mimi siamini kabisa hawa janja janja wanaojitokeza siku hizi za mwisho. wakitumia mbinu mbalimbali na utaalamu wa kucheza na lugha na akili za wengi wasioelewa.
nitaendelea kufwata misingi ya kanisa langu nililokuwa nikiliona na kumwamini mungu kwa namna ninayoona mimi inanipasa kwa miongozo ya imani yangu.
hawa nitabaki kuwasikiliza tu wanayoyasema kama watu wengine wa kawaida penye kucheka nitacheka penye kushangaa nitashangaa kamwe sitaki kuwaamini, oh mchungaji,mtume,nabii,mzee wa upako,mzee wa ufufuo n.k yote haya ni kuwa nayo makini sana katika siku hizi za mwisho kama ilivyotabiriwa katika vitabu vya dini. watakuja kwa lugha tamu,miujiza tele wakisema njoo huku yesu yupo huko lakini WALIO NA ROHO WA KWELI WA MUNGU watajua kuwa hao ni wadanganyifu tu.