Kezilahabi, Mkerewe yuko Botswana sasa. Alipigwa ban na Kanisa Katolic kuhusu kitabu hicho cha Rosa Mistika. Nakumbuka sana kitabu chake cha 'Dunia uwanja wa fujo.
I believe Pili Pilipili was and to me is the best Play, yaani ukiisoma ile kitu huwezi weka chini hadi last page, tumepoteza shujaa wengi wa waliobakia ni wale wa kukopi na kupesti hadithi toka kwenye mtandao..... sorry kwa wanaomfahamu vizuri hivi ndie huy huyu alieandika na ile riwaya ya SIRI ya SIFURI???
Poleni wote jamani alini~Insipire saaaana jamani PUMZIKA KWA AMANI Faraj Katalambula...
Hivi Kezilahabi aliyetunga ROSA MISTIKA...yu wapi? Nakumbuka kipande cha Hadithi yake " Tulikuwa tukisikiliza NEGRO SUCESS NA MATONDO YA BEYA"
Hakika msiba wa Mzee Katalambula umefufua mengi! Nilikuwa natafuta jina la nani mtunzi wa Rosa Mistika maana nilisoma kitabu hicho katika umri wa barehe basi nilikuwa na fantasize vitu lukuki nikisoma kitabu hicho!
Kizazi kipya wanajua kunukuru (sina hakika na kiswahili changu kwenye neno fasaha) tungo za mapenzi na upuuzi mwingine na KUANDIKA RIWAYA ndio aibu tupu!
Sidhani hata kama wanajua (watunzi na waandishi wetu wa kizazi kipya) kuwa walikuwepo watunzi na waandishi ambao walivyotupatia kamwe havitotoka katika vichwa vyetu kwa ufasaha na umahiri walioutumia!
Sterling alikuwa ni Inspector Wingo.FAMBO wa riwaya ya SIMU YA KIFO! Ilikuwa ni kifupisho cha Francis Andrew Mbozia..
R.I.P. Mzee Katalambula
FARAJ KATALAMBULA KUZIKWA MKOANI TABORA
From: g sengo
Aliyekuwa mtunzi mahiri wa vitabu vya hadithi na riwaya nchini marehemu Faraj Katalambula (kulia) anatazamiwa kuzikwa kesho Isevya mkoani Tabora majira ya saa kumi jioni.
Faraj Katalambula alifariki juzi saa kumi na mbili jioni katika hospitali ya rufaa Muhimbili. Faraj Katalambula ambaye ni mmoja wa watunzi wa vitabu mahiri kupata kutokea atakumbukwa zaidi kwa utunzi wake wa kitabu kilichosomwa sana cha ' Simu ya Kifo'. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa John Katalambula mwanae marehemu.
Ewe Mwenyezi Mungu ilaze Mahali Pema Peponi roho ya marehemu, Amen.
NB: Nimeambiwa kuwa atazikwa leo huko Isevya, TABORA. R.I.P. Faraj Katalambula.
I believe Pili Pilipili was and to me is the best Play, yaani ukiisoma ile kitu huwezi weka chini hadi last page, tumepoteza shujaa wengi wa waliobakia ni wale wa kukopi na kupesti hadithi toka kwenye mtandao..... sorry kwa wanaomfahamu vizuri hivi ndie huy huyu alieandika na ile riwaya ya SIRI ya SIFURI???
Mungu Aiweke Pema Roho yake.
Kwa nini mgomo usihusike na ikiwa amefariki Juzi, madakitari wameanza kazi leo.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Dah! Faraji namfahamu sana, siyo ndugu yangu ila ninamfahamu kwa karibu mno tangu utotoni akiwa anaishi pale Tabora miaka ile ya sabini na baadaye tukakutana naye hapo Dar akiwa anaishi Sinza pamoja na mdogo wake Profesa Katalambula wa hapo UDSM.
Faraji alikuwa mtu mwenye akili sana ila nadhani hakupata mazingira mazuri ya kutumia akili hio. tangu alipoandika majarida ya Film Tanzania mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya sabini akiwa na characters za akina Unyeke, Tojo, Hamisa na Amina kabla hajamalizia na ile ya Simu ya Kifo, hakujatokea watunzi wengi wenye mvuto wa aina hiyo zaidi ya yule mtunzi wa Kuli, na labda na Profesa Kezilahabi. Akina Musiba, na wengineo wote walikuwa ni wanafunzi tu meble ya nguli huyu; kitabu chake cha simu ya Kifo kilitumika katika kutoa elimu ya uandishi wa vitabu vya kiswahili kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mungu ailaze pema peponi roho ya merehemu.