Mzee Bulembo acha kudhalilisha watu kwa kuharibu diplomasia wakati wewe ndio muharibu

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Kutokana na uchu na tamaa ya madaraka mzee wangu Abdalah Bulembo na wengine wanakuita alhaji ulitoa kauli ambayo iliishtua dunia na pengine dunia kuamini Tanzania ni nchi ambayo serikali inaua watu wanaohoji pesa za miradi

Kufuatia mkopo wa benki ya dunia(WB) kwenye mambo mbalimbali ambayo yangechochea maendeleo hususani suala la watoto wa like waliopata ujauzito kurudi shule ambalo ni suala ambalo uongozi uliopita haukuliona lipo sawa, zitto kabwe aliitoa maoni yake juu ya sharti hilo kutofanyika kwa kilichokusudiwa kwa mkopo huo na kuomba usitishwe.

Kufuatia maoni hayo ya zitto tarehe 03/02/2020 mzee bulembo ulitoa kauli hii, nanukuu: "Kuna mtu mmoja aliyechukua maswala yetu ya ndani na kuyapeleka nje ya taifa , hafai kuruhusiwa kurudi na anafaa kuuawa pale alipo .Uhaini! kile ambacho bwana Zitto Kabwe amekuwa akilifanyia taifa hili ni uhaini''.

Kauli yako hii ingeweza kuwa ni chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano yote ya kimataifa lakini haikuwa hivyo hivo kwa uongozi unaosema ulivunja mahusiano hayo ulijitahidi kwa gharama yoyote kuyalinda. Hakuna mahali popote Rais Magufuli au waziri Kabudi aliwahi kutotoa kauli yenye kuhatarisha na kuchochea kuvunjika kwa mahusiano hayo ila ni wewe ulifanya hivyo kwa sababu ya uchu ulionao wa madaraka.

Napenda kukumbusha tu mzee bulembo katika uongozi wa hayati Magufuli mahusiano yetu na nchi nyingine yalikuwa ni imara sana hivyo tunajisikia aibu mzee kama wewe unapojaribu kupotosha umma kwa maslahi ya tumbo lako.

Tunaomba ukae kimya na uache kumuongelea vibaya hayati Magufuli kwa sababu utaishia kudhalilika na kuabika hata kwa wajukuu zako ambao wanaona mazuri yake kwa nchi hii.
 
Huyo mzee kaletwa ili walio nyuma ya Polepole wajitokeze. Unfortunately kuna angle CCM inajipeleka tuombe ifike huko ili wasambaratike. Mpasuko ni mkubwa na unapoelekea itakuwa worse.
 
Wakati Wa Mzilankende Nakumbuka Huyu Bulembo Alipigwa Bit Kali Na Rashid Gwajima Akafyata Mkia
Aliambiwa Abdallah Nakuonya, Ukisema, Nikisema Nchi ITATIKISIKA Nayajua Yote

Ilikuwa Kahama, Basi Bulembo Alifyata Mkia Kama....
Ko Ko
 
Huyo mzee kaletwa ili walio nyuma ya Polepole wajitokeze. Unfortunately kuna angle CCM inajipeleka tuombe ifike huko ili wasambaratike. Mpasuko ni mkubwa na unapoelekea itakuwa worse.
Naona wafuasi wa jiwe akili zimeanza kuwarudi mdogo mdogo.
 
Back
Top Bottom