My take.
Mtandao wa makanisa ya Lutherani na Katoliki ni mkubwa sana na umeenea karibu kila sehemu Tanzania.Madhehebu ya akina Mzee wa upako yako mengi sana lakini yako disorganise kiasi kwamba serekali inapata taabu sana jinsi ya kuwasiliana nayo.Utakuta mtumishi wa Mungu anaongoza kanisa lisilokuwa hata jengo [anatumia majengo ya shule] anajiita Askofu na anataka heshima anazopewa Askofu wa kanisa katoliki/Lutherani.Mwingine unakuta kaanzisha kanisa nyumbani kwake kaamua kujita nabii xyz,kanisa lake lina waumini 100 atataka naye kujifaninisha na kina Pengo au Malasusa kwa kweli serekali ipo sahihi kabisa.Makanisa mengine ukiyatazama kwa makini utagundua ni mali ya viongozi,makanisa ya jinsi mara nyingi yanasambaratika wakati viongozi wao wanapofariki au wanapojitokeza baadhi ya waumini wajuaji watakaohoji mambo ambayo viongozi/waanzilishi hawataki kuyaweka wazi.
Makanisa yanayoongozwa na kina mzee wa upako na Askofu Z Kakobe yatatetereka sana siku viongozi wake watakapotangulia mbele ya haki kwasababu misingi yake imejikita zaidi katika vipaji vya uongozi ukilinganisha na makanisa ya Lutherani na Katoliki.
Mzee wa upako ameenda mbali zaidi kwa kusema kwamba wahubiri wa makanisa ya Lutherani/Katoliki hawajui kuubiri wamebaki kubusu pete tu.Mimi ni muumini wa madhehebu ya Lutherani kila j2 na kwenda kanisani kusali kama ningekutana na mahubiri mabovu/hovyo kwa vyovyote ningekubali kupoteza muda wangu nadhani mzee wa upako kaamua kubwabwaja tu labda ana jambo lingine kaamua kulificha.
Huwa naamini katika maneno 100 ya mjinga basi naweza kupata moja au mawili ya kweli.
Ndugu Ngongo, point yako ya kuwa kuna makanisa disorganised sidhani kama ina mantiki hapa.Mzee wa upako anasema serikali inayakumbatia madhehebu ya wakatoliki na walutheran, na umekubali na kusema ni sahihi kabisa.
Kwanza nina wasiwasi sana urafiki huu wa serikali na haya makanisa, nasema nina wasiwasi, kwa sababu akina Malasusa leo ndio wasemaji wa Lowassa na wewe ni Mlutheri na ulikaa kimya, na katu hautamgusa Malasusa katika hilo. Kwa hiyo urafiki huu wa serikali na makanisa ni mbaya kwa maana ya kuwa makanisa yanatakiwa yawe makali kukemea ufisadi lakini kwa sababu ya hizo attention za hapa na pale basi wanakaa kimya.
Urafiki wa serikali na katoliki huwa unawaconfuse wengi kwani vatican ni serikali na wao ni wakatoliki, so usije kukuta hii notion ndio inawafanya wengi waamini serikakali inawakumbatia wakatoliki
Kwa kifupi uarfiki waserikali na makanisa ni wrong, kama serikali itasimama kama serikali, divide and rule ya viongozi wazembe serikalini huwa wanapitia kwenye hizi dini kuwapata walio wao. Ishu ya mahakama ya kadhi ni wazi ni failure ya JK kushindwa kuongoza na kutaka kufavour watu fulani, is the same concpet applies na huku kwenye haya madhehebu. KAnisa inabidi lisimame kama Yohana mbatizaji , Eliya, Shadrack, meshack and Abednego kukataa na kupinga maovu yote.
To my knowledge sijaona kama haya makanisa yamefika level ya juu kiasi cha kupendelewa na serikali, ila napata picha kwamaneno ya Lusekelo na confirmation yako.
Pili si kweli kuwa Lutheran na Katoliki ndio wana netwrok kubwa sana, sijaona ukilitaja Moravian,wasabato,SDA,Angalican, EAGT, TAG,FGBF,.Haya makanisa huwezi kuyadharau hata kidogo, si kwa population wala network.
Unawataja wa makanisa machanga kama ya akina Lusekelo ndio wako wengi zaidi, lakini hii haiipi kibali serikali kuwa iwape attention baadhi ya makanisa, serikali yetu haina dini kabisa. Bungeni tuna askofu Lwakatare hawa ni baadhi ya watu wenye single churches lakini wako powerful. Kuna akina Kakobe-style ya uongozi katika massive population kama ile si ya kuchezea, na ukiacha makanisa mengine mapya, huyu jamaa kanisa lake halina history ya ku-split, kanisa lake la DSM ndio kubwa kuliko yote EAST africa. Mwangalie Mwingira, Gamanywa n.k these are emerging but powerful churches ambapo wakisema wote waseek attention ya serikali ni mbaya sana. Na wanawachukua watu kutoka huko huko Lutheran and catholic, so organisation here without power is nothing!
Sasa imagine haya manisa yote yawe organised (kama unavyotaka ) and then wa seek attention ya serikali!!
Swala la watu kujiita maaskofu , manabii yatakuumiza kichwa as far as faith reigns. Tatizo ni kuwa the very same reformation that happens during Luther it is still going on! Kosa lilishafanyika zile zama za (dark ages) nadhani unafahamu. Kwa kifupi; haya makanisa mapya yanatokea wapi? si yanazaliwa kutoka kwenye existing churches? kuna nini humo mpaka wakimbie? whats wrong? utakuta ni mambo ya Imani.Problem ni kuwa kuna tatizo la kurithi hizi imani without exploring, nalo naliona kwako.Hujajua hasa ukristo na nafasi yake katika jamii.unachosema ni organisation zinazojiita za kikristo.Ndio maana kwa mfano kanisa la Lutheran unalosema liko organised ndio weak kabisa,Kanisa moja utamkuta mchungaji Mlokole na yuko strictly, na lingine utamkuta mchungaji mlevi na mzembe, within same church hakuna universal law ya kuwatambulisha walutheri,Leo hii kuna walutheri walokole na wasio walokole!
Mwisho, kwa knowledge yangu ya ulokole na walokole, sijaona sehemu yoyote katika biblia inayompa kibali Anthony Lusekelo aseme aliyoyasema.Biblia inasema Mungu atakupigania, atakuinua. Kwa hiyo haraka haraka hapa ni kuwa Lusekelo ameviolate divine rule ndogo sana ya kuwa Mungu ndie atakayempigania. Sasa napata picha who is he?
Kama anataka awe sawa na Lutheran, wakatoliki , basi he belong to the same group and class,Katika Biblia viongozi wa dini wako juu sana ya marais, simply kwa sababu walijaa nguvu za Roho mtakatifu na kuwa watakatifu kweli, Siku hizi tunaona maigizo ya vongozi wa dini. Hili ndio linasababisha makanisa kuzaliwa kila siku, If Lutheran and Catholic would have stood in the right path of God, kusingekuwa na huu utitiri wa makanisa. Believe me ndani ya Lutheran na Catholic still today kuna watu wamesimamia kweli ya Mungu.Ni hawa wachache tu akina Malasusa na Pengo ambao kwako unawaona wako sahihi!
Yes kuna ukweli wa walichosema na ukweli ni huu, serikali haina dini. urafiki huu ni wa nini?