako huzitaji sijui ni mtakatifu mwenzetu.
si afanye kimyamya aache unafiki. Anataka msamaha kwetu ama kwa Mungu??
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwani mzee yusuph ukikaa kimya unapoteza nn embu acha kuonesha upuuzi wako mbele za watu bana. Dini ni imani iliyo moyoni mwako wapo wengi waliotenda maovu na wanatubu kimya kimya. Anza usafi kwa mkeo bado analindima majukwani usiku upo naye kitandani.
 
Hongera mzee yusuph kwa kufanya toba,ni jambo jema sana na Mungu anatuagiza tufanye toba
Sasa somo linakuja kwa Wasanii wengine,Mzee Yusuph amepata bahati sana had I kupata nafasi ya kufanya toba ni bahati sana kwa mwenzetu,
Wasanii mupate somo kwa mambo yetu mnayo yafanya
1:Snura na wimbo wa chura hii dhambi itakuwa kizazi na kizazi usipo tubu,Leo wanawake wanaonesha video za uchi wakitingisha chura zao jutia jambo hili
3:Acheni kuimba na kusifia Dhambi
4:Acheni ushirikina Wasanii wengi ni washirikina sana refer to Meneja Maneno
5:Zinaa
Nk: Fanyeni toba nyimbo zetu zinaleta madhara katika jamii
 
Kumbe mzee Yusufu alikuwa na tabia hizo, aisee bora ametubu na kumrudia Mungu wake
 
Huyu katenda dhambi sana
1:Mchawi na mshirikina jamaa ameloga watu sana
2:Umalaya na uzinzi

Bila ya Watu kufanya Dhambi Toba isingekuwepo

Kwa Mujibu wa Imani ya Kiislam Makosa karibia yote yanasamehemeka kwa Masharti Tofauti tofauti

Kwa Mfano kosa ulilomfanyia Mwanadamu Mwenzako Toba yako kwa Mwenyezimungu inapaswa kuanza kwa kuomba Msamaha kwa uliemkosea

Miongoni wa Makosa ambayo Halina Msamaha kabisa ni kosa la Ushirikina hili Utakwenda nalo mpaka siku ya Mwisho kwenda kufanyiwa Assement kati ya Mema yako na mabaya yako
 
Kwani mzee yusuph ukikaa kimya unapoteza nn embu acha kuonesha upuuzi wako mbele za watu bana. Dini ni imani iliyo moyoni mwako wapo wengi waliotenda maovu na wanatubu kimya kimya. Anza usafi kwa mkeo bado analindima majukwani usiku upo naye kitandani.

Chanzo cha hayo aliyoeleza ni Mahojiano na Mtu aliekuwa anamhoji hakuitisha press conference na kuanza kufunguka tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom