Hivi tuwaulize unabii upo dsm tu? na waumini wapo dsm tu? au dsm ndo kuliko na dhambi tu? acheni utapeli fanyeni kazi, hawajamaa sijui watatufikisha wapi maana hawana huruma hata kwa waumini wao mf dec ni hao hao kina mzee wa upako, mi nawashauri kuweni na taratibu za kueleweka, kama katiba na kuwepo na chaguzi za kuchaguana zinazo julikana na kuondokana na umimi na kuwa nakanisa la waumini ambao ndo washika dau ambapo wana uwezo wa kukuondoa madarakani kwa njia ya domokrasia pindi utakapo kosea,pia acheni kuandika vitu majiana yenu tumieni jn la kanisa pia pesa ya kanisa isiwe inasainiwa na lusekelo pekeke yake kuwepo kamati,muda sina ila kama anasoma hapa anitumie e mail yake nitamsaidia kumshauri
Kaka hapa hawatakuelewa hata kidogo. Watasema unapingana na mpakwa mafuta wa Bwana. Yaani hawa walokole ni tofauti na watu waliookoka. Watu waliookoka ndiyo kanisa la Mungu Duniani, ni jambo la kiroho na wako kwenye madhehebu mbalimbali katoliki, lutheran, assemblies, sabato, na hata kwa lusekelo wapo lakini ni Mungu tu ndie anayewaona au kama mtu ni mtu wa Mungu anaweza kuwatambua au pia kwa matunda yao utawatambua.
Walokole sio watu waliookoka. Wao ni watu fulani waliopotoka kwa njia hatari. Ni mtego aliouweka ibilisi na kuutambua ni kazi ngumu mno. Labda nikupe hapa mambo machache yatukumbushe sote:
Mtu aliyeokoka anawapenda watu wote na kushirikiana nao bila kubagua sawa tu na 1 Korintho 13. Mlokole anajiona yeye peke yake ndo anamjua Mungu na wengine wote ni wachafu.
Mtu aliyeokoka anamwamini Yesu Kristo na kujua kuwa wakristo wote ni ndugu zake na ndiyo maana anaokoka na kumpokea Kristo kuwa Bwana na mwokozi wake hata kama ni mkatoliki. Na hana haja ya kuhama katoliki yaani kuokoka kwake kunamfanya awe mkatoliki mwenye udhati. Au mlutheri au mpentekoste mwenye udhati. Lakini mlokole kama yuko kwa Lusekelo anaamini kuwa wasio kwa Lusekelo wote wanaenda Jehanam. Jiulize hii ni akili au upupu.
Mtu aliyeokoka anaamini yeye ni binadamu na anaweza kutenda dhambi kwa hiyo hutubu na kusamehewa. Mlokole anaamini kuwa yeye si mtenda dhambi na ikitokea ametenda dhambi hutafuta mistari ya biblia kutetea tendo lake. Akizini husema bwana amemtuma kama vile Nabii Hosea alivyoagizwa kuoa malaya. Ndo maana kuna vijana wa kilokole wanawaona watu wa jinsia tofauti kama dhambi na huku kwa siri wanapiga puli.
Mtu aliyeokoka hujituma kufanya kazi kwa bidii, husoma kwa bidii, hulipa kodi kwa ukamilifu, huheshimu mamlaka zilizowekwa kwa kuwa hakuna mamlaka iliyopo ambayo haikuwekwa na Mungu, Hutii Bosi wake kama kumtii Kristo. Mlokole anaweza kumtukana Rais wa nchi, serikali, Baba na mama yake, wakubwa zake, mume wake au hata viongozi wengine wa kidini wasio dhehebu lake. Yeye mlokole mchungaji wake ndio yuko sahihi kuliko mtu yeyote duniani.
Kwa kifupi mlokole ni ndondocha. Anachoambiwa na mchungaji wake ndiyo Alfa na Omega. Hata Mungu akisema kitu tofauti na anachosema mchungaji ni mchungaji ndiye atasikilizwa na mlokole.
Ndiyo maana kuna kumeguka kukubwa kwa makanisa kama ya kina Lusekelo kwa sababu shetani anapomshambulia akili zake akaanza kukosea na kuanza kutoa pumba, hakuna wa kumuonya kama alivyofanya Paulo kwa Petro kiongozi wake, Yaani leo hii kanisani kwa Lusekelo yeye ni kama Mungu, Hakosei na ndivyo ilivyo kwa Kakobe, na ndio maana shetani akitaka kuyagawanya haya makanisa ni rahisi mno. Mara nyingi waliookoka huwa wanahama haya makanisa na wanabaki walokole wapotoshaji.
Ndiyo maana ni vigumu mno kwa haya makanisa kukua kufikia kwa mfano hata robo tu ya Roman Catholic Church. Wao akiambiwa jumapili hii wameudhuria watu elfu kumi anaridhika kabisa anafikiri amefanya kazi ya Mungu tayari. Na anajua yeye na familia yake mambo mazuri sasa.
Walokole wao kwao mafanikio( kama unabisha msikilize Lusekelo na Mwingira kwenye mahubiri yao), wao mafanikio ni kuwa na gari nzuri, nyumba, afya nzuri na kazi nzuri, mume au mke na watoto. Kwa mujibu wa mlokole ukishapata hayo basi.
Yaani tafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine yote mtazidishiwa wamesahau. Ndio maana wanang'ang'ania Mijini. Ni wachungaji wa mshahara. Mioyo yao inaangalia watu elfu kumi wahudhurie kanisani wapate sadaka. Ndio maana wanawaambia waumini wao mwezi huu hakikisha umeleta watu kumi. Hawaangalii mamilioni ya watu wanaopotea kwa kuikosa INJILI.
Hata matangazo yao ni biashara tu hayatofautiani na ya waganga wa kienyeji, ooh njoo Yesu atakupa mchumba, gari, utapona magonjwa, mtoto wako aliyepotea atarudi, utaondolewa mikosi, ndoto mbaya zitaondoka. Jamani afadhali hata ya mganga anayetumia ramli kuliko hawa maana hawa wanawaingia watu moyoni kabisa, wakiamini wanamsikiliza Mungu. Hawa ni kundi linalojulikana kama special agents of the Devil.
Soma urudie mahubiri yote ya Yesu mlimani Mathayo 5 yote 6 na saba. Yesu katika mahubiri ya mlimani anaonyesha kuwa kuna watu atawakataa siku ya mwisho ambao walihubiri kwa jina lake na kutoa pepo kwa jina lake na kwa jina lake kufanya miujiza mingi. Kwa hiyo madoido hayo yamewaondoa wakristo wengi makanisani kwao iwe RC, Lutheran, Anglican, SDA, TAG, EAGT na kwingineko na kukimbilia kwa kina Lusekelo kufuata madoido.
Sikiliza Biblia haisemi mtawatambua kwa matendo yao, inasema mtawatambua kwa matunda yao. Kuna tofauti kubwa sana kati ya matendo na matunda. Kwa taarifa yako wauaji na majambazi huwa na mwonekano wa matendo mazuri mno katika jamii unaweza kufikiri ni malaika.
Angalia Galatia 5:23 Inazungumzia nini juu ya tunda la roho. Haisemi ni miujiza, kutoa pepo la hasha ni Upendo, utu wema, upole, unyenyekevu, fadhili, kiasi, uvumilivu jamani mambo ya fujo tunayoyaona hayaonyeshi tunda la roho.
Ninachosema hapa ni kuwa kuna Tofauti kubwa kati ya Mtu aliyeokoka yaani mkristo aliyeokolewa na Yesu Kristo kama tu Mathayo 1:20-21 inavyoainisha na Mlokole ambaye natoa maana hapa chini:
Mlokole ni mtu aliyegeuzwa ndondocha na mchungaji wake kufuata uozo wowote anaoutaka mchungaji huyo bila yeye mwenyewe kuchambua hata kama uozo huo unampinga Mungu aliyemuumba kwa kisingizio cha kuokolewa na Yesu wakati siku ya mwisho Yesu atasema ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu, sikuwajua ninyi kamwe.