My upcoming trip to Jordan

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
13,988
22,379
Kwanza naomba ku-declare interest, miongoni mwa hobby zangu kuu ni kusafiri, kucheza/kuangalia mpira wa miguu na kufanya michezo ya baharini (watersports).

Kama msafiri, namshukuru Mungu kwamba hivi karibuni nitakuwa natembelea nchi yangu ya kumi duniani na hii ni kwa jitihada na malipo binafsi, yaani sisafirishwi na "sirikali". Kusafiri kuwa ni hobby yako ni kitu kimoja, na kuifanyia kazi hobby yako hiyo ili uweze kusafiri ni kitu kingine. Nimewahi mara kadhaa kusema humu jukwaani kuwa kusafiri sio ghali kama wengi wetu tunavyofikiria, kusafiri kunahitaji dhamira na mipango thabiti tu. Hivyo naomba niwasahihishe wale wote wakiwemo Karma na cute b na Devion na wengine wengi ambao kusafiri ni miongoni mwa hobby zao kwamba wazifanyie kazi hobby hizo.

Kuna mengi sana ya kujifunza kwenye kusafiri na elimu hizo mara nyingi haziwezi kupatikana kwa kusoma majarida na makala ziandikwazo na waliosafiri, ili kuzipata elimu hizo inabidi mtu aamue kusafiri ili kujifunza mapya duniani.

travel quote.jpg


Tuelekee kwenye mada:-
Binafsi, inapokamilika safari moja ndipo inapoanza mipango ya kituo changu kinachofuata, sizungumzii kituo kinachofuata ndani ya mwendokasi kuwa ni "kisutu" laa hasha! we are talking about big things here!!! fuatana nami.

Kutokana na baadhi ya sababu kadhaa wa kadhaa, nimechagua na kuamua kituo changu kifuatacho kuwa ni nchi ya JORDAN.

Kwa kifupi, Jordan ni nchi ya kiarabu iliyokuwepo magharibi mwa bara la Asia, kwenye kingo za mashariki za mto Jordan. Nchi hii inapakana na nchi ya Saudia Arabai katika upande wake wa mashariki na kusini, Iraq katika upande wake wa kaskazini mashariki, Syria upande wake wa kaskazini, pamoja na Israel na Palestinian west bank katika upande wake wa magharibi. Bahari maarufu iitwayo "dead sea" ipo katika upande wake wa magharibi na ile ya "red sea" ipo katika upande wake wa kusini magharibi. Mji mkuu wa nchi hii unaitwa Amman (kama uonekanavyo kwenye picha)

jordan at night 2.jpg


Jordan ni nchi yenye watu wapatao milioni kumi tu kwa census ya 2015 na ina wakimbizi wanaozidi milioni 2 kutoka Palestine, Iraq na Syria. Kuna mengi ya kusoma juu ya nchi hii ila ili kujifunza vividly inamuhitaji mtu kwenda kutembelea sehemu kama hizi.

Kuna sababu kadhaa zilizonifanya niichague nchi hii kama my next holiday destination kama zifuatazo.

1. AMMAN! THE CAPITAL CITY OF JORDAN

Mji huu ni miongoni mwa miji ya zamani sana iliyowahi kukaliwa huku ikiwa na historia iliyonakiliwa ya zaidi ya miaka 7000. Amman ni mji mkubwa kihistoria ambapo hapo zamani uliwahi kujulikana kwa jina la Philadelphia kama heshima kwa Ptolemy Philadelphus (ambae alikuwa ni mtoto wa Cleopatra) ambae aliujenga mji huu kabla haujachukuliwa na Herod mnamo miaka 30 B.C na kupewa kwa Warumi (Romans).

amman during the day.jpg


2. PAY RESPECT AT A HOLY PLACE

Moja ya sehemu ambazo ni tukufu kwa watu wa dini ndani ya Jordan ni mlima Nebo, hapa ni sehemu ambapo inaelezwa kuwa mtume Mussa/Moses ndipo alipoiona nchi ya ahadi "The promised land" . Kwa mujibu wa biblia, mtume Mussa/Moses alifia maeneo ya mlima Nebo akiwa na miaka 120 na alizikwa huko, ingawaje eneo la kaburi lake halijulikani exactly. Tangu muda huo wakristo wengi wamekuwa wakitembelea mlima huu ulioko magharibi mwa nchi ya Jordan ambapo sio mbali kutoka katika mji mkuu wa Amman. Kwenye kilele cha mlima huu kuna jiwe maalum la kumbukumbu ya mtume Mussa/Moses na kanisa la Byzentine ambalo lilijengwa na Monks katika karne ya 3 au 4 A.D

mount nebo 2.jpg


Mount nebo 1.jpg


3. STEP BACK IN TIME TO ROMAN EMPIRE

Ndugu yangu na wasafiri wenzangu, tusiishie tu kusoma vitu kwenye makaratasi na kujitengenezea picha zetu vichwani. Ni wakati sasa wa kwenda na kujionea wenyewe ukweli wa mambo juu ya yale tuliyoyasoma mashuleni, hapa PCM, PCB, CBG mtanisamehe. Roman empire ilikuwa ni miongoni mwa tawala kubwa na zenye nguvu sana duniani. Ilitawala eneo kubwa la dunia na kujenga mahekalu na ngome zao sehemu mbali mbali duniani. Nimeamua kwenda Jordan kujionea juu ya mabaki ya majengo madhubuti kabisa yaliyowahi kujengwa na wafalme wa kirumi.

Petra.jpg


Miji hii iliyokuwa chini ya utawala wa kirumi ilijengwa kwa ustadi wa hali ya juu katikati ya miamba migumu kabisa, ni miji ambayo imebaki mpaka leo na inathibitisha kuwa yale tunayoyasome sio hadithi za ibnuwas.

petra 2.jpg


4. THE ONLY LIVING SAHAB

Hapa naomba niwe muwazi kwamba kipindi flani mwaka 2018 nilipata kuangalia YouTube video ilikuwa na jina la "The only living Sahabi" yaani Swahaba pekee anaeishi ambayo inamuhusu Dr. Sule (muhadhir maarufu wa kiislam hapa Tanzania) ambae alipata nafasi ya kutembelea nchini Jordan na kufika eneo hili. Swahaba kwenye uislam ni yule mtu ambae aliishi na mtume (Muhammad s.a.w) hali ya kuwa ni muislam kipindi hicho ambacho mtume alikuwa hai.

Kutokana na video ile nilikuwa inspired sana na nikaweka dhamira kwamba siku moja nitakwenda nchini Jordan kujionea mambo haya.

Kuna mti ambao unasemekana upo eneo flani tangu kipindi mtume akiwa mtoto mdogo kabisa, alipita maeneo hayo akiwa na baba yake mdogo mzee Abi Taalib na baadhi ya watu ambao walikuwa wakienda nae katika safari ya kibiashara huko Sham kupitia Jordan ambako kutokana na miujiza iliyojitokeza alipofika eneo uliopo mti huu, baba yake mdogo alishauriwa amrudishe Mtume S.a.w huko Saudia ya sasa na kamwe asiendelee na safari kuelekea Sham.

Kuna maelezo mengi na atakaetaka kujua zaidi aende YouTube ila kwa kifupi miongoni mwa maajabu ya mti huu ni kwamba, 50 kilometers kila upande kutoka ulipo mti huu, hakuna mti mwengine wowote wenye urefu zaidi ya meter 2. na jengine ni kwamba 30 meters kuuzunguka mti ule kutoka kwenye shina popote utakaposimama basi kuna kivuli, hata kama umesimama nje ya mti ule.

Dhamira yangu ni kuelekea nchini Jorda kwenda kujionea mambo haya.

blessed tree.jpg


5. PANGO LA WATU WA KAHF (ASHABUL KAHF)/ THE PEOPLE OF THE CAVE

Kuhusiana na hili sitaki kuliongelea sana maana kupitia source nilizopitia, kuna mkanganyiko juu ya lilipo hili pango. Wapo wasemao kwamba lipo Jordan, juu ya kauli hizo na kupitia makala hizo, mimi binafsi nimeamua kutembelea nchi hii na kwenda kujionea eneo hilo lisemwalo kwamba ndipo hili suala lilipotokea.

ASHABUL KAHF 1.jpg


ashabul kahf 2.png


MY FLIGHTS TO JORDAN

Kama nlivyotangulia kusema, mipangilio inaanza sasa ikiwemo mambo ya research juu ya ticket ya ndege, hotel na mambo mengine.

Muda mzuri kusafiri kuelekea nchini Jordan ni kati ya mwezi March na May ambapo kule inakuwa ni kipindi cha Spring, au Autumn ambapo ni kati ya mwezi September na November. Ntachkua likizo yangu ya siku 10 ambazo zitanitosha kufanya trip yangu hii kuanzia tarehe 20th May mpaka 30th May.

Mnamo tarehe hiyo ipo ndege ya shirika la ndege la Egypt inayotoka Dar saa 05:20 am na itafika Amman- Jordan saa 07:10 pm siku hiyo hiyo. Siku ya kurudi ambayo ni tarehe 30th May, nitaondoka Amman saa 08:10pm na kufika Dar saa 04:20 am. Nauli ya ndege hii ni USD 571 ambayo ni sawa na TZS 1,300,000/= tu kwenda na kurudi.

Kwa utafiti wangu mdogo sana, hotel nzuri kabisa, itakugharimu kiasi cha shilingi 100,000/= za kitanzania kwa siku, na mpaka hapo ntakuwa tayari mguu moja nipo safarini kuelekea Jordan May 2020.

Bado sijafuatilia visa ya Jordan itanigharimu kiasi gani, lakini kwa wasafiri, hii inakuwa ni minor issue.

Kama nlivyotangulia kueleza ni kwamba, kusafiri ni miongoni mwa hobby za watu wengi sana duniani lakini ni wachache wanaofanikiwa kufikia malengo yao. Wengi hushindwa kwa sababu mbali mbali, lakini naomba niwashajihishe wadau kwamba "PESA" isiwe sababu ya kutofikia malengo yako ya kusafiri.

Natamani bandiko hili liwe ni chachu ya watu kusafiri kwani kupitia kusafiri ndio kunyafanya maisha yawe meaningful.

Wasalaam!

best quote.jpg
 

Attachments

  • Jordan at night.jpg
    Jordan at night.jpg
    9.3 KB · Views: 3
Going places ni moja ya vitu napenda, unfortunately i have never been to the middle East zaidi ya UAE...

Kuna wakati nishawahi kupata offer ya kazi Iraq na Bahrain nikatosa zote, Iraq ni vile hakukuwa na usalama na Bahrain nilitosa baadaye bila sababu ya msingi...

Kati ya vitu vipo kwa bucket list yangu ni hizi sehemu za historia za middle east, plus maeneo fulani ya magharibi mwa India ambapo wanapatikana settlers waliotoka East Africa miaka ya zamani, and some still preserve zile norms za Afrika Mashariki...
 
Watu8,
Mkuu, middle east kuna historia kubwa sana hususan kwa wafia dini. Ndio kuna history kubwa ya christianity na Islam huko.

Hongera mzee, Iraq as it stands haipo kwenye list yangu labda baadae huko lakini Bahrain mkuu mbona ulichemka kuiacha hiyo offer???

India is on my list japo sijui ni lini
 
Hahaha...ile offer came while i was pursuing mavitu mengine...haikuwa ridhiki mkuu
Mkuu, middle east kuna historia kubwa sana hususan kwa wafia dini. Ndio kuna history kubwa ya christianity na Islam huko.

Hongera mzee, Iraq as it stands haipo kwenye list yangu labda baadae huko lakini Bahrain mkuu mbona ulichemka kuiacha hiyo offer???

India is on my list japo sijui ni lini
 
Heheh hivi Kili ni kutalii kweli kule au ni some sort of enduring test

Ngorongoro ni sehemu poa sana nadhani kuliko vivutio vyote vipo Tanzania ikifuatia Serengeti
Bad for me hata sijawahi kufika huko. Hii haijakaa poa.

Naskia tu utalii wa ndani utalii wa ndani, once nlifanya saadani nkawa disappointed nkasema ndiyo yale yale tu.
 
Daah shukrani sana, keep on inspiring me bro nakuonea wivu ila ndiyo hivyo picha linaanza tu mimi passport sina na ninasikia ni ishu kupata kwa nchi yetu hii kwahiyo huwa naishia kufanya utalii wa ndani tu kwenye some national parks na historical sites na kutembelea bahari na milima ila Inshaallah Mungu akijalia I will work on my dreams.
Passport huna?? That can't be really.

Kweli???
 
Ningekuwa napanda ndege labda ningekuwa napenda, yaani sipendi aisee nikiwa na safari huwa nabaki kusogeza siku mbele
Duh! Wewe ni kijana wa kwanza kukuskia hupendi kusafiri, once nilitaka kuwaandalia safari my bosses waende Peru for a month wakapumzike, mzee akaniambia hawezi kusafiri na hapendi but yeye yupo 62 years old.

Sasa kama wewe hapo unaandaliwa kila kitu unakataaje sasa rafiki??
 
Back
Top Bottom