Gadizooooo!!! sijui hisia zangu zikoje kuweza kutajwa kwenye mstari mmoja na mtu ambaye amehusika sana ubinafsishaji wa raslimali zetu na ambaye amerudishwa tena kusimamia sekta hiyo hiyo - watu wakiamini kuwa anaweza kubadili msimamo wake. Upande mwingine mimi na Kigoda tumejenga urafiki mkubwa sana ambao wengi hawaujui na kwa wanaokumbuka tulishirikiana kufanikisha jambo moja la kifamilia kule Handeni - bila msaada wa Kigoda nisingeweza kufanikiwa kabisa kuunganisha ile familia.
Lakini, ni ulinganisho wa pande mbili - mimi kwama mtu wa kawaida, mwenye kudhauralika, na ambaye jamii inaniona mshamba - hence 'mwanakijiji' na wale ambao jamii inawaona ndio wenye nchi na wenye kustahili zaidi. Japo wengine wameona ni ulinganisha wa kazi ya mwandishi binafsi naona ni ulinganisho wa mchango wa kila mmoja wetu. Mada nzima ninavyoiona mimi ni kuwa wapo watu wengi wanaotoa mchango katika jamii yetu kwa nafasi walizonao na labda wakati mwingine wanaonekana kujitolea zaidi kufanya mambo hayo kuliko wale ambao waliomba kazi na kuajiriwa kulipwa mshahara kufanya kazi hizo!! this to me is the paradox. Iweje mtu aliyeomba kazi (akachaguliwa au kuteuliawa) anapewa posho, na mishahara minono aonekane anafanya madudu na mtu mwingine anayejitolea anaonekana ana uchungu zaidi na kazi hiyo?
Tumeona kina mama na vijana, wake kwa waume wakifanya mambo mbalimbali katika jamii zao na wengine wakiendeleza harakati za mabadiliko. Wapo ambao ni mashujaa wasiotajwa ambao huko maofisini wameona madudu na wakayaibua na sifa ikawaendea wana siasa wa kuchaguliwa. Jibu laweza pia kuwa rahisi - hawa wanaojitolea hawastahili kudai lolote (iwe fidia au tuzo) kwani wanafanya kutoka kwenye mioyo yao; bila kuombwa au kulazimishwa. Hili ndilo pia tishio kubwa dhidi yao - mtu ambaye anafanya kazi kwa kujitolea utamkataza vipi wakati hujamuajiri, humlipi na wala humgharimii kwa vyovyote? Well, mtu huyo ANAKUWA NA NGUVU kuliko wale wanaolipwa na kuajiriwa kufanya mambo kwani hawa wanafanya mambo wakifikiria matokeo yake. Siyo kwamba hawawezi kufanya wanayofanya "kina mwanakijiji" bali wanafikiria wakifanya zaidi wataitwa na kukaripiwa, watatishiwa ajira zao na labda watanyanyaswa kwa namna moja au nyingine...
Inafikirisha sana....
Mzee mwenzangu mwanakijiji naomba nikupe mfano huu, "mtoto analelewa na wazazi na walezi wengine lakini huyo mtoto akiharibu atanyooshewa kidole mzazi mara hili mara lile, vivyovivyo na akitenda baya, sababu mzazi ndio decision maker wake hata kama yule mzazi alikuwa anamuongoza vibaya na majirani wakamrekebisha mtoto akawa na tabia njema sifa itarudi kwa mzazi"
Narudi kwako Mzee mwenzangu ukitaka posho na heshima za kiuwaziri nenda jimboni kwako gombea wakuchague sisi tulio majimbo mengine tupambane na changamoto kwa pamoja ndio uiano huo utakuwepo.
Kumbuka ukiwa icon mabaya yako na mazuri yako yote yataonekana, tutakupima kwahilo zaidi ya hapo embu jifananishe na watumia kalamu wenzako muone kwanini Michuzi ni maarufu au anamarupurupu zaidi yako wakati yeye ni std7 with camera professional na leo yuko Ikulu. Heshima mkuu na jamani wale wenzangu karibuni kesho Jangwani