Mzee kipara afariki Dunia

somo kwa wasanii waliobakia: mzee kipara kwa namna moja au nyingine kifo chake kimechangiwa na uwezo duni wa kifedha aliokua nao ambao kwa namna moja ua nyingine ulimchelewesha kupata matibabu kwa wakati na kwa madaktari bingwa.

nyie mliobakia ambao kila kukicha mnaonekana kuendekeza starehe na kutoka kwenye magazeti na kashfa mbalimbali, msipokua makini mkajitambua ya kuwa kipaji mlichonacho ni cha mda kinapita basi mtakua kwenye wakati mgumu maradufu ya marehemu mzee wetu kipara, huyu mzee pamoja na kuheshimika na kuwa mfano kwa jamii bado hakupata ile misaada kwa wakati itakua nyinyi ambao kwanza hamjiheshimu pili kila siku mnajifanya wajuaji??? yani maadui wa wasaniii wasasa hvi ni mara mia ya wale wasanii wa zamani. anzeni kujipanga, ukweli unauma lakini ndio huleta mabadiliko. Mia
 
Pumzika kwa amani mzee kipara, dah timu ya kina mzee pwagu yote imeisha sasa. Eeh Mungu warehemu hawa waja wako. Ameen
 
Pumzika kwa amani mzee kipara, dah timu ya kina mzee pwagu yote imeisha sasa. Eeh Mungu warehemu hawa waja wako. Ameen

kama mtu akifa anapumzika,basi huyu mzee akapumzike,ameugua kwa muda mrefu sana,kwa x ya mwisho nilimwona kwenye show ya Take One last 3 wiksi
 
RIP mzee, ulionyesha uzalendo mkubwa kwenye fani atsnia ya filamu na kukuza vipaji vya wengi...lakini ni kama yale yalimpata Dk Remmy Ongala...umeugua muda mrefu lakini wasanii wengi/viongozi walikutupa mkono , hukuonja msaada wowote/mdogo toka kwao...tutakukumbuka sana hasa kwenye vipindi vya radioni(mchezo wa radio) Rest mkuu!!
 
Inna Lillah Waina Illahi Rajoon

"Ewe Mwenyezi Mungu msamehe Mzee Fundi Said na ipandishe daraja yake katika walioongoka, na weka badili yake kwa aliyowacha nyuma na utusamehe sisi na yeye ewe Mola wa viumbe vyote na umkunjulie yeye katika kaburi lake na umtilie mwangaza ndani yake"

"Sisi ni wa Allaah nasi Kwake tutarejea, Ee Allaah Walipe wafiwa kwa msiba huu na uwape badili yake bora kuliko huo"
 
Yes, nimeisikia Radio one habari hiyo. Mzee Kipara (Fundi Saidi) aliugua kisukari kwa muda mrefu sana
 
Inna Lillah Waina Illahi Rajoon

"Ewe Mwenyezi Mungu msamehe Mzee Fundi Said na ipandishe daraja yake katika walioongoka, na weka badili yake kwa aliyowacha nyuma na utusamehe sisi na yeye ewe Mola wa viumbe vyote na umkunjulie yeye katika kaburi lake na umtilie mwangaza ndani yake"

"Sisi ni wa Allaah nasi Kwake tutarejea, Ee Allaah Walipe wafiwa kwa msiba huu na uwape badili yake bora kuliko huo"

Aamin yarabi aamin.

Inna Lillahi wainna ilaihi rajihunna.

Pumzika kwa amani mzee Kipara, nilikusikia tangu enzi hizo radio tanzania kwenye michezo ya radio e.g mkataa pema pabaya panamwita n.k
 
Back
Top Bottom