TANZIA Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya Afariki dunia

RIP. Chrisant mzindakaya Maji ya Tanga nukumbuka 2010 ulituuliza swali kwamba walio hai na walio kufa wengi wepi.tulipokujibu walio kufa ukasema basi umeshashinda ubunge kwakuwa wafu watakuchagua

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app

Ha ha ha zee chawi sana hili.
 
Crisant Majiyatanga Mzindakaya aliijeruhi vilivyo Serikali ya Mkapa ilipoanza kujihusisha na rushwa mwaka 1996.
Waziri wa Fedha Profesa Mbilinyi, Waziri wa Viwanda Juma Ngasongwa, na manaibu Kilontsi Mpologomyi, walikuwa Mawaziri wa mwanzo kwenye serikali ya awamu ya tatu kutoswa kutokana na kashfa alizoibua bungeni mh Mzindakaya.
Pumzika Mzindakaya, binafsi nitakukumbuka kwa kazi yako hiyo
 
Yale Yale ya dhalimu kuweka mkwara mzito kwa mgombea mwingine kwa kumtisha au hata kujidai atamnunua kisha kuingia mitini.
Enzi zake nasikia ilikuwa marufuku mtu mwingine kugombea ubunge jimboni Kwake aliwatisha na ndumba.
 
Sote ni wapitaji huwa nashangaa mtu anamuua mwenzake hali nae ni mpitaji
 
View attachment 1811771
Wandugu.
Mwanasiasa mkongwe humu nchini bwana Christian mzindakaya amefariki dunia. Mzindakaya amefariki jioni hii katika hospital ya taifa ya Muhimbili ulipokuwa akipatiwa matibabu.

Wakati wa uhai wake bwana Mzindakaya aliwahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo kuwa mbunge wa Sumbawanga kwa miaka mingi.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa.

Dk Crisant Majiyatanga Mzindakaya, aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1965 kama Mbunge wa Jimbo la Ufipa Kusini, lakini mbio zake ziliingia doa mwaka 1981 baada ya mahakama kumvua ubunge kutokana na ushindi wake wa mwaka 1980 kwamba alitumia faulu.

Lakini mwaka 1982 alirejea bungeni kwa 'mgongo' mwingine baada ya kuteuliwa na Rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, wakati huo wakuu wa mikoa walikuwa wanaingia bungeni moja kwa moja.

Katika historia ya bunge, mbunge huyo hawezi kusahaulika, baada ya kujijengea umaarufu kama mzee wa mabomu wakati wa enzi za utawala wa serikali ya awamu ya tatu, alipokuwa akifichua ufisadi mbalimbali ndani ya serikali.

Dk Mzindakaya atakumbukwa zaidi alipomlipua aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Iddi Simba, kutokana na kashfa ya sukari iliyosababisha waziri huyo kujiuzulu.

'Mabomu' mengine ambayo yalimjengea umaarufu zaidi ni pale alipomlipua aliyekuwa Waziri wa Fedha, Profesa Simon Mbilinyi na hatimaye kujiuzulu na kwenye kikao cha bunge kinachoendelea amerusha 'bomu la mkono' kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, ambalo madhara yake ni kidogo.

Hata hivyo, baada ya 'kulipua' wenzake kwa muda mrefu naye alianza kugeukiwa akidaiwa kukopeshwa fedha kwa ajili ya kujengea kiwanda cha kusindika nyama mkoani Rukwa na kudhaminiwa na Serikali ambazo ilidaiwa hakurudisha

Zaidi, soma:

1 Mzindakaya:Mbunge wa muda mrefu CV yake hii hapa
View attachment 1811793
Aliiba fedha nyingi. Haya majizi yakipungua angalau huenda wanangu wakabadili mfumo huu wa kijambazi uliowapa nafasi ya kuhujumu taifa na kufa na mali zetu.
 
"Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe." - Ayubu

Alale salama Mzee Mzindakaya
Pole Kwa familia, na wote walioguswa na msiba huu
Sabaya na bashite injili hii wao ngumu kuelewa
 
Huyu na Lyatonga walikuwa watu machachari sana kwa CCM pamoja na wao kuwa CCM, kabla ya Lyatonga kufuata njia zake za siasa za upinzani...
 
Mbali ya madhaifu yooote aliyowahi kuwa nayo lakini alikuwa na moja kubwa katika uanasiasa wake!! Hakuwa mbaguzi wa kiitikadi.
 
View attachment 1811771
Wandugu.
Mwanasiasa mkongwe humu nchini bwana Christian mzindakaya amefariki dunia. Mzindakaya amefariki jioni hii katika hospital ya taifa ya Muhimbili ulipokuwa akipatiwa matibabu.

Wakati wa uhai wake bwana Mzindakaya aliwahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo kuwa mbunge wa Sumbawanga kwa miaka mingi.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa.

Dk Crisant Majiyatanga Mzindakaya, aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1965 kama Mbunge wa Jimbo la Ufipa Kusini, lakini mbio zake ziliingia doa mwaka 1981 baada ya mahakama kumvua ubunge kutokana na ushindi wake wa mwaka 1980 kwamba alitumia faulu.

Lakini mwaka 1982 alirejea bungeni kwa 'mgongo' mwingine baada ya kuteuliwa na Rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, wakati huo wakuu wa mikoa walikuwa wanaingia bungeni moja kwa moja.

Katika historia ya bunge, mbunge huyo hawezi kusahaulika, baada ya kujijengea umaarufu kama mzee wa mabomu wakati wa enzi za utawala wa serikali ya awamu ya tatu, alipokuwa akifichua ufisadi mbalimbali ndani ya serikali.

Dk Mzindakaya atakumbukwa zaidi alipomlipua aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Iddi Simba, kutokana na kashfa ya sukari iliyosababisha waziri huyo kujiuzulu.

'Mabomu' mengine ambayo yalimjengea umaarufu zaidi ni pale alipomlipua aliyekuwa Waziri wa Fedha, Profesa Simon Mbilinyi na hatimaye kujiuzulu na kwenye kikao cha bunge kinachoendelea amerusha 'bomu la mkono' kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, ambalo madhara yake ni kidogo.

Hata hivyo, baada ya 'kulipua' wenzake kwa muda mrefu naye alianza kugeukiwa akidaiwa kukopeshwa fedha kwa ajili ya kujengea kiwanda cha kusindika nyama mkoani Rukwa na kudhaminiwa na Serikali ambazo ilidaiwa hakurudisha

Zaidi, soma:

1 Mzindakaya:Mbunge wa muda mrefu CV yake hii hapa
View attachment 1811793
Faulu ya UBUNGE wake Mwaka 1980 ilikuwa ni RUSHWA Usifiche Maneno
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom