Mzee wa Upako aishukia serikali

Kanisa la Gospel Revival Centre linajulikana kwasababu kaamua kutumia channel 10.Juzi juzi nilikuwa natazama kipindi chake anataka tumchangie 100,000/= au zaidi umtajie mambo yako matano akuombee.Kwa maana hiyo basi usipokuwa na hizo 100,000/= hawezi kukuombea kweli siku hizi Yesu kawa biashara nzuri.
hahaha mbona hiii huwa anaitoa kwenye mikutano yake,kuna jamaa zangu huko shinyanga walijaza fomu na laki wakatoa,niliwaambia wanaibiwa tu juhudi zao ndo zinafanya wafanikiwe,by the way kwani wao wanashindwa kuomba hadi mzee upako sijui awaombee tena na hela juu,huyu mwizi kwa kweli na watu wanaingia mkenge.
 
jamani dini inatumika vibaya siku hizi!!!! sasa mama 5j, wajiombee wenyewe kwani wana upako??? si mpaka mzee mwenyewe aliyetunukiwa uwezo huo awasaidie!!!!
 
jamani dini inatumika vibaya siku hizi!!!! sasa mama 5j, wajiombee wenyewe kwani wana upako??? si mpaka mzee mwenyewe aliyetunukiwa uwezo huo awasaidie!!!!
hahaha kumbuka nae ni binadamu kama wao,mpaka wanajaza fomu tena kwa malipo,fikiria yeye anapoomba ujibiwe maombi yako analipa kwa MUNGU ili maombi yajibiwe?hilo laki moja ya nini wakati yeye hamlipi MUNGU anapoomba maombi ya watu yajibiwe.

Mungu anajibu maombi weka bidii panga mikakati jinsi ya kuyatatua hayo unayomwandikia A.LUSEKELO NA KUMLIPA PESA.Then plus sala mambo yatakwenda.
 
Huyu Mzee wa Upako (na kweli anajua kupakaza!)

Channel ten wanampa free airtime ili kutukana madhehebu mengine na kuyagawa. Wakati wa sakata la msamaha wa kodi aliweka kipindi maalum ili kuwatukana maaskofu.

Nafuu sana ya Mtikila, siyo huyu anayeweka bei ya sala na baraka.
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni, kipindi siyo free, analipia, sio free, tena hela ikiongezeka atatia timu na Star TV. ITV na TBC wanakataa kupokea vipindi vya watu wa wokovu.

Sio tuu analipia airtime, japo anamiliki studio yake, lakini bado analipia cameramen na editors, producer ni yeye mwenyewe, no wonder sometimes poor production maana kuwa producer ni professional ya watu kama ilivyo kuhubiri.
 
Wazawa nadhani hamna ulazima sana ku quote li habari lote unapo toa maoni yako, kwa tunaelewa ni habari gani inazungumziwa,...., tuwe wachumi kidogo! Hii ni kwa post zote.
 
mkuu Pasco asante kwa kunifumbua macho hapo kwenye bold!!!
 
Hakuna cha upako wala ufutaji, huyo mzee wa mpako kama anvojiita anatoka kule kule kwenye madhehebu 700 mkoa mzima.Uaskofu kajipa mwenyewe sasa anategemea serikali imfanyie nini zaidi?alale mbele huko tena asituchafulie amani yetu!
 
Au umepotoshwa au umepotosha wewe.
Hakuna Dhehebu ambalo halikuwa na muasisi na yote yamesimama kwenye nguzo za hao waasisi.
Hakuna dhehebu lililoanza na likawa na jengo lake kubwa la kifahari siku hiyo hiyo.
Hata hayo majengo unayoyaona mazuri ya makanisa unayoshabikia yako mijini zaidi lakini vijijini majengo wanayotumia waamini wao ni duni kama vile vibanda vya kuku wa kienyeji.
Kwa sababu hiyo muasisi akishaanzisha hata akifa Mungu aliyempaka mafuta afi. Ndio sababu madhehebu yote haya pamoja na lako bado yapo na mmejibebea misifa.

Heshima kwako Mchukia Ufisadi,

Mkuu wangu labda umeshindwa kunielewa hoja yangu.

Ukiangalia historia ya kanisa kama Lutheran mwanzilishi wake Martin Luther alitofautina na uongozi wa kanisa katoliki,alkuwa na sababu za msingi ambazo hata leo bado zinasimama.Miaka hiyo waumini wa kawaida kanisa katoliki hawa kuwa na access ya kusoma biblia,ni Martin Luther alianza kutafsiri agano jipya kwa kijeruman hiyo ilikuwa mwaka 1522 na baadae alitafsri biblia yote kazi ambayo ilichukua miaka kumi.Kazi aliyofanya Martin Luther ilikuja kusababisha biblia ikapata tafsiri kwa lugha mbali mbali,kama si yeye pengine tungekuwa tunalazimishwa kusoma biblia kwa lugha ya kirumi tu kitu ambacho si kizuri.

