Michael B. Jordan afuata Nyayo za 'Manguli', ashinda Oscar yake ya kwanza

Michael B. Jordan afuata Nyayo za 'Manguli', ashinda Oscar yake ya kwanza

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,965
download (1).jpg


Katika kinyang'anyiro kikali cha kuwania tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume (Best Actor), staa wa filamu ya Sinners, Michael B. Jordan, ameibuka kidedea kwenye Tuzo za 98 za Academy (Oscars) zilizofanyika usiku wa kuamkia Jumatatu.​

Katika filamu hiyo, Jordan ameigiza uhusika maradufu kama mapacha (Smoke na Stack) ambao mipango yao ya kufungua ukumbi wa muziki huko Mississippi miaka ya 1930 inaharibiwa na nguvu za giza. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Jordan kutajwa (kuwa nominated) na kushinda tuzo ya Oscar, akiwabwaga mastaa wengine wakubwa waliokuwa wakiwania kipengele hicho ambao ni Timothée Chalamet, Leonardo DiCaprio, Ethan Hawke, na Wagner Moura.

Mshindi wa mwaka jana, Adrien Brody (aliyeshinda kupitia filamu ya The Brutalist mwaka 2025), ndiye aliyepanda jukwaani kutangaza majina ya washiriki. Brody aliwavunja watu mbavu kwa kujifanyia utani kuhusu tabia yake ya kutoa hotuba ndefu sana za shukrani aliposhinda mwaka jana na aliposhinda mwaka 2003 kupitia filamu ya The Pianist.

Akitoa shukrani zake kwa mwongozaji wa filamu ya Sinners, Ryan Coogler, Jordan alisema: "Nina heshima kubwa kukuita mbia wangu na rafiki, umenipa fursa na mwanya wa kuonekana."

Jordan anakuwa muigizaji wa sita mweusi kushinda katika kipengele hicho. Katika hotuba yake iliyogusa hisia za wengi, alitoa heshima kwa kuwataja kwa majina washindi weusi sita waliotangulia kubeba tuzo za Muigizaji Bora wa Kiume na wa Kike, akieleza kuwa ni heshima kubwa sana "kuwa miongoni mwa hawa manguli."

"Nimesimama hapa kwa sababu ya watu waliotangulia kabla yangu - Sidney Poitier, Denzel Washington, Halle Berry, Jamie Foxx, Forest Whitaker, na Will Smith," alisema.

Alimalizia kwa kuwashukuru mashabiki: "Asanteni nyote mliopo kwenye ukumbi huu na wote mlioko nyumbani, kwa kuniunga mkono kwenye safari yangu ya sanaa. Ninazihisi hisia zenu, najua mnatamani nifanye vizuri, nami nataka kufanya hivyo kwa sababu mmeniamini na kuweka matumaini yenu kwangu."​
 
Back
Top Bottom