Mzee Mwanakijiji vs Waziri Abadallah Kigoda.

Mzee Mwanakijiji vs Waziri Abadallah Kigoda.

Ng'wanakidiku hapa umeongeza maneno na kubadilisha maana nzima ya uchangiaji. Kwa msaada zaidi, Marekani na kwingineko kwenye demokrasia iliyopevuka mihimili mikuu ya nchi (serikali, bunge, mahakama) utendaji wake hauingiliwi katika maamuzi yake kisheria. Vyombo vya habari haviko juu ya rais, bali uhamasisho(influence) wake kwa jamii ni mkubwa ambapo Raisi inabidi avitegemee sana katika utendaji wake ili ujumbe wake uiwifikie jamii katika hali chanya.
Tena waandishi wa rais wa US wanatengewa nafasi zao mahsus kwenye Air Force One!.
 
Idawa ni kweli kwa asilimia 100% mimi Pasco wa jf kwa bahasha stahiki, hunitoi!. Nimeshazivuta sana nilipokuwa reporter na sasa mimi ndio msambazaji wa bahasha hizo kama mwezeshaji!.

mkuu pasco hivi bahasha mnzopewa au unazosambaza zipo kisheria au takrima.?
 
Kamanitakuwa nimeelewa nadharia ya Aweda, anachosema ni kuwa hao akina mwanakijijiwa maeneo tofauti wanajenga nyumba ile ile anayojenga Kagoda.

Kagoda akiangukiwa na fito wakati wa kujenga nyumba anakimbizwa Appollo india kwafedha kutoka katika kikapu kile kile wanachochangia na'' mwanakijiji''

Mwanakijij iakiangukiwa na fito anapelekwa kulala chini pale muhimbili akisubiri donda lioze ili mungu ampende Zaidi.

Kama wotewanajenga nyumba inayoitwa taifa, haya yanatokeaje?

Pili, kuhusuwaandishi kuwa mhimili wa nne, hilo kwa nchi za wenzetu ni haki.
Hapa kwetu nisingependa wapewe heshima hiyo.

Hawana heshima wala sifa ya kuwa mhimili wanne.
Siwakashifu naeleza ukweli, na hapa Namwita Salva Rweyemam anitetee.

Slava ni mwandishi wa habari, wiki mbili zilizopoita alisimama katika kipaza sauti nakutetea rushwa aliyoiandaa kwa waandishi. Salva kawataja kwa majina,ikimaanisha wanafanya kazi hiyo siku nyingi tu.

Taarifa zaEscrow zinaonyesha waandishi walipewa mgao wa Ruge ili watuhakikishie kuwa hakuna pesa za umma. Walifanya kazi hiyo.

Huku kwenyesocial media ndiko usiseme, kazi yao si kuisaidia jamii, ni kutimiza matakwa yawazee wanaowatuma.

Hadi hapo waandishi watakaporudisha thamani ya taaluma yao nchini, nabaki kusema nimhimili wakwingine, Tanzania waandishini vijakazi.

Samahani,sijui kupindisha maneno ili kuburudisha watu!
 
Kagoda akiangukiwa na fito wakati wa kujenga nyumba anakimbizwa Appollo india kwafedha kutoka katika kikapu kile kile wanachochangia na'' mwanakijiji''

Mwanakijij iakiangukiwa na fito anapelekwa kulala chini pale muhimbili akisubiri donda lioze ili mungu ampende Zaidi.

Hapo ndio panapo taka mtu uwe makini na chances zako na kupima risk zako, vinginevyo ukijifanya mtundu wa kuparamia mabati yenye kutu wakati unajua insurance umeacha kukata na unajua hali ya muhimbili sasa yakikukuta shauri zako or when the call of help comes watu wanaweza sema ndivyo alivyo bila kujua bati safari hii limemkata vipi.
 
Sina uhakika umeelewa maana nzima ya kile nilichoongelea.
Ungechukuaimuda wa kusoma, kuelewa na kasha kujibu usingefika hapo.

Mkuu, nyumba inayojengwa ni Tanzania. Fito si lazima ziwe za miti, ni msemo tu.
Labda ningesema kwa lugha utakayoelewa kwa urahisi.

Kama wotewanajenga taifa, na wana kikapu cha pamoja, mmoja ana uwezo wa kuchota kwendaIndia, mwingine hawezi kupata asprin kwasababu kikapu hakina pesa kwake, lakinikwa Kagoda kina pesa, wapi kuna ujenzi wa pamoja.

Ukizumgumzia insurance, sasa kama ni hivyo huyo Kagoda kwanini asiwe na yake ili mwanakijiji awe na yake, tukiache kikapu kama kilivyo?

Cc Mkandara
 
Ooops lost in translation my bad.

By the way kule kwenu kwengine kwa GT ukitualika ukiona kimya ni kwa sababu hatuna access nako.
 
Mchukulie mzee mwanakijiji kama mwandishi makini na msomi anayetumia akili yake aliyojaliwa na mwenyenzi Mungu kufikiri juu ya nchi yake na kuziandika fikra hizo ktk mitandao ya kijamii na magazetini. Mwanakijiji ni mwakilishi wa waandishi wote wazuri wa habari akiwepo wewe wa JF. Mchukulie waziri Abdallah Kigoda, waziri wa viwanda na biashara kama mwakilshi wa mawaziri na watumishi wote wa Serikali.

Wote hawa ( Mwanakijiji na Kigoda) ni watanzania na wana haki sawa, wote wanawatumikia watanzania kwa nia njema ya kusukuma guruduma la maendeleo mbele. Mmoja analipwa mshahara, posho, gari, mkopo wa mil 90 ( kama mbunge nk ) mwingine (mwanakijiji) hana vyote hivyo. Kwanini? jibu, ndivyo ilivyo.

Wote wawili wanatumia akili, wote wawili wanawatumikia watz, wote wanatumia muda wao kufanya kazi moja ya kujenga nyumba moja TZ, Wote wamesomeshwa na kodi zetu na wote ni watanzania. Tafauti za nini kati yao? Jibu ndivyo ilivyo.

Kati yao hakuna mwenye haki ya uraia zaidi ya mwingine na kazi zao zina tija sawa. Pengine mwanakijiji anaweza kuwa bora kuliko baadhi ya mawaziri ambao hata watz waliowengi hawawajui hata kwa majina. Kwa nini tofauti kwenye masilahi baina yao? Jibu, ndivyo ilivyo.

Kwanini inapofika kwenye maslahi (Mishahara, posho, mikopo na magari) tunabaguana? Je, kwa nini michango ya hawa watz wawili inaheshima tofauti sana mbele ya Serikali? ndivyo ilivyo.

Au Je, kwa kuwa mmoja cheo chake kinatangazwa redioni na kwenye vyombo vya habari na Rais ndio sababu ya kuwa na maslahi zaidi? Je, waziri wa habari naye angepewa Jukumu la kutangaza waandishi wa habari wenye vigezo fulani elimu nk, wangeweza kuwa na sifa ya kupata hayo maslahi ya watumishi wengine? Au je, tija ya waandishi ni ndogo sana kuliko hawa mawaziri wanaopata maslahi? Je, ni watu wanagapi wanasoma makala za mwanakijiji na kufunguka? Kwa nini imekuwa hivi?

Kwenye nchi za wenzetu, vyombo vya habari inakaribia kuwa mhimili wa nne wa dola, kwetu sisi hata shukrani hamna. Kwanini? ndivyo ilivyo.

Je, hii ni sawa? Je, tunawezaje kuliweka jambo hili vizuri ktk katiba mpya? Hivi huyu mtanzania aliyetumia akili yake kuanzisha JF ambayo imekuwa msaada sana hakustahili maslahi hayo anayopata Abadallah Kigoda?

Jibu la wengi ni, hivyo ndivyo ilivyo. Kwa maoni yangu si kila jambo lilivyo, ndivyo inavyopaswa kuwa, mengine NDIVYO ILIVYO LAKINI SIVYO INAVYOTAKIWA KUWA. Inawezekana Kinyume chake pia ni nzuri zaidi.

Mfumo wetu wa maisha umefanya fani ya uandishi kukosa uzito stahiki, na pia waandishi wenyewe wamekua wakitumika kikanjanja kama polisi
 
Back
Top Bottom