My dream in Malawi, ndoto inayoweza kuwa movie bora kutoka Afrika 2024

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,923
2,002
Wakuu niko usingizini najikuta mimi na wanajeshi wenzangu (japo mimi sio mwanajeshi) tumetumwa nchini Malawi kupeleleza mienendo ya kikundi cha uasi kinachoweza kuzusha vita katika nchi hiyo.

Tukiwa katika kijiji kimoja ambacho kinakaliwa na waasi inatokea majeshi ya nchi hiyo wanashambulia kijiji kutokana na taarifa tulizowapatia,ghafla hali hiyo inazua tafrani kubwa kila mtu anajaribu kuokoa roho yake,wenzangu baadhi wanapoteza uhai.Mimi kwenye kuokoa roho yangu nakimbilia kwenye kijumba,kumbe hicho kijumba kuna mwanajeshi muasi anayelinda chumba cha ndani anacholala mkuu wake.

Hapo nusura nitolewe uhai,kwakuwa mimi ni special force napambana na yule askari mpaka nikafanikiwa kumpiga risasi ya tumbo,Mara mlango wa chumba cha ndani ukafunguliwa nikajificha nyuma ya mlango,sikuamini macho yangu alotoka hakuwa yule ofisa wa waasi,bali binti mmoja mrembo Africast

Nilichomoka speed mlangoni na kumdaka yule binti na kumgeuza yule binti ngao yangu,kwa kuwa mlango ulikuwa wazi,sikuona Dalili ya uwepo wa mtu mwengine mule ndani,nilianza kumkokota kuingia naye ndani kwa taadhari kubwa.mda nilioridhika kuwa niko salama mule ndani,Mwamba alitokea ukutani na kuniamuru ninyoshe mikono juu na nisigeuke,kumbuka muda huo yule Africast alikuwa kitandani akihema kutokana na kubali niloyomdibiti nayo wakati najilinda.

Kilichoniokoa ni baada ya kuambiwa kila nilichonacho nitoe niweke chini na nivisogeze umbali alokuwa yule Africast na nitulie.

Mwanamke alimwambia yule jamaa ambaye hata mda huo sijui anafananaje zaidi ya kuisikia Sauti yake kuwa huyu jamaa nyaraka zake zinaonesha ni mtanzania..itaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom