Mzee kipara afariki Dunia

Alikuwa na sauti ya kiume hasa. Poleni wafiwa na tasnia yote ya sanaa nchini akina Swebe, Bi Hindu, Muhogo, Kanumba,...
 
ni somo kubwa ktk jamii,akiwa hai alishaomba msaada kwa mchango wake kwenye jamii alistahili kukimbiliwa.nikweli msibani watu watajitoa kweli lakini haitasaidia kama kujitoa alivyokuwa hai.mungu amlaze mahali pema peponi amen.
 
Mbona kuna thread nyingine ya huyu mzee?mods tunaomba muziunganishe iwe moja

Nimesearch kwanza nione kama kulikua na uzi lakin page zote mbili sikupata uzi huo ndo nikaanzisha kumbuka natumia cm na si computers za bure ofisini so kusearch kwa cm sio 100 sure
 
R.I.P Mzee kipara, ulifungua milango ya mafanikio kwa wasanii wengi wa filamu na maigizo mchango wako hautasaulika
 
huyu mzee nimemjua tangia enzi za film tanzania 1971 alipoact mchezo wa Simu ya kifo. Alijulikana kama mzee kikaango! Yaani tusingekuwa na azimio la kishetani la Arusha , huyu mzee angekuwa milionaire! Ame a perform michezo mingi sana Radion na katika magazeti lakini Ona alivyoishia kuwa masikini!!!!!!!!!!! Kama angekuwa Kenya au Nigeria, mzee kipara angeishia kuwa na magorofa saba!!!!!!! Usanii katika nchi za kenya na Ghana , Nigeria unalipa sana .

pamoja na sifa zote alizonazo mzee kipara kaishia kuishi nyumba ya babu yake pale living stosne karibu na kina mohamedi makanyaga na alikuwa mesenger au tarish pale railway station karibia maisha yake yote akivaa magwanda yaliyozeeka ya kaki ! Jina lake halisi ni saidi fundi na ana asili ya tabora! Mungu amlaze mahali pema mzee kipara!!

Ona azimio la la kishetani la arusha lilivyo watesa watu wenye vipaji vyao waliotikisa nchi kwa usanii mzuri na kuishia kuchangiwa uji msibani! Nyerere kweli anastahili kuwa mtakatifu jamani? kweli jambo hili lilimpendeza mungu ? baraza la maaskofu, tafadhalini, kuweni waungwana !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom