My upcoming trip to Jordan

Kwa sie tunaopenda adventure ,umeniongezea points,,kwa middle east napenda kufika Egypt,uae,katar ,na Israel
Asia natamani kufika china,Malaysia,Singapore,ufilipino,Maldives,Thailand na Vietnam
Ulaya napenda nifike uingereza,Germany,Italy,Belgium,switzland,France na Scandinavia countries
Amerika napenda kufika USA,Canada,panama,
Bila kusahau Japan,Chile,peru,Trinidad and tobago,na Australia
Afrika natamani kufika Ethiopia,Nigeria,Ghana,code voire,Senegal,moroco,Botswana,Namibia,angola na Mauritius,cape Verde na saotome and principal
Hadi sasa nimefika Kenya,Zambia na Malawi tuu..Hope kabla sijaingia kaburini nizitembelee hizo nchi,Mungu nisaidie
 
20191104_100356.jpg


Ama kweli kutembea ni kusoma. Elimu hii huwezi ipata kwenye vitabu. Nipo nchi flani hivi, nimekutana na dereva uber alieishi Zanzibar for five years na akaamua kuondoka na kuja nchi hii. Tumeongea sana. Nitegee sikio uelimike na upate nguvu na ujasiri na imani ya kwamba hata Tanzania unaweza ukatoboa pia
 
Hii ni nchi miongoni mwa nchi zilizopo Arab gulf, huyu jamaa kiasili ni M-Pakistan, amekuja hapa 2 years ago na kazi yake ni kuendesha uber. Gari hii ameinunua kwa pesa zake mwenyewe na ameinunua 2 years ago kwa thamani ya $55,000/= ikiwa ni zero km. Ila ili apate permit ni lazima aioneshe serikali kwamba yuko chini ya udhamini wa raia wa nchi hii ambae anakuwa kama guarantor and always a boss.

Yanayoendelea ndani ya nchi hii ni ya kusikitisha sana. Waafrika na watu wa Asia hawako-treated na sawasawa na wazungu au watu kutoka Europe. Jamaa ananiambia, maximum salary from a very good and respected company ambayo ina-deal na security services kwa raia from Africa or Asia ni around 1.85M gross. Ila kazi hiyo hiyo akipewa mzungu basi salary yake itakuwa mara mbili ya huko.

Jana wakati nipo kuzunguka na gari yake akanieleza kisa cha raia wa Pakistan aliekaa miaka 15 hapa akitafuta maisha na baadae akadhulumiwa lori zake 7 na huyo guarantor wake ambae alifanya juu chini kuhakikisha anakosa permit renewal ya permit yake. Inaskitisha sana kwa kweli.

Nimekutana na mama wa around 40-45 years old kutoka Philippines ambae ni receptionist kwenye hii hotel niliyopo sasa. Alivyomuona mtoto wangu akaniambia amemkumbuka sana mwanae, ana miaka 7 sasa hajamuona, nkamwambia kwa nini asichkue likizo aende Philippines akaniambia she needs to work every day ili aweze kumsomesha mwanae na kumshughulikia mama yake waliopo huko Philippines.

Mambo ni mengi sana wakuu na hakika tembea ujifunze
 
Kumbe upo huku?? Daah ule uzi wa selfie umenibana hadi nashindwa kuona notifications za nyuzi nyingine nilizochangia..I will my brother I will ngoja nianze kufanya mchakato mambo yakikaa sawa nakwea pipa yuleeeee next stop Dubai,, by the way nimekumiss..
Karma Fanya juu chini mkuu utembee. Mwenzio cute b anaandaa safari hivi
 
Kumbe upo huku?? Daah ule uzi wa selfie umenibana hadi nashindwa kuona notifications za nyuzi nyingine nilizochangia..I will my brother I will ngoja nianze kufanya mchakato mambo yakikaa sawa nakwea pipa yuleeeee next stop Dubai,, by the way nimekumiss..
Nipo huku ndugu yangu.

Napunga upepo kidogo, uzi wa selfie unatuma maselfie yako tu huku mimi umeninyima. Kweli tunafanyiana hivi??
 
Hilo swali naomba nikuulize na wewe ulipotelea wapi?? Nimekumiss mimi jamani yaani kuna watu nisipowaona JF hata siku mbili huwa nakosa mood ya kuchangia na mimi..
Haswaaaaa. Yeye mwenyewe nimeenda hadi nyumbani kwake sikumkuta nkapata wasiwasi ila mungu ni mwema Leo huyu hapa tupo nae
 
Huwa najiuliza, hivi hawa wanaojiita viongozi wetu wanavyokuja ziara za mafunzo huku kwenye nchi za watu wanakuwa wanakuja kujifunza nini actually?? Mwaka Jana nilipokuwa Malaysia nilizungumzia jambo dogo tu la namna parking za magari kwenye parking areas zao zilivyokuwa designed. They are designed in such a way hautakuta kamwe gari moja limempiga pin gari jengine kwamba haliwezi kutoka mpaka dereva wa lile gari aje.

Huku nilipo Leo, katikati ya mji kuna gardens ambazo zimetengenezwa in a way kwamba mtu unakaa unapumzika na kuangalia ukubwa wa uumbaji. Hii nchi ipo Jangwani lakini upatikanaji wa maji ni mkubwa kuliko Tanzania yenye mito na maziwa kedekede. Ndio maana kwa wenye namba yangu ya WhatsApp wataona jana nimeweka status inyosema "Politicians will never lie to me, I have seen enough "

Mwisho wa siku unaona ni kiasi gani viongozi wa hizi nchi ni wazalendo, uzalendo wao sio ule wa kulazimisha. Hawa ndio wazalendo haswa.
 
Huku kwetu kazi kutumbuana tu
Yaani kiukweli kabisa huko kwetu hao wanaojifanya wana uchungu na nchi au maendeleo ni na mashaka nao. Sidhani kama wana dhamira za dhati za kuleta hayo maendeleo.

Huku raia anaheshimika na anapewa priority over a foreigner or a visitor. Mkienda police mnakaa foleni kusubiri huduma. Akija tu mwenyeji basi nyoote mtasubiri kwanza ashughulikiwe yeye raia. Kwetu Sisi ni tofauti, mzungu ana thamani kubwa sana kuliko khantwe aliezaliwa hapo hapo na ambae analipa kodi constantly na ambae ndio mlinzi wa kwanza wa nchi yake, yaani huko kwetu kila kitu ni kinyumenyume
 
Siku moja nilikwenda wizara ya elimu, mmoja wa waliokuwa walimu wangu yupo pale, nilikuwa nimekasirika sana na issue flani hivi inayohusu elimu. Katika maongezi yangu, nilimwambia wazi kwamba "mwalim unajua fika ili kuikomboa jamii yoyote inabidi hiyo jamii ipewe elimu, mnachokifanya nyinyi kama wizara na serikali hakina tija kwa mwananchi. Kiukweli hanna dhamira ya dhati ya kuwakomboa wananchi. Yule mwalimu alikubaliana nami, kikubwa alichoniambia ni kwamba, sometimes things happen out of your control na nkawa nimemuelewa"
 
52 Reactions
Reply
Back
Top Bottom