Mzee wa Upako alimtabiria Raila ODINGA angeshinda uchaguzi

Mzee wa Upako alimtabiria Raila ODINGA angeshinda uchaguzi

Mchungaji Anton Lusekelo au kwa jina maarufu la Mzee wa upako tarehe 31 januari 2013 ,ndani ya kanisa lake alisema Raila Odinga ndiye angeshinda uchaguzi wa Kenya na Uhuru Kenyatta asingeshinda labda asubiri miaka ijayo na si kwenye uchaguzi huu.

Aliongea maneno haya kwa msisitizo na kurudiarudia sana na kwa mujibu wake utabiri huo alikuwa ameoteshwa na mungu wake.
Mwendawazimu huyo hana upako wa kweli wa Mungu,amebaki kuwa mtabili na mshauri mkuu wa CCM,na kupiga vita viongozi wenzake wa kiroho hasa wanapoonekana kuikosoa serikali wazi wazi.huyu ndiye aliyetoa ushauri kwa ccm,kutumia au kutotumia police kwenye mikutano ya cdm,na ndio matunda ya akina nape na mwigulu kuporomosha matusi kila wanaposimamama jukwaani kuilaani cdm,hata kama wananchi wanadai maji na shule safi wao wanatukana cdm tu.
 
.
Tofautisha kwanza kile ulichoita tofauti kati ya unabii na utabiri. Mbona hujafanya hivyo katika hii post yako? Hebu rudia kuisoma kwa makini.
.
Thank you...nime-edit comment yangu!
 
Mungu wake alimuotesha uongo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Namkubali saaana katika mafundisho yake, mambo ya ubashiri kama huo wa kenya kila mfuatiliaji wa siasa alikuwa na mtizamo wake. mimi binafsi sio mfuatiliaji saana wa mafundisho ya mchungaji huyu lkn mara chache ninapokutana na vipindi vyake kwenye tv hupenda kumsikiliza hasa anapokuwa anazungumzia hali za maisha kwa ujumla.
 
Mtabiri wa Chadema huyo!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
si kila atakaye liita jina la yesu ata iona mbingu,na wengine watatoa pepo kwa kutumia jina hilo ila lkn?.....
Bible;yesu anasema nawajua watu wangu kwa majina.
 
naona mzee wa upako aliishia kutabiri mshindi, akasahau kutabiri ''doctoring''
 
Kama alisema ameoteshwa na Mungu kuwa Odinga atakuwa Rais na hajawa,ebu tujiulize ni Mungu gani huyo?Wengine ni wajanja janja wanakuwa na hisia na mapenzi yao wanasingizia Mungu kawaonyesha.Siwezi kumzungumzia sana huyu eti mzee wa upako ,upako gani?Msimchezee Mungu atakuja kuwaambua kwa kuwapiga upofu.Namfahamu Lusekelo ni mbunifu wa kawaida tu haya ya kuoteshwa yametoka wapi?Acha ujanja ujanja rudi kwenye huduma
 
Hivi kwanini watu mnasahau kumpa mungu nafasi yake? Vile vile kwanini mnapenda kuingilia kazi ya mungu? Endeleeni tu Babu kwanywisha watu vikombe vya maji akidai dawa watu wakafa wengi tu, Sheikh Yahya kawadanganyeni kuwa eti Raila atashinda kashinda Kenyatta, Mchungaji Lusekelo na hivyo hivyo mnaingia chaka.

Jamani mambo ya kesho mwachieni mungu ndio pekee anayejua kitu gani kitatokea kwako au kwetu. Sisi wengine tunapiga matarumbeta tu!!!!
 
Sitorudi madhabahuni mpaka Augustine Mrema awe Rais - Zakaria Kakobe (mwaka 2000).
Jakaya kikwete ni chaguo la Mungu-Methodius Kilaini

N.B Nimeondoa vyeo vyao kwa sababu maalum
 
Mchungaji Anton Lusekelo au kwa jina maarufu la Mzee wa upako tarehe 31 januari 2013 ,ndani ya kanisa lake alisema Raila Odinga ndiye angeshinda uchaguzi wa Kenya na Uhuru Kenyatta asingeshinda labda asubiri miaka ijayo na si kwenye uchaguzi huu.

Aliongea maneno haya kwa msisitizo na kurudiarudia sana na kwa mujibu wake utabiri huo alikuwa ameoteshwa na mungu wake.

mkuu kitulo huko kanisani sisi hatukuwepo ungetuwekea clip tafadhali
 
Kwa wale wanaomfahamu Lusekelo hawatashangazwa na utabiri wake. Ni ujanjaujanja tu na kucheza na hisia za watu. Hebu jiulize ni vipi wengi wa wanaoanguka katika ibada zake ni kinamama. Soma historia uone jinsi Hitler alivyoweza kuziteka hisia za wanawake na mwisho kusaburuza watu wake katika vita ya pili ya dunia. Kibwetere hivyo hivyo. Tafakari na uchukue hatua.
 
Mchungaji Anton Lusekelo au kwa jina maarufu la Mzee wa upako tarehe 31 januari 2013 ,ndani ya kanisa lake alisema Raila Odinga ndiye angeshinda uchaguzi wa Kenya na Uhuru Kenyatta asingeshinda labda asubiri miaka ijayo na si kwenye uchaguzi huu.

Aliongea maneno haya kwa msisitizo na kurudiarudia sana na kwa mujibu wake utabiri huo alikuwa ameoteshwa na mungu wake.

Mungu wa huyu jamaa anatumia mfumo wa analogia uliotumiwa na yule nabii mzee aliyemrubuni na hatimaye kusababisha kifo cha nabii kijana.
 
Wanamfanya Mungu wa wakristo kunekana muongo.
 
Hii nadhani imekuwa biashara inayolipa sana hapa Duniani,
Huu ni udhalilishaji wa dini ya kikristo.
Amkeni watu wa Mungu.

Back
Top Bottom