Mzee Pwagu hatunaye tena

Tumsifu Samwel

JF-Expert Member
Jul 30, 2007
1,407
159
Aliyekuwa msanii wa kaole MZEE PWAGU amefariki dunia nusu saa iliyopita katika hospital ya Amana jijini Dar es salaam. Habari kamili mtaendelea kufahamiswa....! MUNGU amlaze mahari pema peponi....!

2425940.jpg

Rajab Kibwana Hatia al maaruf Mzee Pwagu
 
duuh mungu amlaze mahali pema peponi na asante zangu kwake kwa kazi nzuri ya sanaa aliotupa wakati wa uhai wake.
 
hahaa,uyu jamaa si nimemsoma sasa ivi anasema anataka kuondoka alikuwa anawaomba mods wamuondolee ID yake..kujilipua kususa na boycott imeshindikata mzee? namwongelea CarthbertL....

POLE KWA WAFIWA, BWANA ALITOA, NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
 
A legend indeed.. na kama kawaida yetu watu kama hawa waliochangia kwa kiasi kikubwa katika ulimwengu wa burudani hatuwaenzi hadi wanapotutoka.

Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi Amin, na awafariji famili, ndugu na jamaa wote katika wakati huu wa huzuni na maombolezo.
 
Aliyekuwa msanii wa kaole MZEE PWAGU amefariki dunia nusu saa iliyopita katika hospital ya Amana jijini Dar es salaam. Habari kamili mtaendelea kufahamiswa....! MUNGU amlaze mahari pema peponi....!

Utatufahamishaje na wewe umeomba akaunti yako na post zako zifutwe?

Mungu amlaze mahali pema peponi.

Wengine hatumjui, mwenye picha aweke tafadhali
 
katika wazee nawaheshimu kwenye sanaa ni huyu na jangala,mzee small na majuto na bi chau.basi na mwingine yule sijui muhogo mchachu kidogo nawakubaali sana,wanaigiza kiuhalisia kabisa,kama pwagu kafa ni jambo la kusikitika kwa kweli maana sijui kwanini hawa kina kunumba hawawaoni wazee kama hawa kufanya nao muvi hizo,labda wanataka pesa nyingi,lakini hawa wazee wanajua jinsi ya kufanya comedy for real.
 
Hakika tu wapitaji ktk ulimwengu huu. Msiba hauzoeliki, poleni wafiwa. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana na libarikiwe
 
Hakika tu wapitaji ktk ulimwengu huu. Sisi tu mavumbi na mvumbini tutarejea, maana tulitwaliwa huko.
Msiba hauzoeliki, poleni wafiwa.
Bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana na libarikiwe
 
Nenda mzee Pwagu.
Kapumzike kwa amani mzee wangu.
Kazi yako bado itaendelea kuheshimika ingawa haupo nasi tena.
 
RIP Mzee Pwagu. Poleni wafiwa. Mungu akupeni moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
 
Poleni wafiwa, Mungu ailaze mahali pema peponi, Amin.

Basata mna mpango gani wa kumuenzi gwiji huyu wa sanaa za maonyesho Tanzania????
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom