Mzee wa Upako aishukia serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee wa Upako aishukia serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Jan 12, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  MCHUNGAJI wa Kanisa la Gospel Revival Centre, Antony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako, ameishukia serikali na Idara ya Usalama wa Taifa kwa kukumbatia zaidi madhehebu ya Katoliki na Lutherani.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mzee wa Upako aliwaonya viongozi wakuu wa serikali kutoichezea amani iliyopo kwa kubagua madhehebu mengine yanayoitwa ya vichochoroni.

  Alionya kwamba ni rahisi kuipoteza amani iliyopo sasa kuliko kuitafuta, hivyo aliwataka viongozi wa serikali kuacha kuyadharau baadhi ya makanisa kutokana na ukweli kwamba wanaohubiri injili ni walinzi bora wa rasilimali watu katika kutunza amani ya nchi.

  “Makanisa ni kama makabila, hivyo kitendo cha serikali kuwapendelea zaidi baadhi ya viongozi wa dini ni kutishia ustawi wa amani iliyopo.

  “Serikali inalea sana makanisa haya, maaskofu wengine wanapewa passport za diplomat, wakipita popote hawakaguliwi, wakati wengine tukipita uwanja wa ndege pale tunakaguliwa hadi soksi…hii inaonyesha kwamba hawatuamini,” alisema na kuongeza kwamba sheria ya usajili wa makanisa ni moja hivyo anashangazwa na ubaguzi wa aina hii.

  Aidha, aliwatahadharisha viongozi wa serikali kukumbuka yaliyotokea Rwanda ambako kwa asilimia kubwa kanisa lilichochea mauaji ya kimbari hali iliyosababisha washitakiwa wakuu katika kesi ile kuwa viongozi wa dini.

  Huku akionyesha kujiamini sana, alisema vyombo vya usalama wa taifa vimelala na kwamba havitambui wajibu wao kutokana na ushauri mbaya hasa kwa upande wa madhehebu aliyosema huitwa ya kikanjanja kutothaminiwa.

  Mchungaji huyo ambaye makao makuu ya kanisa lake ni Ubungo Kibangu, jijini Dar es Salaam alisema pasi na shaka kwamba dharau ya viongozi wa serikali dhidi ya makanisa hayo imekithiri kiasi cha kutodiriki kujibu hata barua za mwaliko wanazopewa na wachungaji.

  Akitolea mfano aina ya ubaguzi huo, aligusia sakata la upitishwaji wa umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 132 kwenye Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lililo chini ya Askofu Zachary Kakobe.

  “Hili suala linalomsumbua Askofu Kakobe pale, kama umeme huo ungepitishwa St. Joseph akatoka Pengo kulalamika mngesikia Waziri Mkuu amekwenda na angemwomba kwa kumtuliza na mambo yangeisha, lakini sio Kakobe hadi leo anahangaika,” alisisitiza Mzee wa Upako.

  Katika hilo aliishauri serikali kumsikiliza Kakobe na kutafuta njia nyingine ya kumsaidia, na kwamba yupo naye bega kwa bega ili kuhakikisha suala hilo linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu.

  Aidha, alibainisha kwamba wanasiasa wote waliofilisika kisiasa wanakimbilia makanisani hivyo kutahadharisha upatikanaji wa rais ama viongozi wa kiserikali wasiostahili kutokana na shinikizo la viongozi wa dini wanaoonekana kuaminiwa zaidi na serikali huku usalama wa taifa ukiwa kimya.

  “Ni hao wanaopewa passport za diplomat ndio wanaoonekana viongozi wa dini, wametusahahu kabisa sisi. Huku tunakoelekea tutawekewa rais hata kichaa kwa sababu tu amepitia kwao.

  “Haya makanisa mnayoyaona yana watu wengi mkitoka nje ya mipaka yetu hayana waumini. Yanaheshimika hapa tu, hawajui kuhubiri hadi wawashe mishumaa. Wataishia kubusu pete za viongozi wao huko nje,” alisema alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari.

  Hata hivyo, aliweka wazi mapenzi yake kwa Rais Jakaya Kikwete na kusema anatamani aendelee kuongoza Tanzania. “Binafsi mimi kama Lusekelo, namfagilia Rais Kikwete, natamani aendelee kuongoza,” alisema.


  Source: Tanzania Daima.

  My take.

  Mtandao wa makanisa ya Lutherani na Katoliki ni mkubwa sana na umeenea karibu kila sehemu Tanzania.Madhehebu ya akina Mzee wa upako yako mengi sana lakini yako disorganise kiasi kwamba serekali inapata taabu sana jinsi ya kuwasiliana nayo.Utakuta mtumishi wa Mungu anaongoza kanisa lisilokuwa hata jengo [anatumia majengo ya shule] anajiita Askofu na anataka heshima anazopewa Askofu wa kanisa katoliki/Lutherani.Mwingine unakuta kaanzisha kanisa nyumbani kwake kaamua kujita nabii xyz,kanisa lake lina waumini 100 atataka naye kujifaninisha na kina Pengo au Malasusa kwa kweli serekali ipo sahihi kabisa.Makanisa mengine ukiyatazama kwa makini utagundua ni mali ya viongozi,makanisa ya jinsi mara nyingi yanasambaratika wakati viongozi wao wanapofariki au wanapojitokeza baadhi ya waumini wajuaji watakaohoji mambo ambayo viongozi/waanzilishi hawataki kuyaweka wazi.

  Makanisa yanayoongozwa na kina mzee wa upako na Askofu Z Kakobe yatatetereka sana siku viongozi wake watakapotangulia mbele ya haki kwasababu misingi yake imejikita zaidi katika vipaji vya uongozi ukilinganisha na makanisa ya Lutherani na Katoliki.

  Mzee wa upako ameenda mbali zaidi kwa kusema kwamba wahubiri wa makanisa ya Lutherani/Katoliki hawajui kuubiri wamebaki kubusu pete tu.Mimi ni muumini wa madhehebu ya Lutherani kila j2 na kwenda kanisani kusali kama ningekutana na mahubiri mabovu/hovyo kwa vyovyote ningekubali kupoteza muda wangu nadhani mzee wa upako kaamua kubwabwaja tu labda ana jambo lingine kaamua kulificha.
   
 2. bht

  bht JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hasira zote hizi ni kwa kutopata attention ya sirikali tu au kuna lingine!!! sasa wakatoliki/Lutherans wamemkosea nini hapo!!??

  kweli Yesu biashara siku hizi!!!
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Hawa ndio wale wale, ila huyu jamaa bado ana afadhali kidogo, bado hajaota mapembe na kutoa makucha. Mwenzake mapembe tayari na makucha nje nje kusubiri mparurano.
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Kanisa la Gospel Revival Centre linajulikana kwasababu kaamua kutumia channel 10.Juzi juzi nilikuwa natazama kipindi chake anataka tumchangie 100,000/= au zaidi umtajie mambo yako matano akuombee.Kwa maana hiyo basi usipokuwa na hizo 100,000/= hawezi kukuombea kweli siku hizi Yesu kawa biashara nzuri.
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umesema ukweli kabisa juu ya mambo haya ya ajabu juu ya imani nyingine za makanisa ya kisasa kama hivi
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  [/quote]Au umepotoshwa au umepotosha wewe.

  Hakuna Dhehebu ambalo halikuwa na muasisi na yote yamesimama kwenye nguzo za hao waasisi.

  Hakuna dhehebu lililoanza na likawa na jengo lake kubwa la kifahari siku hiyo hiyo.

  Hata hayo majengo unayoyaona mazuri ya makanisa unayoshabikia yako mijini zaidi lakini vijijini majengo wanayotumia waamini wao ni duni kama vile vibanda vya kuku wa kienyeji.

  Kwa sababu hiyo muasisi akishaanzisha hata akifa Mungu aliyempaka mafuta afi. Ndio sababu madhehebu yote haya pamoja na lako bado yapo na mmejibebea misifa.
   
 7. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mzee wa upako ni aina ya viongozi watakaokuja kutupa shida ikiwa serekali itakubali kumwachia aendelee kuongea mambo ya kutugawa.Hana maana kwanza ukisiliza mahubiri yake Chenel ten unaweza kushangaa, ni mahubiri ya kibiashara kwa asilimia mia.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hivi huo upako ndo ukoje wajameni??
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hebu tufumbue macho..Mahubiri ya kibiashara kivipi??
   
 10. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Duh amani inaletwa na mungu mwenyewe wewe umeanza kuhubiri juzi juzi tu ila amani tanzania ipo miaka yote , Mzee wa upako unatakiwa kujenga taasisi imara ambayo itakuwezesha kuonekana imara kama walivyofanya walutheri na wakatoliki vimginevyo utaendelea kupiga ukelele mimi huwa nafuatilia maombezi yake sana mwaka juzi alikuwa akimshambulia kakobe sana kwa kitendo chake cha kuwakataza waumini wake kujipendezesha hiyo ilikuwa ni baada ya kakobe kumbeza mzee wa upako kwa kuendesha maombi ya kuleta utajiri hivyo anaweza kuona kuwa wao bado hawajakomaa kuweza kuaminiwa wanavyotaka kwani hata wenyewe hawaheshimiani.

  Hata ukianzisha leo benki hauwezi kupewa nafasi sawa na benki kongwe zilizo
   
 11. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbona povu linakutoka au ni wale wale nini.Kwa taarifa yako majengo ya makanisa mengi (lutherani/katoliki) ni mazuri hata huko vijijini.Makanisa ya kina mzee wa upako yako Dar tu ukienda vijijini hawajulikani na ukichunguza kwa makini waumini wa mzee wa upako / kakobe wengi wamechanganyikiwa,wamepoteza dira ya mwelekeo wa maisha,wamekata tamaa.Nina wasiwasi hata wewe ni mmoja wao.
   
 12. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Soma post No# 4 & 10.
   
 13. bht

  bht JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  unaombewa na mtu mwenye uwezo huo kama mzee wa upako n akisha unapokea muujiza wako!!!
   
 14. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  jamani hizi hasira ni kwakukosa diplomatik pass au kuna mengine ukiona serikali aijakujali ujue mda wako bado ucjikweze kwann yy anataka kujikweza hilo ndo tatizo umefungua kanisa leo leo unataka upewe heshima sawa na aliyefungua kanisa miaka 50 na ulikuwa unasali ukouko kweli hii ni haki nashangaa aina hii ya watumishi kweli serikali isikae kmya
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Post #10, sijaona kama inazungumzia 'mahubiri ya kibiashara', labda mwenzangu kama wewe unayaona.

  Post #4 inazungumzia kumchangia (hata mwenye kupost hasemi mchango huo unamakusudio gani huenda hapa ingefunua zaidi ili sisi wengine from neutral persepective tujue pumba na mchele) sijaona kama kuna precondition kuwa kama hutoi hiyo hela hatakuombea.
   
 16. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  tafadhali rekebisha kauli yako akuna aliyeokoka ambaye amechanganyikiwa pls omba radhi kwa hilo
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Loh, kumbe. Kwa hiyo muujiza ndo upako?
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Humu ndani kuna watu wanamajibu ya kejeli kwelikweli halafu wanajiita wakristu. Hivi kuna mtu aliyeomba kuwa na shida hapa duniani??
   
 19. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa is yearning for govt. attention na ndio maana anazungumzia hata mambo ya DIPLOMATIC passport na kukaguliwa kiwanja cha ndege.Juu ya yote kwa kumalizia anajikomba kwa Jakaya eti angependa aendelee kutawala!! Huko kote ni kuganga njaa tu .Kujifananisha na makanisa yenye waumini dunia nzima na kanisa lenye waumini kiduchu ni kutokuwa makini katika hoja inayojengwa!!
   
 20. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Huyu Mzee wa Upako (na kweli anajua kupakaza!)

  Ana matatizo maalum. Ipo siku watanzania tutakuja kushtushwa na mambo yake kwa kuchelewa. Siku moja aliomba hela mwishoni mwa program yake. Nikapiga simu kuomba account namba yake ya benki. Akapokea simu na kunipa namba. Nikamwuliza jina la account, akasita kutaja na kusisitiza "wewe weka fedha, jina la account litajileta". Nilipombana akasema jina "Anthony Lusekelo". Nikamwambia mimi nataka kuchangia kanisa siyo mtu, akakata simu. Hapa TRA inabidi watusaidie.

  Lakini pia ana tatizo la kupenda ukuu na ndiyo maana analalama kunyimwa diplomatic passport na kutopitia VIP.

  Channel ten wanampa free airtime ili kutukana madhehebu mengine na kuyagawa. Wakati wa sakata la msamaha wa kodi aliweka kipindi maalum ili kuwatukana maaskofu kwa kusema "nani aliwatuma kujenga mashule na mahospitali?"

  Nafuu sana ya Mtikila, siyo huyu anayeweka bei ya sala na baraka.
   
Loading...