Mzee wa Upako: Watanzania hawana ustashi kuchangia maendeleo ya nchi yao

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) nchini Tanzania, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ ameonyesha sura mbili katika sakata la tozo za miamala ya kielektroniki.

Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeonyesha usikivu kwa umma baada ya kupungua na kufuta baadhi ya tozo katika miamala ya kielektroniki.

Tozo hizo zilianza Julai mosi, 2022 ikiwa ni utekelezaji wa marekebisho ya Sheria ya Fedha ya 2022 na zimedumu miezi miwili tu kabla ya kufanyiwa marekebisho baada ya makundi mbalimbali kupinga.

Marekebisho hayo yataanza kutumika Oktoba 1, 2022.

Msingi wa hoja yake leo Jumamosi umejikita katika muhimu wa kuzingatia viwango halisi vinavyotakiwa kutozwa bila kuumiza wananchi ikiwa ni tofauti na hoja yake ya wiki tatu zilizopita.

Itakumbukwa Septemba 3, 2022, Mzee wa Upako alinukuliwa mbele ya wanahabari akisema jambo la kwanza ni nia na utashi wa kulipa kodi nchini.

“Viwango sio tatizo, utashi wa watanzania kuchangia maendeleo ya nchi yao haupo, hata ungeweka sh100 wangetakaa (kulipa), muhimu ni kujenga nia ili serikali itimize malengo yake.”

Hoja ya leo, Mzee wa Upako amesema Ufalme wa Israel chini ya Rehoboam ulianguka baada ya kubeza maoni ya wazee walioshauri kupunguza viwango vya kodi.

“Lakini Rais amezingatia maoni na hisia za wananchi akiwa tofauti na mfalme Rehoboam, kodi lakini kiwango gani ndio ilimuangusha,” amesema na kuongeza:

“Mwezi uliopita nilisema kulipa kodi ni lazima kwa mujibu wa Biblia, atakayepinga ama ni mlevi wa konyagi au mvuta bangi, hakuna nchi inayojiendesha bila kodi.”

Alipoulizwa sababu za kutoa kauli mbili zinazokinzana katika tozo, Mzee wa Upako amesema awali alihoji pia umuhimu wa kujadili viwango.
 
Ila wanao utashi kuchangia maendeleo ya kanisa lake🚶
 
Back
Top Bottom