A.Lusekelo( Mzee wa Upako, Pombe Si DHAMBI, ni kosa.

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,103
22,547
Salaam, Shalom!!

Baada ya Pope wa Katoliki kuwadissapoint waumini, Mzee wa Upako,kama anavyojiita, Tingatinga, ametoka hadharani na kuhalalisha pombe Kwa waumini wake.

Ameongea hayo madhabahuni kuwa, BIBLIA haijakataza POMBE,Wala KULEWA, Bali Biblia imekataza ULEVI.šŸ˜³šŸ˜³ Amejiumaumaaa.....

Amedai kuwa pombe haijakatazwa kwenye BIBLIA, uliokatazwa ni ulevi, ndo sababu ulevi wa pombe ukazuiwa.

Kwa mliokuwa mnajiuliza mara mbili ikiwa Anto Lusekelo ni Nabii wa uongo au la, uamuzi ni wenu sababu naye ameonyesha RANGI zake halisi tena madhabahuni.

Ni suala la muda tu, manabii matapeli wote, watakiri hadharani kuwa wao Si watumishi wa Mungu, Bali matapeli.

(Yoshua 1:8 )na (Zaburi 1:2) inatutaka kulitafakari SHERIA ya BWANA Mungu Mchana na usiku.

(Waefeso 5:18) Msilewe Kwa mvinyo maana mna ufisadi, Bali mjazwe Roho.

(1 Korinthians 6:9-11) says Mtu asiwadanganye, Bali waongo ,wazinzi ,WALEVI hawataurithi ufalme wa Mungu.

Source: Upako wa Mzee Tv

KaribunišŸ™
 
Mimi sio mlokole na sisali kwake ila pombe sio dhambi,ulevi ni dhambi.Yesu kwenye harusi ya Kana alitengeneza divai na watu walikunywa,kila kitu kinapaswa kuwa kwa kiasi.Anaweza kuwa nabii wa uongo ila ameongea ukweli.
Divai Si pombe.

Divai waliyokunywa haikuchachuliwa.

Hawakulewa. Nenda Israel hata Leo, divai hiyo utaikuta.

Kimbia haraka manabii fake,

Wapo manabii wa Kweli nenda kwao.
 
Salaam, Shalom!!

Baada ya Pope wa Katoliki kuwadissapoint waumini, Mzee wa Upako,kama anavyojiita, Tingatinga, ametoka hadharani na kuhalalisha pombe Kwa waumini wake.

Ameongea hayo madhabahuni kuwa, BIBLIA haijakataza pombe,Wala kulewa, BIBLIA imekataza ulevi.

Amedai kuwa pombe haijakatazwa kwenye BIBLIA, uliokatazwa ni ulevi, ndo sababu ulevi wa pombe ukazuiwa.

Kwa mliokuwa mnajiuliza mara mbili ikiwa Antony Lusekelo ni Nabii wa uongo au la, uamuzi ni wenu sababu naye ameonyesha RANGI zake halisi tena madhabahuni.

Ni suala la muda tu, manabii matapeli wote, watakiri hadharani kuwa wao Si watumishi wa Mungu, Bali matapeli.

Source: Upako wa Mzee Tv

KaribunišŸ™
Rekebisha andiko lako, Lusekelo sio nabii bali anajiita mchungaji alimaarufu kama chief Mwantembe, mzee wa upako, Chief Masandube et al.
 
Bado mnamsikiliza huyo tapeli? Shauri zenu. Alikuja nabii Tito na injili yake ya pombe mkamsupport ila alipojitangaza shoga mkamkimbia. Shauri zenu.
 
Divai Si pombe.

Divai waliyokunywa haikuchachuliwa.

Hawakulewa. Nenda Israel hata Leo, divai hiyo utaikuta.

Kimbia haraka manabii fake,

Wapo manabii wa Kweli nenda kwao.
Yohana 2:7
Yesu akawaambia: ā€œIjazeni mitungi hiyo maji.ā€ Nao wakaijaza pomoni. 8 Akawaambia: ā€œChoteni kidogo na kumpelekea msimamizi wa karamu.ā€ Basi wakampelekea. 9 Msimamizi wa karamu alipoonja maji yaliyokuwa yamegeuzwa kuwa divai, bila kujua divai ilitoka wapi (lakini wahudumu waliokuwa wamechota maji hayo walijua), akamwita bwana harusi 10 akamwambia: ā€œKila mtu hutoa divai nzuri kwanza, kisha hutoa divai hafifu wakati ambapo watu wameingiwa na kileo. Lakini wewe umehifadhi divai nzuri mpaka sasa.ā€

Divai ni pombe.
 
Haya ni maoni yangu, hayana reference

Kwa mujibu wa uhalisia ktk maisha, pombe sio dhambi bali matokeo ya pombe hupelekea dhambi.

Mimi ni Mkristo ambaye si mfuasi wa papa, akina Lusekelo, mtume flani wala nabii x .

Sijawahi onja pombe na sitegemei kuonja kilevi kinachoenda kwa jina lolote la pombe.
 
Back
Top Bottom