Wakuu naomba mnitoe ujinga kidogo ninvyoelewa mimi maana ya virus ni huwa kirusi hakifi kwa dawa yotote ile sasa unapopimwa viral load na kuambiwa unavirusi kazaa na unapoanza kutumia dawa viral load inaweza kuwa nil kama mnavyosema maana yake ikiwa nili virusi havione kani swala langu ni kama dawa zinafubaza na haziui virusi kwanini virusi visibaki vile vile vya mwanzo unapoanza kutumia dawa badala yake virusi vinapungua hadi viral load inakuwa undetected sawa vinakwenda wapi wakati dawa ni za kufubaza tu
Asante mkuu kwa swali zuri sana. Ndugu yetu amesema hakuna Daktari anayeweza kulijibu hili swali.. kama kawaida me nasema labda Daktari wa upande wa kwao.. Madaktari wa upande wa kwetu tunao upeo na uelewa japo ni mdogo.
Kabla sijakujibu labda niseme kuwa miongoni mwa masomo magumu "duniani" ni "immunology".. Samahani kwa kusema hivi japokuwa sina uelewa wa tasnia nyinginezo.. Kulielewa ni hadi udedicate muda wako na jitihada za kutosha sana.
.
.
Kuna kitu kinaitwa White Blood Cells na kuna kitu kinaitwa Latent HIV Reservoir. Nitajaribu kueleza kwa urahisi kadiri nitakavyobarikiwa
1. Life span (Siku za kuishi) ya white blood cells ni as early as 3 days to 6 or 9 months.. Kumbuka CD4 ni aina ya white blood cells ambazo life span yake ina average miezi 6.
2. Kufa kwa white blood cells: Zinauawa kwenye Lymphatic systems (Lymph nodes) kwenye spleen, brain, intestines etc
3. Kumbuka HIV infection anashambulia CD4 cells ambazo zinauawa na lymphatic system kwa wastani wa kila baada ya miezi 6.
4. Kumbuka kazi ya ART ni kuzuia HIV replication. Akizuia replication means no longer replications. Zile cells ambazo zimeshashambuliwa zinauawa baada wastani wa miezi 6 kwenye lymphatic system.
5. Kwavile huyu mdudu tumesema hafi, na kwavile kwenye damu kuna dose ya dawa muda wote inayozuia replication, hawa wadudu wanabaki at latent phase "latent HIV reservoir" kwenye ule mfumo unaoziua white blood cells
6. Ndiyo maana wataalam wakapendekeza tupime uwingi wa virusi vya UKIMWI mwilini "HIV viral load" baada ya kuwa kwenye dawa kwa zaidi ya miezi 6 tukitegemea % kubwa ya white blood cells zitakuwa zimeuawa and hence HIV amepelekwa kwenye latent phase.
Ndugu yangu amesema tunatekeleza tu yaliyoandikwa kwa miongozo ya WHO. Niseme kwamba miongozo haikuandikwa kwa kuotea otea.. kila kitu kina sababu zake. Muongozo unatuambia kupima viral load baada ya miezi 6 kwasababu hizi.
Zipo na sababu nyingine.
Just tried my best to make a difficult language understandable. Japo nakiri hii mada ya immunology ni ngumu sana. Siyo immunology in relation to HIV alone, bali kwa ujumla wake.
Asante.