MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 295
- 679
Askofu wa Kanisa la Gospel Revival Center – Ubungo Kibangu Mchungaji Anthony Lusekelo, Mzee wa Upako (Chifu Mwantembe) amewataka watanzania kuendelea kuiunga serikali mkono katika ulipaji wa kodi (Tozo) uliotukuka ili kuweza kujenga taifa lenye uchumi imara.
Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari leo Septemba 3, 2022 ofisini kwake Ubungo Kibangu, amesema swala la kulipa Tozo lipo toka zamani na hata katika vitabu vya dini limezungumzwa.
“watu wengi watakuwa wanajua maana ya Zaka na Zabihu, zilichukuliwa kwa wananchi ili kuendesha nchi yao, hivyo mambo ya kuchukua tozo yalianza kutoka mambo ya Torati, hamuwezi kuendesha nchi yenu bila kuchukua nguvu za wananchi wenyewe kwa kuendesha taifa lenu na mambo ya ibada” alisema Mzee wa Upako.
Mzee wa upako ameeleza kuwa, katika vitabu vya dini ulipaji wa kodi ulianza mnamo kipindi cha waisraeli walipokuwa wakihitaji mfalme wao Sauli na kuambiwa wataendesha nchi yao kwa kutozwa kodi ili kuimarisha taifa lao.
Mzee wa Upake alihitimisha mazungumzo yake na wanahabari kwa kusema "Kulipa kodi ni wajibu wakila Mwananchi katika kujenga Taifa, viongozi wetu wana nia ya dhati kabisa katika taifa hili, hivyo ni wajibu wetu sote kulipa Tozo na Kodi ili kujiletea maendeleo"