Mzee Mwanakijiji vs Waziri Abadallah Kigoda. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Mwanakijiji vs Waziri Abadallah Kigoda.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, May 25, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mchukulie mzee mwanakijiji kama mwandishi makini na msomi anayetumia akili yake aliyojaliwa na mwenyenzi Mungu kufikiri juu ya nchi yake na kuziandika fikra hizo ktk mitandao ya kijamii na magazetini. Mwanakijiji ni mwakilishi wa waandishi wote wazuri wa habari akiwepo wewe wa JF. Mchukulie waziri Abdallah Kigoda, waziri wa viwanda na biashara kama mwakilshi wa mawaziri na watumishi wote wa Serikali.

  Wote hawa ( Mwanakijiji na Kigoda) ni watanzania na wana haki sawa, wote wanawatumikia watanzania kwa nia njema ya kusukuma guruduma la maendeleo mbele. Mmoja analipwa mshahara, posho, gari, mkopo wa mil 90 ( kama mbunge nk ) mwingine (mwanakijiji) hana vyote hivyo. Kwanini? jibu, ndivyo ilivyo.

  Wote wawili wanatumia akili, wote wawili wanawatumikia watz, wote wanatumia muda wao kufanya kazi moja ya kujenga nyumba moja TZ, Wote wamesomeshwa na kodi zetu na wote ni watanzania. Tafauti za nini kati yao? Jibu ndivyo ilivyo.

  Kati yao hakuna mwenye haki ya uraia zaidi ya mwingine na kazi zao zina tija sawa. Pengine mwanakijiji anaweza kuwa bora kuliko baadhi ya mawaziri ambao hata watz waliowengi hawawajui hata kwa majina. Kwa nini tofauti kwenye masilahi baina yao? Jibu, ndivyo ilivyo.

  Kwanini inapofika kwenye maslahi (Mishahara, posho, mikopo na magari) tunabaguana? Je, kwa nini michango ya hawa watz wawili inaheshima tofauti sana mbele ya Serikali? ndivyo ilivyo.

  Au Je, kwa kuwa mmoja cheo chake kinatangazwa redioni na kwenye vyombo vya habari na Rais ndio sababu ya kuwa na maslahi zaidi? Je, waziri wa habari naye angepewa Jukumu la kutangaza waandishi wa habari wenye vigezo fulani elimu nk, wangeweza kuwa na sifa ya kupata hayo maslahi ya watumishi wengine? Au je, tija ya waandishi ni ndogo sana kuliko hawa mawaziri wanaopata maslahi? Je, ni watu wanagapi wanasoma makala za mwanakijiji na kufunguka? Kwa nini imekuwa hivi?

  Kwenye nchi za wenzetu, vyombo vya habari inakaribia kuwa mhimili wa nne wa dola, kwetu sisi hata shukrani hamna. Kwanini? ndivyo ilivyo.

  Je, hii ni sawa? Je, tunawezaje kuliweka jambo hili vizuri ktk katiba mpya? Hivi huyu mtanzania aliyetumia akili yake kuanzisha JF ambayo imekuwa msaada sana hakustahili maslahi hayo anayopata Abadallah Kigoda?

  Jibu la wengi ni, hivyo ndivyo ilivyo. Kwa maoni yangu si kila jambo lilivyo, ndivyo inavyopaswa kuwa, mengine NDIVYO ILIVYO LAKINI SIVYO INAVYOTAKIWA KUWA. Inawezekana Kinyume chake pia ni nzuri zaidi.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Very Philosophical, inafikirisha na kutafakarisha mkuu. Big up!!!
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Fikra pevi zaidi
   
 4. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Thx, fursa ya katiba mpya ni lazima tuitumie vizuri. Turekebishe kila tatizo.
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji yupo juu zaidi
   
 6. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Very said M/Kiti wangu. Kuna ubaguzi ktk kugawana keki ya Taifa, kamwe tusikubali kuandikiwa katiba mpya na CC Kuu ya CCM.

  Katibu wa Tawi Pugu Bombani Chadema.
   
 7. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mwanakijiji (na wengineo) avute subira kidogo. anaweza kuwa karibu kidogo na Kigoda kimaslahi na mambo mengine. wameanza kutoa ma DC kutoka miongoni mwao (wana habari).

  ila wasi wasi wangu ni kuwa M.M. anasema ukweli mno na kuonekana mpinzani, cjui kama atapewa u DC.
  NDIVYO ILIVYO!
   
 8. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Suala la mfumo wa utawala hutegemea pai utamaduni wa wananchi juu ya kuihoji serikaliyao. Mfano USA vyombo vya habari vipo juu ya rais, na mahakama ipo juu ya rais. Nadhani kuna umuhimu wa kuliweka kwenye katiba
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Aweda,

  Huwezi fananisha nanasi na ndizi.

