Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Aliyekuwa mtunzi mahiri wa vitabu vya hadithi na riwaya nchini Tanzania
marehemu Mzee Faraj Katalambula (kulia) anatazamiwa kuzikwa kesho
Isevya mkoani Tabora majira ya saa kumi jioni.
Faraj Katalambula alifariki juzi saa kumi na mbili jioni katika hospitali ya rufaa Muhimbili.
Faraj Katalambula ambaye ni mmoja wa watunzi wa vitabu mahiri kupata
kutokea atakumbukwa zaidi kwa utunzi wake wa kitabu
kilichosomwa sana cha ' Simu ya Kifo'.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa John Katalambula ambaye ni Mtoto wa Marehemu.
Ewe Mwenyezi Mungu ilaze Mahali Pema Peponi roho ya marehemu, Amen.
NB: Nimeambiwa kuwa atazikwa leo huko Isevya, TABORA. R.I.P. Faraj Katalambula.