My upcoming trip to Jordan

My upcoming trip to Jordan

Ohhhh thanks.

That will be easier


Oukey acha kwa kifupi nishirikishe moja ya safari nilizoenda nje ya Tanzania. Ilikuwa miaka mingi tuu huko nyuma na nilienda Italy eneo la Milano au Milan.

Nilikuwa mwenyewe, safari niliiandaa kwa mwaka mzima kwa maana ya booking ya ndege nilitumia KLM, hoteli nilibook online nikachagua hoteli zilizokuwa na offer. Nilienda msimu wa mwezi wa 12 hivyo kubook mapema ilinisaidia kupata hoteli ya bei rahisi. Mara nyingi huwa napenda kukaa eneo ambalo naweza kutumia usafiri wa uma kutoka airport ili nijionee mambo na kujifunza na kushangaa humohumo bin kutoa ushamba.

Nilikaa kule kwa wiki mbili kamili yaani siku 14 ukitoa siku za kusafiri na nilifanikiwa kufika miji mingine ya Italy kwa kutumia usafiri wa Treni.

Kitu kikubwa ni kuzingatia afya yako, pamoja na kukata bima ya afya ya muda ila huwa natengda hata dola 200 kwa ajili ya matibabu incade unagonjweka.

Na mwezi mmoja kabla ya safari nafika zahanati za serikali wananifanyia vipimo kujihakiki niko fit kusafiri (hasa kwa sie umri ulioenda maana waweza kaa kwenye ndege mkifika miguu hainyanyuki kumbe misuli imekakamaa kwa kukaa mkao mmoja muda mrefu eehehehehe) hapa ndo utatambua umuhimu wa business class na first class.
Japo huwa najiuliza mbona kwenye ndege hakunaga second class??

Tuachane nalo, mnaona siweki gharama maana nimejaribu kutafuta nyaraka sizioni na sikumbuki jumla ilinigharimu kiasi gani.

Ila kupanga safari mwaka mmoja kabla au miezi sita kabla unasevu gharama kubwa tuu.
 
Kasie,
Ahsante kwa ku-share mkuu. Hongera sana pia maana kusafiri sio utani.

Ndio kama nlivyosema mimi, safari zangu napanga well in advance kwa sababu kuziandaa hizi ni very stressful
 
Experience ya Dar - Greece

Kwa kifupi safari hii niliiandaa kwa mwaka , tulipanga kusafiri na mfanyakazi mwenzangu (travel buddy yeye yupo ofisi ya Burkina Faso ) huwa tunapanga hivi kwa kuwa yupo fluent in French na Mimi Kingereza ili tukipita maeneo tuwe na wa kusaidiana.

Nilibook KLM well in advance - na nilisafiri mwezi wa tano . Destination yetu ilikuwa kisiwa kiitwacho Eretria huko kaskazini mwa Athens. Ni kisiwa chenye historia sana ya vita, starehe, dini , uhamiaji nk. Na ndipo kitovu cha yale mameli makubwa ya starehe ya kigiriki yalipoanzia. Kisiwa hiki watu wake ni wakarimu mnooooo na wala hamna ubaguzi kabisa. Wengi wanafahamu kifaransa na kigiriki chao - kingereza ni kidogo.

Tulikaa one week hapo na kurudi Athens kukaa siku 3 kutembelea sehemu za historia kama makumbusho makubwa ya ugiriki (Acropolois Museum) dah haya makumbusho unaweza enda siku nzima na usimalize kuna historia kubwa ya mediteranean Europe.

Katika vitu vikubwa nilivipenda ni hospitality, food - mediteranean food, muziki wao una flava ya kizungu na kiarabu , historia na hali ya hewa mwezi wa 5 ni nzuri sana .

Gharama sijaweka maana hadi nirejee ka diary kangu ka mwaka juzi.

Nadhani itatoa mwanga
 
Mwaka huu wakati nachagua destination nliangalia Madagascar na Seychelles lakini nkaona wako ghali kiasi flight zao.

Cape town pako poa and it's cheap to go but hiyo issue ya xenophobia imechafua hali.

Morocco kuna mji wao unaitwa Marrakech naskia uko poa

Morocco ndio nchi ambayo sasa watalii wote wanakimbilia
Kwa sababu sio tu bei ni reasonable ila hata chakula ni kizuri sana na ni patulivu sana na amani
Europeans wote wanajimwaga huko
Na sehemu nyingine nzuri ni Turkey
Kuanzia Antalya, Cappadocia na Istanbul
 
Mimi napenda sana kusafiri, kwenda kutalii sehemu tofaut tofaut na kujifunza mambo mapya kwa kweli ninapenda ....huwa nikisikia nina safari ya kwenda sehemu fulani huwa nafurahi km ni baada ya wiki basi natamani nisogeze siku ziende haraka haraka
 
Kumbe??? I didnt know this aiseee

Mkuu wazungu wengi wamenunua mpaka nyumba huko na sio wazungu tu hata mataifa mengine
Fursa hizi za kununua nyumba zimekuwa ndio fashion kwa wengi kuanzia Dubai mpaka Morocco, Spain France na turkey
Hapo mtu huna haja tena ya kushukia hotel
Na wengine wamezikodisha na wakifika umri wa kustaafu wanaenda huko kumalizia mda wao wa kuishi chini ya jua
 
Mimi safari zangu za hapa hapa ndani halafu leo nina safari naianza saa 12 jioni.
Twin unakumbuka ile issue tulioongea last weekend ukanishauri nikakwambia next weekend ndio kita "happen"?
My prayers are with you babe..!!
Nipo for the time being fanya ukuje kule, kabla lile balaa halijanikumba tena.!!
 
Na wewe MLEVi Mmoja njoo basi utupe experience ya kule Patong na Pattaya bhana acha kuwa mchoyo maana sijaona aliyepaongelea

Ila tu usije na story zako za wale makahaba wazuri uliowanunua kule wewe njoo na story za mandhari tu pakoje na kuenda kule inagharimu kiasi gani
 
Sasa bro Relief Mirzska kuna mtu kaniambia anataka kuenda sehemu nzuri kwa ajili ya holiday na hajui ni wapi hivyo kaniomba nimsaidie kupanga

Budget yake ni $6000 na mimi kama unavyonijua siyo mzoefu sasa naomba msaada wa kupanga ni wapi panamfaa ili nikamuambie
 
Na wewe MLEVi Mmoja njoo basi utupe experience ya kule Patong na Pattaya bhana acha kuwa mchoyo maana sijaona aliyepaongelea

Ila tu usije na story zako za wale makahaba wazuri uliowanunua kule wewe njoo na story za mandhari tu pakoje na kuenda kule inagharimu kiasi gani
Nlienda Pattaya mwaka Jana November aisee. Around saa nane usiku nipo maeneo, hakufai kule mkuu

🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hii mada hatari sana,Kwa mwaka huu sijatoka ndani ya mkoa niliko(Iringa) nachukia sana kusafiri hasa hizi safari za basi..Eti Iringa to Bukoba dahh
 
Naona tu mnavyorushiana huu mpira
Sawa mie nitakutembeza niambie lini uko tayari nikukatie ticket ya ndege kabisa halafu ukishatua pale JNIA nakupokea na msafara wa SUVs 10 za maana ambazo bei yake si chini ya million 100 kila moja halafu tunazunguka jiji zima (in Kiduku Lilo's handwriting)
 
Back
Top Bottom