Mzee Rukhsa: Safari ya Maisha Yangu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
MZEE RUKHSA: SAFARI YA MAISHA YANGU
Leo nimeingia Maktaba nikawa naangalia makala ambazo nimeandika kuhusu mambo tofauti ya serikali wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Kilichonifanya nifanye hili ni kule kusoma sehemu za kitabu cha Mzee Mwinyi na katika kusoma huko kukanikumbusha baadhi ya matukio muhimu ambayo yalinisukuma kuandika makala wakati mwingine katika magazeti ya nje kama inavyoonekana katika picha - Africa Events na New African yote majarida yakichapwa London na wakati mwingine tukiandika katika magazeti yetu ya ndani.

Hapa nitacheka kidogo kwani ujana hakika una raha zake, wakati mwingine tukiandika kutoka ''msituni.''

Kwa hakika kipindi cha utawala wa Mwinyi hakupungukiwa na watu waliokuwa wanaona raha kumshambulia.

Ilisikitisha kuwa kulikuwa na magazeti yalimpa nafasi Reverend Mtikila kumshambulia Rais.

Kuna baadhi ya vijana wa wakati ule waliona wana wajibu na dhima kubwa ya kumtetea Rais pale ilipodhihiri kuwa hakuwa na mtetezi.

Nilikuwa mmojawapo wa vijana walioamua kumtetea Rais Mwinyi.

Namsoma Rais Mwinyi, ''Mzee Rukhsa Historia ya Maisha Yangu,'' na natingisha kichwa kwa mengi ninayokutananayo.

Natingisha kichwa kwa kuwa baadhi ya matukio na mambo yaliyomo kitabuni mimi na wenzangu tuliyafahamu kwa undani na tuliyaandika kwa yale yaliyostahili kuandikwa na mengine tuliyanyamazia.

Ninapotembea katika Maktaba hakika inanikumbusha mengi na kuwaleta wenzangu wengi tuliokuwa pamoja baadhi wameshatangulia mbele ya haki.

Maktaba inanikumbusha watu muhimu sana wa nyakati zile kama Augustine Mrema Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Waziri Mkuu, Sheikh Kassim bin Juma Imam Mkuu wa Msikiti wa Mtoro na Mchungaji Christopher Mtikila Muasisi na Kiongozi wa Full Salvation Church.

Hakika zile zilikuwa nyakati za aina yake.

1658167206670.png
1658167277209.png
1658167304653.png
 
Back
Top Bottom