  Mwanakijiji kumfananisha na Abdallah Kigoda ni kama kufananisha Mbingu na Ardhi.

  Nini cha maana na cha akili alichofanya Mwanakijiji zaidi ya majungu na fitna za mitandaoni?

  Abdallah Kigoda on the other hand, ni mmoja katika watu mahiri sana na "he is a born leader".
   
 10. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160

  Nilidhani sote tunaishi duniani kumbe sivyo.
   
 11. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #11
  May 25, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Sasa La-Aweda, mimi hapa nashindwa kukuelewa... Unamaanisha kila anayetoa mchango kwa wananchi alipwe. au unamaanisha hata wanaotoa mchango kupitia serikali, sio lazima walipwe kiasi hicho kwa sababu kuna wengine wasiokuwepo serikalini nao wanatoa michango na hawalipwi?

  Au unamaanisha waandishi wa habari na wanaharakati walipwe na serikali?!!!

  Kama unamfuatilia Mzee Prof Shivji kwenye mihadhara yake ya katiba, ile siku ya kwanza alisema kuwa Katiba ni mfumo ulioanzishwa ili kuwalinda na kutetea maslahi ya watawala dhidi ya watawaliwa... Hayo maneno yanaweza kuonekana kama ya kipuuzi, but ukiyawaza sana utaona yana point kubwa sana. Usitegemee, wala usitarajia kuwa itaandikwa katiba itakayotoa usawa kati ya watawala na watawaliwa, never...
   
 12. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2012
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Haa!! Mkuu Ribosome, mbona unatembea kichwa chini miguu juu?!!!!!
   
 13. alberaps

  alberaps JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,450
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280
  Hii ni Kweli


  Hii Pia bado Ni kweli


  Hii ni GUBU na Wivu Mkali.

  ==>Tuambie alichofanikisha Kigoda Kwenye Nchi hii cha mfano ambacho nchi kama Kenya {Nimechagua Nchi ya jirani kabisa na sisi} wanaweza kuiga kwetu.

  ==>Tuambie na hizo fitna unazozisema za Mwanakijiji Tafadhali


  Mahiri Katika Nini labda unaweza kutuelezea labda? Ni kipi alichofanya beyond Expectation?
   
 14. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Kwani kuna mtu ambaye hajabeborn as a leader? mbona hata Mzazi wangu alizaliwa akiwa kiongozi na ndiyo maana kaiongoza vyema familia yake.:violin:
   
 15. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Maoni yana tija kwa taifa,kweli tutoe mapendekezo kwa tume ya warioba,katiba mpya iwe na nafasi kwa vyombo vya habari na waandishi kwa ujumla
   
 16. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aweda huwa tunakuonaga sana kwenye vipindi vya ITV tena sana sana kipima joto au sema usikike.

  swali, wewe ni mwanaharakati au mtanganyika tu wakawaida??
   
 17. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Pole sana Comrade kumbe hata kwenye mwanga huu wa jua bado upo gizani kwa nini huiishi kuwatumikia watu badirika ndugu yangu utatumwa mpaka lini huuni ufahari wa wewe nawe kuwatuma watu:
  Niko tayari
   
 18. J

  JTHANY Member

  #18
  May 25, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mtazamo wangu mim wote wanfanya kazi ya kijamii ila Mwanakijiji anafanya kazi kwenye mazingira magumu zaidi yanayomuhitaji awe involved direct compare to Waziri ambaye anasupaviz utendaji, hivyo wote wana haki za msingi kama posho n.k base on kazi wanazofanya na risk iliyopo.
   
 19. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #19
  May 25, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kama inawezekana na kama tunakubaliana kuwa Kigoda na mwanakijiji wanatoa mchango kwa wananchi basi walipwe wote. Kama haiwezekani kuwalipa wote basi hata kutambua mchango wa huyo ambaye tumeshindwa kumlipa ni muhimu. Tatizo ni kwamba waandishi hawalipwi na hawaheshimiki wakati ni fani muhimu sana. Ikumbukwe hapa tunajadili zaidi ya mwanakjijij na Kigoda.
  Na swali la pili ni je, kwa kuwa tunaandika katiba mpya, je kuna haja ya kutambua mchango wa hao waandishi wa habari? Je, kama taifa hatuwezi?
   
 20. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mwanakijiji anaitaji pongezi .pöngezi zetu za kutoka moyoni ni fadhila tosha zaidi ya hongo wanayopewa mawaziri wetu.
   
Loading...