TANZIA Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya Afariki dunia

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
10,526
13,015
images.jpeg
Wandugu,

Mwanasiasa mkongwe humu nchini bwana Christian mzindakaya amefariki dunia. Mzindakaya amefariki jioni hii katika hospital ya taifa ya Muhimbili ulipokuwa akipatiwa matibabu.

Wakati wa uhai wake bwana Mzindakaya aliwahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo kuwa mbunge wa Sumbawanga kwa miaka mingi.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa.

Dk Crisant Majiyatanga Mzindakaya, aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1965 kama Mbunge wa Jimbo la Ufipa Kusini, lakini mbio zake ziliingia doa mwaka 1981 baada ya mahakama kumvua ubunge kutokana na ushindi wake wa mwaka 1980 kwamba alitumia faulu.

Lakini mwaka 1982 alirejea bungeni kwa 'mgongo' mwingine baada ya kuteuliwa na Rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, wakati huo wakuu wa mikoa walikuwa wanaingia bungeni moja kwa moja.

Katika historia ya bunge, mbunge huyo hawezi kusahaulika, baada ya kujijengea umaarufu kama mzee wa mabomu wakati wa enzi za utawala wa serikali ya awamu ya tatu, alipokuwa akifichua ufisadi mbalimbali ndani ya serikali.

Dk Mzindakaya atakumbukwa zaidi alipomlipua aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Iddi Simba, kutokana na kashfa ya sukari iliyosababisha waziri huyo kujiuzulu.

'Mabomu' mengine ambayo yalimjengea umaarufu zaidi ni pale alipomlipua aliyekuwa Waziri wa Fedha, Profesa Simon Mbilinyi na hatimaye kujiuzulu na kwenye kikao cha bunge kinachoendelea amerusha 'bomu la mkono' kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, ambalo madhara yake ni kidogo.

Hata hivyo, baada ya 'kulipua' wenzake kwa muda mrefu naye alianza kugeukiwa akidaiwa kukopeshwa fedha kwa ajili ya kujengea kiwanda cha kusindika nyama mkoani Rukwa na kudhaminiwa na Serikali ambazo ilidaiwa hakurudisha

Zaidi, soma:

1 Mzindakaya:Mbunge wa muda mrefu CV yake hii hapa

 
Wandugu.
Mwanasiasa mkongwe humu nchini bwana Christian mzindakaya amefariki dunia. Mzindakaya amefariki jioni hii katika hospital ya taifa ya muhimbili ulipokuwa akipatiwa matibabu.
Wakati wa uhai wake bwana mzindakaya aliwahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo kuwa mbunge wa sumbawanga kwa miaka mingi.
Bwana ametoa, beans ametwaa .

"Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe." - Ayubu

Alale salama Mzee Mzindakaya
Pole Kwa familia, na wote walioguswa na msiba huu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom