Mzee aliyetoa zawadi ya Jogoo, apanda gari kuja kumuaga Rais Magufuli, Dar

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mnamkumbuka yule mzee aliyempa Magufuli zawadi ya Jogoo kule Kilwa? Mzee Shaweji Kimbwembwe amepanda basi kutoka huko kijijini kwao kuelekea Dar ili apate fursa ya kumuaga Rais Magufuli.

Alimpa Rais Magufuli Jogoo baada ya kuelezea kadhia ya huduma hafifu za afya katika eneo lake la Somanga ikiwemo kina mama wanaojifungua wakati Rais akisalimia wananchi katika ziara zake. Rais Magufuli alimpa ahadi ya kujenga kituo cha afya na kutimiza ahadi hiyo.

Ndipo Rais alipopita kwa mara nyingine wakati akitoka kwenye mazishi ya Rais mstaafu, hayati Benjamin Mkapa akamzawadia Jogoo kwa kutimiza ahadi yake na kumuomba ampelekee mama yake mzazi Chato kwa kumfundisha wema na huruma kwa wanadamu, pia alimtabiria ushindi kwenye uchaguzi wa 2020.

Rais Magufuli alimpokea jogoo na kumtania kwamba siku akienda Chato atamkabidhi mama yake ali awe baba yake

I pray awahi kufika ili, asijekuta washaelekea Dodoma, roho yake ikamuuma.

Rais atasafirishwa kuelekea Dodoma, saa 11 jioni

PIA, SOMA=> Somanga: Rais Magufuli asikitishwa na uzembe wa Wizara ya Ujenzi kutokarabati barabara Somanga. Azawadiwa jogoo


 
Nasikia yule ni mzee wa kitengo.
Lile tukio lilikuwa staged.

Watonyaji wanasema yule mzee yuko kwenye TISS payroll kwa miaka mingi. Lakini analipwa pesa kidogo sana.
Wanaomjua wanasema ameshaishi maeneo mengi hapa Tz, na kila eneo alilofika anajifanya ni mwanakijiji, anatafuta ubini ili aonekane ni mzawa na anapiga mishe zake, watu wakimshutukia tu anahama!
 
Muda wa kushika fedha umewadia muda wa Siasa za Propaganda umekwisha
giphy-3.gif

Vipara watupu!
 
Back
Top Bottom