Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,498
Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere, Joseph Butiku, amewataka Watanzania kukubaliana na uhalisia kwamba nchi tayari ina Rais aliye tayari kwa maridhiano.
Butiku ametoa kauli hiyo leo Machi 4, 2026, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Maridhiano (Maridhiano Day) yaliyofanyika katika ukumbi wa Kwa Tunza, wilayani Ilemela, mkoani Mwanza.
Akizungumza katika hafla hiyo, amesema kuwa tume iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeongezewa muda hadi mwezi Aprili, na kuwataka wananchi kuwa na subira.
“Nimesikia tume iliyoundwa na Rais Samia imeongezewa muda mpaka mwezi wa nne (Aprili). Tukubali tusubiri aje atuambie jambo na lije litusaidie kwenye mazungumzo,” amesema Butiku.
Aidha, amewataka viongozi wa dini nchini kuendelea kuhimiza haki na amani kwa wakati mmoja, akisisitiza kuwa hakuna amani ya kweli bila haki.