Mzee wa upako kamwe hawezi kusimama jukwaa moja na mtu kama Martin Luther ambae wakati wake aliweza kupambana na sheria kali za kanisa ambazo zilikuwa kinyume na mafundisho ya Mungu.Ukifuatilia mafundisho yake channel 10 yamejikita zaidi kuwaokoa watu wenye uwezo,kitu ambacho kwenye biblia hakuna.Sijaona andiko kwenye biblia takatifu mtu alitakiwa kuokolewa au kuombewa baada ya kutoa fedha.Mafundisho ya mzee wa upako pia ni kwaajili ya kuwachukua watu kutoka madhehebu mengine ambao tayari wameshamjua kristo kuwa ni mwokozi wa maisha yao,Mzee wa upako alitakiwa na bado anayo nafasi ya kwenda vijijini ambako wako watu wengi wanaohitaji kumjua kristo.Mzee wa upoko alinishangaza sana alipokuwa anatetea uanzishwaji wa mahakama ya kadhi kupitia kipindi cha Makwaia wa Kuenga [Je tutafika] ndipo nilipomstukia yuko kwaajili ya maslahi binafsi.
 
Wazawa nadhani hamna ulazima sana ku quote li habari lote unapo toa maoni yako, kwa tunaelewa ni habari gani inazungumziwa,...., tuwe wachumi kidogo! Hii ni kwa post zote.

haaaa unaogopa karatasi zitaisha!!!!! (just kidding)
 
Huyu Mzee wa Upako (na kweli anajua kupakaza!)

Ana matatizo maalum. Ipo siku watanzania tutakuja kushtushwa na mambo yake kwa kuchelewa. Siku moja aliomba hela mwishoni mwa program yake. Nikapiga simu kuomba account namba yake ya benki. Akapokea simu na kunipa namba. Nikamwuliza jina la account, akasita kutaja na kusisitiza "wewe weka fedha, jina la account litajileta". Nilipombana akasema jina "Anthony Lusekelo". Nikamwambia mimi nataka kuchangia kanisa siyo mtu, akakata simu. Hapa TRA inabidi watusaidie.

Lakini pia ana tatizo la kupenda ukuu na ndiyo maana analalama kunyimwa diplomatic passport na kutopitia VIP.

Channel ten wanampa free airtime ili kutukuna madhehebu mengine na kuyagawa. Wakati wa sakata la msamaha wa kodi aliweka kipindi maalum ili kuwatukana maaskofu kwa kusema "nani aliwatuma kujenga mashule na mahospitali?"

Nafuu sana ya Mtikila, siyo huyu anayeweka bei ya sala na baraka.

Heshima kwako Baija Bolobi,

Hapa ndipo ninapotofautiana na Mzee wa upako yaani anataka kuturudisha nyuma kwenye ile miaka 1500.Kuna mafundisho ya wakati huo waumini walitakiwa kutoa fedha kwaajili ya kuwaombea marehemu [ndugu zao waliokufa zamani]wakiamini kufanya hivyo kutawapeleka ndugu zao peponi bila kujali wakati wa uhai wao walitenda nini.Tukiendelea kumwacha Mzee wa upako afanye atakavyo iko siku ataka kodi zetu zitumike kulipia gharama za vipindi vyake visivyo na tija ya kiroho.
 
Hapa ni kuganga njaa tu! Mzee wa upako ni mfanyabiashara kama wafanyabiashara wengine, yaani ameona sadaka hazitoshi mpaka aanze kuwaombea watu kwa malipo?
Kama anataka kujenga kanisani achangishe waumini wote siyo wenye shida.
Wakati bibilia inaelekeza matajili wauze mali zao ili kusaidia masikini, yeye anaelekeza watu wamchangie ili wawe matajiri, huyu Askofu wa aina hii inabidi achunguzwe
 
Huwezi kuzaliwa na kukimbia siku hiyohiyo! hiihaijawahi kutokea. Huyu Jamaa Lusekelo ni mgomvi sana sijawahi kuona acha kule kuwa kiongozi wa Dini hata angekuwa Muumini wa kawaida tu anastahili kuwekwa Segelea ndipo atachunga kauli za midomo yake maana yeye kutukana tu ndo kumemjaa. Sasa kanisa lake hata jina nashindwa kulikumbuka ndio lifanane na makanisa mengine? ana masihala makubwa huyu!!!

Na huyu Jamaa ni Mlutheri kabatizwahuko na kupata kipaimara hukohuko! akiwa Iringa na sasa kaanza majungu Sijui kama huwa asoma JF lakini tungependa kuwambia kuwa anyamaze atakimbiza hata hao wateja wake ambao ni waumini. Maana anayoyasema anajitukanisha hata huyo Kakobe anaesema nae ni Mkatoriki aliyebatizwa Kigoma na kupata komonio ya kwanza na ya pili kwenye kanisa hilohilo.

KAMA ZAWADI YA KUSEMA SANA NI FEDHA BASI ZAWADI YA KUKAA KIMYA NI DHAHABU.
 
sasa jamani kwa nini lawama zinamwangukia mzee wa upako kwa kuwatoza watu pesa ili awaombee.
je na hao wanaoridhia kumpa pesa?? maana hajamkaba mtu akamlzaimisha bali ni uamuzi wa mtu binafsi.
 
Hapa ni kuganga njaa tu! Mzee wa upako ni mfanyabiashara kama wafanyabiashara wengine, yaani ameona sadaka hazitoshi mpaka aanze kuwaombea watu kwa malipo?
Kama anataka kujenga kanisani achangishe waumini wote siyo wenye shida.
Wakati bibilia inaelekeza matajili wauze mali zao ili kusaidia masikini, yeye anaelekeza watu wamchangie ili wawe matajiri, huyu Askofu wa aina hii inabidi achunguzwe

Heshima kwako Mtumiabusara.

Kwa kweli unaonekana una busara kama lilivyo jina lako.Mzee wa upako ni mfanyabiasha kama walivyo kina R Mengi,manji na nk tofauti hapa ni ndogo sana mzee wa upako antumia mwavuli wa dini kuficha biashara zake pengine kukwepa kulipa kodi ya kaisari.
 
Maatizo ya Lusekelo:

1. Uchu wa Mali

2. ''Ucheki bob''

3. Elimu Dunia ndogo sana

4. Elimu ya Mungu (dini) ndogo sana

5. Inferiority complex- kazaliwa Mbeya anasema kazaliwa Iringa

6. Kuhubiri kwa mashindano

7. Kujikomba kwa wanasiasa

8. Wivu kwa huduma za wenzie

Ushauri.
Kama unataka diplomatic passport fanya kile hao maaskofu wengine walicho fanya kupata hizo passport maana serikali haikuwapelekea hao maaskofu bali maaskofu ndo waliozitafuta.
 
Huyu mtumishi wa Mungu aliniacha hoi nilipomuona kwenye luninga akisema namnukuu "Weka shilingi laki moja katika akaunti nitakayokutajia sasa, ksiha tuma maombi yako kumi kwa njia ya meseji" Sasa mi nikabaki kujiuliza ina maana hapa kila ombi unalipia elfu kumi ama? kweli ndio maana vijana wa siku hizi wameacha kwenda makanisani.
 
Heshima kwako AmaniGK,

Mzee wa upako ana maubiri yanayotiashaka ukristo kuliko mataifa wanaodai Yesu hakusulubiwa msalabani.
 
tatizo kila siku makanisa yanazaliwa hii serikali itayapa attention makanisa mangapi?
 
Maatizo ya Lusekelo:

1. Uchu wa Mali

2. ''Ucheki bob''

3. Elimu Dunia ndogo sana

4. Elimu ya Mungu (dini) ndogo sana

5. Inferiority complex- kazaliwa Mbeya anasema kazaliwa Iringa

6. Kuhubiri kwa mashindano

7. Kujikomba kwa wanasiasa

8. Wivu kwa huduma za wenzie

Ushauri.
Kama unataka diplomatic passport fanya kile hao maaskofu wengine walicho fanya kupata hizo passport maana serikali haikuwapelekea hao maaskofu bali maaskofu ndo waliozitafuta.

diplomatic passport haiji kwa kuubiri pale ubungo peke yake....lazima zaidi ya mahubiri atoe na huduma za jamii kama watoto yatima,afya[mahosipitali],shule za awali hadi vyuo vikuu,.....tatizo wahubiri wengi wanakazana kuhubiria roho tu..bila kujenga mwili ulio beba roho......pesa wanapata nyingi sana ...za sadaka ..lakini hawatoi huduma za jamii..

kuna yule mwingine pale ubungo ....amenunua HAMMER anaendesha gari la milioni 300 ...wakati kanisa lake liko in shambles like a make shift....watu wanasali kwenye jengo linaloweza kuanguka wakati wowote.....ukumbi una gorofa la mbao za mpodo...watu wanakaa kwa mamia...linaweza kuanguka anytime....pesa wanatoa nyingi lakini sijui kwa nini hataki kujenga jengo lenye viwango vya kihandisi...anabaki kuendesha hammer.......sasa serikali ikiingilia kati na kulifunga jengo lake kwa kuwa linahatarisha maisha .....utasikia analalamika ameonewa ....
 
Back
Top Bottom