Mzee Mwanakijiji vs Waziri Abadallah Kigoda.

Pwito now you talking.
Nani aliyesema kuwa waandishi wa habari ni house made hivyo hawastahili kulipwa? Ni nani huyo aliyesema nafasi ya uwaziri house wife hivyo wanastahili maslahi makubwa? Je alitumia vigezo gani kufikia uamuzi huo? Je, wakati tunapohama toka karne ya Viwanda na kuingia information age hivyo vigezo bado vina tija?

Shida iko wapi, muingizeni kwenye payroll ya cdm si mnapata ruzuku? mchango wa mwanakijiji zaidi ya kwenye cdm kwa wananchi wa kawaida haujulikana na haujaonekana bado
 
Aweda,

Huwezi fananisha nanasi na ndizi.

Mwanakijiji kumfananisha na Abdallah Kigoda ni kama kufananisha Mbingu na Ardhi.

Nini cha maana na cha akili alichofanya Mwanakijiji zaidi ya majungu na fitna za mitandaoni?

Abdallah Kigoda on the other hand, ni mmoja katika watu mahiri sana na "he is a born leader".

Born leader?!!! kwa lipi? acheni kuandika tu kisa mna bandwidth za kuchezea
 
Ok. Nimekuelewa. Kumbe unataka waandishi wa habari wapate heshima wanayostahili. Naunga mkono, lakini... Mimi ni mwanasheria, wakili wa kujitegemea, na kwa bahati mbaya/nzuri sijaajiriwa serikalini. Naomba nitambuliwe kwa ni natoa mchango mkubwa kutetea haki za wananchi
Mimi ni daktari, sijaajiriwa serikalini, lakini nina hospitali yangu. Naomba nitambuliwe kwa sababu ninatoa mchango kwa jamii.
Mimi ni dereva wa daladala, naendesha mamia ya watu kila siku kutoka temeke hadi muhimbili. Kwa bahati mbaya sikuajiriwa serikalini. Naomba nilipwe na serikali kwa sababu natoa mchango mkubwa sana kwa jamii...

Bwana Mikael P Aweda naomba unitetee popote utakapoweza nami niatmbuliwe...

Kuhusu kuyaingiza hayo kwenye katiba bwana Mkaili, nilishakwambia; Katiba ni document ya kuwalinda na kuwatetea watawala dhidi ya watawaliwa... Kama unataka waandishi wa habari wawe watawala sawa...

Mkuu tuko nimekupata,
Umenipa changamoto nzuri sana.Hoja yangu ni kwamba kutokana na unyeti wa sekta hii ya habari ingekuwa vizuri tukaipa uzito fulani. Kwa namna gani sote tuumize vichwa vyetu. Kuna walimu walioajiriwa kila kona, na kuna wanasheria kila wilaya. Nadhani tungekuwa na wanahabari pia kila wilaya in the long run.
 
Wakurogwa,
Nadhani hujanielewa hata kidogo. Mimi sijasema kwamba Mwanakijiji au waandishi wa habari walipwe mishahara na posho sawa sawa na wabunge, mikopo mil 90 nk. Hapana. Inafahamika kuwa ktk nchi hii kila mtu analipwa mshahara kulingana na kazi anayofanya na ngazi aliyopo. mwl mkuu wa shule na mfanya usafi hawalipwi sawa. Swali ni je, ngazi ya waandishi wa habari kwa ujumla wao ndani ya nchi iko wapi? Na je, waandishi wa habari hawana mchango ktk taifa hili? kama wabunge, walimu na madaktari tunawalipa vipi kuhusu wao?
Mikael P Aweda, mambo mkuu kwanza kabisa long time not seen anyway tutawasiliana baade.

coming back to the point, ni vigumu sana kusema eti Tz watu wanalipwa kulingana na kazi wanayofanya, mfano hapa tz utaona watumish asiokuwa kwenye nafasi za kisiasa ndio wanaolipwa mishahara midogo kuliko walioo kwenye nafasi za kiserikali kwa maana ya nafsi za kisiasa. Mimi hainiingii akilini eti mwalim anakwenda kusahihisha mitihani ya wanafunzi 350000 kwa muda wa wiki mbili halafu unampa laki 4 tu. wakati huohuo kuna mtu anasafiri kwenda kwenye ziara za kikazi hiyo sh 4 ni hela ya mafuta ya gari tu.

sitaki kuamini kuwa waziri kwenda kukagua mradi wilayani kuna umuhimu kuliko huyu anayekaa kusahihisha mitihan, ndani ya fume chamber tena akiwa ametengwa na familia yake wala uhuru wa kuwasiliana nao hana. Hili naliongea kwakua nina uhakika nao.

ukiwaza swala la waandisha wa habari nafikir vyombo husika kama waajir wao wanapaswa kutambua mchango wa kila mmoja japo kuwa kweli ni kwamba serikali haijali watumish wake hasa walioko katika technical operations. anyway waache wao wenye visu wale nyama sisi wenye mikono tufute meza but haya yanamwisho tu ingawa sion kama katiba ndio mwisho wao kuna laziada linalohitajika ambalo ni mapinduzi ya dhati tena yale ambayo enzi zile tulisemaga hayaji ila kwa mtutu.
 
Last edited by a moderator:
Tukielewa vyema maana na tofauti ya maneno haya, hatuta umiza vichwa kwa hoja za Maeda:
Uwiano na Usawa.
Lakini pia mimi niliposoma Somo la uchumi ktk hatua za awali,
Kuna maswali yalikosa majibu,nayo ni:
Kwanini watu wanaofanya kazi kubwa na ngumu inayotumia nguvu nyingi Hawalipwi vizuri mfano Wapasua kokoto n.k. lakini watu wanaofanya kazi ambazo hazihitaji nguvu kubwa wanalipwa vizuri, mfano TRA.
Ndivyo ilivyo.
 
Mkuu tuko nimekupata,
Umenipa changamoto nzuri sana.Hoja yangu ni kwamba kutokana na unyeti wa sekta hii ya habari ingekuwa vizuri tukaipa uzito fulani. Kwa namna gani sote tuumize vichwa vyetu. Kuna walimu walioajiriwa kila kona, na kuna wanasheria kila wilaya. Nadhani tungekuwa na wanahabari pia kila wilaya in the long run.

Sawa bw Aweda...
Wasiwasi wangu ni kwamba, hao waandishi wakiajiriwa na serikali, probably wataandikia vyombo vya habari vya serikali. Kwa hiyo wataandikia Habari Leo, Daily News, TBC, nk. Ni kwa kiasi gani hawa wachache waliopo leo kwenye hivi vyombo vya habari kwa sasa 'wananawasaidia wananchi'?. Kama ilivyo kwa tasnia nyingine, ushahidi unaonyesha waandishi wa habari pia ni watu wa HOVYO tu hapa Tanzania... Utamtofautishaje mwandishi wa Habari Leo na OCD Mwombeji? Wanachakuchua habari kama baadhi ya mahakimu na majaji wanavyochakachua kuibeba serikali... Wanachakachua habari kama polisi wanavyochakachua ulinzi na haki za raia kuibeba serikali.
Mwanakijiji leo tunamuona alivyo 'mzalendo', lakini huwezi kumtabiria atakuwaje siku akiwa mkurugenzi wa TBC...

Hata hivyo simaanishi kuwa waandishi hawana mchango, wana mchango mkubwa sana, lakini tungeanalyse positive results za uandishi wa habari Tanzania leo, I am sure 98% or more itakuwa imetokana na vyombo vya habari binafsi (sio binafsi vyote viko huru). Kama kuna namna tunaweza kuwasaidia wanahabari, na kusaidia kazi zao, sio kwa kuwalipa fedha kutoka serikalini. Nadhani ipo namna nyingine, waandishi wenyewe mtakuwa mnaifahamu bw Mikael P Aweda
 
Aweda,

Huwezi fananisha nanasi na ndizi.

Mwanakijiji kumfananisha na Abdallah Kigoda ni kama kufananisha Mbingu na Ardhi.

Nini cha maana na cha akili alichofanya Mwanakijiji zaidi ya majungu na fitna za mitandaoni?

Abdallah Kigoda on the other hand, ni mmoja katika watu mahiri sana na "he is a born leader".

Mkuu Nanasi na ndizi vinafananishika kwani yote matunda. Tofauti tu ya Kigoda na M.M ni FURSA na si jambo la kimiujiza sana. Kigoda alipata fursa ya kupeana huko CCM na akawa Waziri na kuonyesha kipaji chake ambacho actually ni cha kawaida kabisa ila MM hakufanikiwa kupata upendeleo wowote ndo maana hadi leo ni mpiganaji asiyetaka kuvutwa shati ili kufika anapotaka kufika. Ninaamini kwamba fighter wengi kama MM ni watu makini na wenye uwezo wa kuona mbali na kutenda tofauti na wanaokaa kusubiri huruma za kugawiwa vyeo.
 
Kama issue ni kuwatetea wanahabari embu tuanze na mtiririko wa background ya huyo mwanahabari. Alipomaliza form 4 akaenda wapi au kipi kilifuata maana kuna house made aliona wife wa bosi wake kanunuliwa nguo nzuri na yeye akaletewa ya kawaida akaanza kunong'ona eti mimi naamka saa kumi nafanya kazi zote yeye anaamka saa tatu hana analolifanya ndo anapata kizuri. Jamani unapokuwa ngazi ya juu wewe ni decision maker, siye wachini tutatumika mpaka position ndio itakayokuokoa. Naomba tufunge mjadala maana tutachukiana bure ingawa ndo ukweli wenyewe

Mkuu, post yake haiko wazi kama unavyoichukulia! Kuna mtu hapo juu amesema and I quote"too pholosophical" Sasa kama hujaelewa Takeshi time to your self and read between the lines.

Mimi sikulaumu Ika ukweli ni Kuwait hujaelewa hii post mazima!
 
Aweda,

Nimekupata mkuu, natumaini unamaanisha katiba mpya iwe na muundo utakaoheshimu kazi ya wanahabari. Natumaini humaanishi waandishi kuajiriwa wooote na serikali, but rather katiba itabumbue kuruhusu uwazi wa habari kufikia umma wa wa Tanzania. Yaani uhuru kwa vyombo vya habari ufikie kiwango cha Kuwa na nguvu ya muhimili wa dola. Ifikie wanahabari wawe watch dogs kwa serikari, ili kuimarisha intergrity, tofauti na sasa, watawala tumeona imefikia hatua wanatumiwa na vigogo kama condom!

Naunga mkono hoja na nawasilisha kama mchango wangu.
 
Jibu la swali hili naweza sema kwamba wapo watu walioajiriwa na wale ambao hawakuajiriwa wakifanya kazi ya kanisa. Mwanakijiji yawezekana yupo ktk kundi la wafanya kazi ya kanisa na wakisubiri malipo yao sii kwa fedha bali pale wewe unapoitambua kazi yake na kuithamini hivyo kumpa heshima, umaarufu na upendo. Pengine kazi ya Mwanakijiji wapo wadanganyika kibao wanaiweza hivyo haiwezi kuthaminika kutokana na kwamba kila mtu analiweza vuvuzela na kupiga tararira...Maana wabongo kwa kuchonga hatujambo, ukitangaza ajira kwa kazi hiyo utawapa millioni wamejichimbia vijiweni tu.

Na lazima tukubali ya kwamba sasa hivi tupo ktk dunia ya kibepari ambayo inaendeshwa na soko la mahitaji (demand) ili kuthaminisha kitu au kazi ya mtu. Leo hii Facebook tovuti la kuuza sura ina thamani kuliko banki ya NMB kwenye fedha kwenyewe hivyo ni muhimu kutambua kwamba ni kiasi gani kitu au mtu huyo anahitajika ndivyo atakavyo thaminika.

Mpasua mawe ya kokoto analipwa fedha kidogo kwa sababu wapo watu wengi wanaiweza kazi hiyo kuliko nafasi za kazi zilizopo. Sawa na wapiga debe, wajakazi, walinzi, utingo, wakulima, machinga, Madalali ndiko wananchi kibao wanazo sifa na uwezo wa kazi wakati nafasi za ajira ni chache ukilinganisha. Labda kinachoshangaza ni malipo ya Walimu na Madaktari lakini pia maadam MaSheikh/Mapadre na Waganga wa kienyeji wanalipwa zaidi hii inaonyesha wazi kwamba kuna soko kubwa la elimu ya dini kuliko elimu dunia pia madawa ya kienyeji yana soko kubwa kuliko madawa ya Hospital - NDIVYO TULIVYO!
 
Aweda,

Huwezi fananisha nanasi na ndizi.

Mwanakijiji kumfananisha na Abdallah Kigoda ni kama kufananisha Mbingu na Ardhi.

Nini cha maana na cha akili alichofanya Mwanakijiji zaidi ya majungu na fitna za mitandaoni?

Abdallah Kigoda on the other hand, ni mmoja katika watu mahiri sana na "he is a born leader".

Muulize Kigoda aliiuaje General Tyre na sasa anataka kuifufua? Kweli nyani haoni kundule hasa wewe
 
Mkuu Nanasi na ndizi vinafananishika kwani yote matunda. Tofauti tu ya Kigoda na M.M ni FURSA na si jambo la kimiujiza sana. Kigoda alipata fursa ya kupeana huko CCM na akawa Waziri na kuonyesha kipaji chake ambacho actually ni cha kawaida kabisa ila MM hakufanikiwa kupata upendeleo wowote ndo maana hadi leo ni mpiganaji asiyetaka kuvutwa shati ili kufika anapotaka kufika. Ninaamini kwamba fighter wengi kama MM ni watu makini na wenye uwezo wa kuona mbali na kutenda tofauti na wanaokaa kusubiri huruma za kugawiwa vyeo.

Hapana unakosea, ungefananisha ndizi mzuzu na ndizi kisukari au bukoba ningekuelewa.

Kigoda hajapewa, kagombania Ubunge na kashinda kwa uwezo alikuwa nao. Isitoshe Kigoda ana kisomo kuliko Mwanakijiji, kama hujuwi yule ni Dokta Abdallah Kigoda. Mwanakijiji hata shahada ya pili sijui kama anayo wacha udokta, hiyo ya kwanza yenyewe nnashaka hana.

Sasa wewe unataka wawe na fursa sawa katika kuajiriwa?

Kama alivyosema Mkandara, wapiga porojo ni wengi sana, wasomi wa haja kama Kigoda ni wachache sana Tanzania.

Unafananisha Mpopoo na Mpapai?

Mgomba hata nyuma ya choo unaota, nenda kapande mnanasi nyuma ya choo uone kama utaota. Ushaukuta mnanasi nyuma ya choo? ingawa yote ni matunda!
 
Hapo nilipokuwekea nyekundu badilisha, inaonesha kuwa Kiswahili chako ni cha manati.

Nashkuru Mungu kukufahamisha kuwa sijawahi kuwa mlala hoi wala mlala hai nimezaliwa nikiwa mlala heri na mpaka leo ni mlala heri. Naajiri toka nimezaliwa AlhamduliLllah.

kumbe tunaongea na mafyatu,unajisifia et?....mlala heri!...una nin?....sikusikii vizuri hvyo vyeti vyako vichafu vya kununu vya IT ndio unajiona maisha umeyamaliza!we dogo jiangalie sana wewe,huwa na kutahadhalisha sana,jiangalie we dogo.....ohooo!!
 
Shida iko wapi, muingizeni kwenye payroll ya cdm si mnapata ruzuku? mchango wa mwanakijiji zaidi ya kwenye cdm kwa wananchi wa kawaida haujulikana na haujaonekana bado

Weka pembeni issue ya CDM hapa, wewe yaelekea kila ukisaini JF unawaza kugombana kivyama tu. Kwa dizaini hii hatutasolve mambo ya maana kwaajili ya haya makundi makundi yenu mnayoya extend kuanzia kwenye ubongo mpaka kisiginoni
 
Aweda,

Huwezi fananisha nanasi na ndizi.

Mwanakijiji kumfananisha na Abdallah Kigoda ni kama kufananisha Mbingu na Ardhi.

Nini cha maana na cha akili alichofanya Mwanakijiji zaidi ya majungu na fitna za mitandaoni?

Abdallah Kigoda on the other hand, ni mmoja katika watu mahiri sana na "he is a born leader".

Plus ni president material
 
Mkuu, post yake haiko wazi kama unavyoichukulia! Kuna mtu hapo juu amesema and I quote"too pholosophical" Sasa kama hujaelewa Takeshi time to your self and read between the lines.

Mimi sikulaumu Ika ukweli ni Kuwait hujaelewa hii post mazima!

Mbona hakuna philosophy iliyotumika hapo zaidi ya elimu ndogo ya kuelewa tu. Na hapa hatutakubaliana sababu anayetaka atetewe amesahau kama kuna vitengo vingi vilivyo na umuhimu zaidi ya uandishi, akumbuke bila mwalimu asingetaipu sasa hivi kutetea haki yake, bila manesi na madaktari sijui ataishi vipi na wengine wengi. Ndo maana nimesema akajipange aje upya
 
Gadizooooo!!! sijui hisia zangu zikoje kuweza kutajwa kwenye mstari mmoja na mtu ambaye amehusika sana ubinafsishaji wa raslimali zetu na ambaye amerudishwa tena kusimamia sekta hiyo hiyo - watu wakiamini kuwa anaweza kubadili msimamo wake. Upande mwingine mimi na Kigoda tumejenga urafiki mkubwa sana ambao wengi hawaujui na kwa wanaokumbuka tulishirikiana kufanikisha jambo moja la kifamilia kule Handeni - bila msaada wa Kigoda nisingeweza kufanikiwa kabisa kuunganisha ile familia.

Lakini, ni ulinganisho wa pande mbili - mimi kwama mtu wa kawaida, mwenye kudhauralika, na ambaye jamii inaniona mshamba - hence 'mwanakijiji' na wale ambao jamii inawaona ndio wenye nchi na wenye kustahili zaidi. Japo wengine wameona ni ulinganisha wa kazi ya mwandishi binafsi naona ni ulinganisho wa mchango wa kila mmoja wetu. Mada nzima ninavyoiona mimi ni kuwa wapo watu wengi wanaotoa mchango katika jamii yetu kwa nafasi walizonao na labda wakati mwingine wanaonekana kujitolea zaidi kufanya mambo hayo kuliko wale ambao waliomba kazi na kuajiriwa kulipwa mshahara kufanya kazi hizo!! this to me is the paradox. Iweje mtu aliyeomba kazi (akachaguliwa au kuteuliawa) anapewa posho, na mishahara minono aonekane anafanya madudu na mtu mwingine anayejitolea anaonekana ana uchungu zaidi na kazi hiyo?

Tumeona kina mama na vijana, wake kwa waume wakifanya mambo mbalimbali katika jamii zao na wengine wakiendeleza harakati za mabadiliko. Wapo ambao ni mashujaa wasiotajwa ambao huko maofisini wameona madudu na wakayaibua na sifa ikawaendea wana siasa wa kuchaguliwa. Jibu laweza pia kuwa rahisi - hawa wanaojitolea hawastahili kudai lolote (iwe fidia au tuzo) kwani wanafanya kutoka kwenye mioyo yao; bila kuombwa au kulazimishwa. Hili ndilo pia tishio kubwa dhidi yao - mtu ambaye anafanya kazi kwa kujitolea utamkataza vipi wakati hujamuajiri, humlipi na wala humgharimii kwa vyovyote? Well, mtu huyo ANAKUWA NA NGUVU kuliko wale wanaolipwa na kuajiriwa kufanya mambo kwani hawa wanafanya mambo wakifikiria matokeo yake. Siyo kwamba hawawezi kufanya wanayofanya "kina mwanakijiji" bali wanafikiria wakifanya zaidi wataitwa na kukaripiwa, watatishiwa ajira zao na labda watanyanyaswa kwa namna moja au nyingine...

Inafikirisha sana....
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom