Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mwanakijiji anaitaji pongezi .pöngezi zetu za kutoka moyoni ni fadhila tosha zaidi ya hongo wanayopewa mawaziri wetu.
Pole sana Comrade kumbe hata kwenye mwanga huu wa jua bado upo gizani kwa nini huiishi kuwatumikia watu badirika ndugu yangu utatumwa mpaka lini huuni ufahari wa wewe nawe kuwatuma watu:
Niko tayari
Suala la mfumo wa utawala hutegemea pai utamaduni wa wananchi juu ya kuihoji serikaliyao. Mfano USA vyombo vya habari vipo juu ya rais, na mahakama ipo juu ya rais. Nadhani kuna umuhimu wa kuliweka kwenye katiba
Mkuu we una wivu,majungu na unafiki.samahani lakini kwa maneno hayo.Hivi tangu lini watu wakafanana kimaisha au kipato?yaani umefananisha vitu viwili tofauti nafikiri hapo ungefananisha huyo Mzee Mwanakijiji na Mh.Mbowe na Dr.Slaa lakini ufananisho wako ni wa majungu na chuki binafsi.Nina hakika we una tofauti kubwa ya kipato,posho na mengineyo na katibu kata wako wa chama chako hilo hujaliona.Ni kweli Mzee mwanakijiji ana mchango mkubwa wa kimawazo ktk jamii tena inaonesha ni mahiri katika fani yake lakini ni wangapi wanamfahamu au kufaidika na mawazo yake ambayo mara nyingi yapo kwenye magazeti na mitandao? Mara nyingi makala zake zipo biased anapendelea sana CDM na ndiyo maana we umepata msukumo wa kumsifu hapa.Tafakari kwanza then utoe vitu vinavyofanana uzito.Hivyo ndivyo ilivyo mkuu.Mchukulie mzee mwanakijiji kama mwandishi makini na msomi anayetumia akili yake aliyojaliwa na mwenyenzi Mungu kufikiri juu ya nchi yake na kuziandika fikra hizo ktk mitandao ya kijamii na magazetini. Mwanakijiji ni mwakilishi wa waandishi wote wazuri wa habari akiwepo wewe wa JF. Mchukulie waziri Abdallah Kigoda, waziri wa viwanda na biashara kama mwakilshi wa mawaziri na watumishi wote wa Serikali.
Wote hawa ( Mwanakijiji na Kigoda) ni watanzania na wana haki sawa, wote wanawatumikia watanzania kwa nia njema ya kusukuma guruduma la maendeleo mbele. Mmoja analipwa mshahara, posho, gari, mkopo wa mil 90 ( kama mbunge nk ) mwingine (mwanakijiji) hana vyote hivyo. Kwanini? jibu, ndivyo ilivyo.
Wote wawili wanatumia akili, wote wawili wanawatumikia watz, wote wanatumia muda wao kufanya kazi moja ya kujenga nyumba moja TZ, Wote wamesomeshwa na kodi zetu na wote ni watanzania. Tafauti za nini kati yao? Jibu ndivyo ilivyo.
Kati yao hakuna mwenye haki ya uraia zaidi ya mwingine na kazi zao zina tija sawa. Pengine mwanakijiji anaweza kuwa bora kuliko baadhi ya mawaziri ambao hata watz waliowengi hawawajui hata kwa majina. Kwa nini tofauti kwenye masilahi baina yao? Jibu, ndivyo ilivyo.
Kwanini inapofika kwenye maslahi (Mishahara, posho, mikopo na magari) tunabaguana? Je, kwa nini michango ya hawa watz wawili inaheshima tofauti sana mbele ya Serikali? ndivyo ilivyo.
Au Je, kwa kuwa mmoja cheo chake kinatangazwa redioni na kwenye vyombo vya habari na Rais ndio sababu ya kuwa na maslahi zaidi? Je, waziri wa habari naye angepewa Jukumu la kutangaza waandishi wa habari wenye vigezo fulani elimu nk, wangeweza kuwa na sifa ya kupata hayo maslahi ya watumishi wengine? Au je, tija ya waandishi ni ndogo sana kuliko hawa mawaziri wanaopata maslahi? Je, ni watu wanagapi wanasoma makala za mwanakijiji na kufunguka? Kwa nini imekuwa hivi?
Kwenye nchi za wenzetu, vyombo vya habari inakaribia kuwa mhimili wa nne wa dola, kwetu sisi hata shukrani hamna. Kwanini? ndivyo ilivyo.
Je, hii ni sawa? Je, tunawezaje kuliweka jambo hili vizuri ktk katiba mpya? Hivi huyu mtanzania aliyetumia akili yake kuanzisha JF ambayo imekuwa msaada sana hakustahili maslahi hayo anayopata Abadallah Kigoda?
Jibu la wengi ni, hivyo ndivyo ilivyo. Kwa maoni yangu si kila jambo lilivyo, ndivyo inavyopaswa kuwa, mengine NDIVYO ILIVYO LAKINI SIVYO INAVYOTAKIWA KUWA. Inawezekana Kinyume chake pia ni nzuri zaidi.
Mkuu we una wivu,majungu na unafiki.samahani lakini kwa maneno hayo.Hivi tangu lini watu wakafanana kimaisha au kipato?yaani umefananisha vitu viwili tofauti nafikiri hapo ungefananisha huyo Mzee Mwanakijiji na Mh.Mbowe na Dr.Slaa lakini ufananisho wako ni wa majungu na chuki binafsi.Nina hakika we una tofauti kubwa ya kipato,posho na mengineyo na katibu kata wako wa chama chako hilo hujaliona.Ni kweli Mzee mwanakijiji ana mchango mkubwa wa kimawazo ktk jamii tena inaonesha ni mahiri katika fani yake lakini ni wangapi wanamfahamu au kufaidika na mawazo yake ambayo mara nyingi yapo kwenye magazeti na mitandao? Mara nyingi makala zake zipo biased anapendelea sana CDM na ndiyo maana we umepata msukumo wa kumsifu hapa.Tafakari kwanza then utoe vitu vinavyofanana uzito.Hivyo ndivyo ilivyo mkuu.
Jamani hapa tusikae kishabiki bila mantiki, wekeni CV ya mwanakijiji na ya Kigoda ndo tujadili. Alafu huyu mwanakijiji ninani hasa na je anajulikana na wangapi? Embu tujadili kiakili tutoe itikadi zetu, maana nyie mnaomtetea inawezekana mnamjua tangia zamani lakini sisi wengine tumemuonea JF. Na angekuwa anajitambua na kujiheshimu angeachana na nickname akaweka jina kamili. Kwakweli hapa namfananisha na msanii maana ili atoke kwakutojiamini anatumia jina lenye swaga kibao.
Aweda,
Huwezi fananisha nanasi na ndizi.
Mwanakijiji kumfananisha na Abdallah Kigoda ni kama kufananisha Mbingu na Ardhi.
Nini cha maana na cha akili alichofanya Mwanakijiji zaidi ya majungu na fitna za mitandaoni?
Abdallah Kigoda on the other hand, ni mmoja katika watu mahiri sana na "he is a born leader".
Mkuu wewe unaitwa nani? pwito? Mbona hujaweka majina yako yote matatu kikamilifu?
Kama wewe unataka tujadili maoni yako wakati hutumii majina yako halisi kwa nini unataka tusiheshimu maoni ya huyu mpambanaji mwakijiji? Hoja ni hoja aliyotoa wala siyo sura yake AU kimo chake.
Kama issue ni kuwatetea wanahabari embu tuanze na mtiririko wa background ya huyo mwanahabari. Alipomaliza form 4 akaenda wapi au kipi kilifuata maana kuna house made aliona wife wa bosi wake kanunuliwa nguo nzuri na yeye akaletewa ya kawaida akaanza kunong'ona eti mimi naamka saa kumi nafanya kazi zote yeye anaamka saa tatu hana analolifanya ndo anapata kizuri. Jamani unapokuwa ngazi ya juu wewe ni decision maker, siye wachini tutatumika mpaka position ndio itakayokuokoa. Naomba tufunge mjadala maana tutachukiana bure ingawa ndo ukweli wenyewe
Mwanakijiji (na wengineo) avute subira kidogo. anaweza kuwa karibu kidogo na Kigoda kimaslahi na mambo mengine. wameanza kutoa ma DC kutoka miongoni mwao (wana habari).
ila wasi wasi wangu ni kuwa M.M. anasema ukweli mno na kuonekana mpinzani, cjui kama atapewa u DC.
NDIVYO ILIVYO!
Kama inawezekana na kama tunakubaliana kuwa Kigoda na mwanakijiji wanatoa mchango kwa wananchi basi walipwe wote. Kama haiwezekani kuwalipa wote basi hata kutambua mchango wa huyo ambaye tumeshindwa kumlipa ni muhimu. Tatizo ni kwamba waandishi hawalipwi na hawaheshimiki wakati ni fani muhimu sana. Ikumbukwe hapa tunajadili zaidi ya mwanakjijij na Kigoda.
Na swali la pili ni je, kwa kuwa tunaandika katiba mpya, je kuna haja ya kutambua mchango wa hao waandishi wa habari? Je, kama taifa hatuwezi?
Aweda,
Huwezi fananisha nanasi na ndizi.
Mwanakijiji kumfananisha na Abdallah Kigoda ni kama kufananisha Mbingu na Ardhi.
Nini cha maana na cha akili alichofanya Mwanakijiji zaidi ya majungu na fitna za mitandaoni?
Abdallah Kigoda on the other hand, ni mmoja katika watu mahiri sana na "he is a born leader".
Thx, fursa ya katiba mpya ni lazima tuitumie vizuri. Turekebishe kila tatizo.
Wewe ndugu yangu humfahamu Mzee mwanakijiji, ila ipo siku utamfahamu! hata mimi wakati flani nilikuwa kama wewe lakini leo nimefunguka kifikra!hope wengi wamefunguka pia