Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,039
12,364
Inahuzunisha sana kuona kazi wafanyazo watoto waliosomeshwa kwa gharama wakiwa bodaboda na wachoma chips.

Mzazi kugharamia masomo ya mwanao ili aje kuwa mpambaniaji wa kazi hizo na za namna hiyo au kutokuja kuwa na future yoyote mtaani inaleta huzuni kwa mtoto mwenyewe hata kwa mzazi pia.

Wanasiasa hawafanyi ujinga huu kamwe wao na kizazi chao wanaandaliana future bora watoto wao. Hakuna mwanasiasa hata mmoja ataruhusu mwanae awe boda boda au mchoma chipsi wala kutanga tanga mtaani hovyo bila future yoyote ile.

Mzazi jukumu lako lisiishie kuzaa na kupeleka mtoto shule pekee bali muandalie na future bora mtoto wako.

[IMG alt="lukesam"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/275/275627.jpg?1500562796[/IMG]

lukesam

JF-Expert Member​

  • "Hatuwezi kuwa matajiri wote kama Bakhresa lakini ni vizuri sisi watu weusi tukajifunza kwao na jamii nyingine kama za wahindi.
Inawezekana wazee wetu walishakosea huko nyuma ila sasa ni muda wa kujisahihisha na kuwa bora kuliko wao.

Wazazi wa kiafrika wana tabia za kichoyo na kibinafsi, hata akiwa na duka lake hataki mtoto wake auze au ajue jinsi ya kuendesha biashara, anaogopa kuibiwa hata kijana wake hamuamini.

Watoto wetu wanahangaika sana kutafuta ajira kwasababu walienda shule kusomea taaluma za ndoto zao bila kujua baada ya kumaliza wataenda kufanyia kazi wapi. Tofauti na sisi, hawa wenye asili ya kihindi na matajiri wengine, watoto wao wanaenda shule kusomea taaluma ambazo wanajua wakitoka hapo wataenda kupata ajira kwenye miradi ya familia.

Tuweke nguvu katika kuanzisha miradi ya kifamilia, familia za kitanzania tuache ubinafsi. Ndio maana hata ukimshauri mtu aandike wosia au agawe mali zake akiwa hai anakushangaa, mzee kabisa anataka afe akiwa anamiliki mali zake zote.

Suluhisho la kusomea uhasibu au uchumi na kuishia kuwa muuza chipsi au bodaboda ni kuanzisha miradi ya kifamilia. Binafsi naona hii itapunguza sana tatizo la ajira na hali ya umaskini katika familia zetu.

Inaumiza sana kupoteza miaka mingi shuleni na kuishia kufanya kazi ambazo hata hazihitaji elimu".
 
Inahuzunisha sana kuona kazi wafanyazo watoto waliosomeshwa kwa gharama wakiwa bodaboda na wachoma chips.

Mzazi kugharamia masomo ya mwanao ili aje kuwa mpambaniaji wa kazi hizo na za namna hiyo au kutokuja kuwa na future yoyote mtaani inaleta huzuni kwa mtoto mwenyewe hata kwa mzazi pia.

Wanasiasa hawafanyi ujinga huu kamwe wao na kizazi chao wanaandaliana future bora. Hakuna mwanasiasa hata mmoja ataruhusu mwanae awe boda boda au mchoma chipsi wala kutanga tanga mtaani hovyo bila future yoyote ile.

Mzazi jukumu lako lisiishie kuzaa na kupeleka mtoto shule pekee bali muandalie na future bora mtoto wako.
Mkuu hii imekaa poa. Lakini changamoto kuna familia unaweza ukadondosha chozi kwa hali waliyo nayo. Hata hiyo kuandaa future ya mtoto wanaiandaaje zaidi ya kumpeleka shule tu?

Labda kama watamfundisha shughuli ambazo wao wanafanya ili nae aje kuendeleza. Kama ni kupasua mawe basi nae aishi humo, kama ni uvuvi aishi humo pia.

So sad for sure
 
Mkuu hii imekaa poa. Lakini changamoto kuna familia unaweza ukadondosha chozi kwa hali waliyo nayo. Hata hiyo kuandaa future ya mtoto wanaiandaaje zaidi ya kumpeleka shule tu?

Labda kama watamfundisha shughuli ambazo wao wanafanya ili nae aje kuendeleza. Kama ni kupasua mawe basi nae aishi humo, kama ni uvuvi aishi humo pia.

So sad for sure
Hiyo nayo option nzuri kama familia haina uwezo kabisa wajaribu hata kazi wanazofanya wawapatie ujuzi watoto wao.

Wazazi wanao fanya biashara,kilimo hata ndogo ndogo wasiwafiche watoto wao waanze kuwaandalia mazoea na usimamizi bora wa hizo kazi mdogo mdogo
 
Hoping is not a strategy
I hate hope. Kuna kauli nazichukia sana. Sijui ni mipango ya Mungu. Sijui kwa mapenzi ya Mungu. Sijui jipe moyo tu mambo yataenda sawa, komaa tu utafanikiwa, hazina uhalisia kabisaaaaaaaaaaaa https://jamii.app/JFUserGuide https://jamii.app/JFUserGuide that's why kuna mijitu haiamin hata uwepo wa Mungu mtu anakwambia tu sijui tumwachie Mungu utapata kazi tu ukicheck huna Connection, huna pesa ufukara kuanzia ngazi ya familia, connection ulizonazo hazina maana huthaminiw huna kitu mtu kitu....
 
Changamoto ya ajira inaanzia hapa. Wazazi wetu wengi ni masikini kipato cha chini kabisa na wametusomesha kwa kuunga unga. Hawana connection zakutosha na walizonazo hazina uzito tokana na walicho nacho, tunaelewa mtu kitu.
Tatizo la ajira in broader ni kubwa. Mbaya zaidi hsuluhu làke linalitoa kuwa tatizo la kila mtu na kuwa tatizo la watu Fulani wenye sifa zinaxofanana.

Muhimu ni kukumbuka kwamba the aim higher the bigger achievement. Mm naona watoto wa maskini kama tunazikomalia siasa. Huko utakuwa karibu zaidi na wanufaika wa mfumo
 
Back
Top Bottom