Mwl. Nyerere (Mjamaa) na Lowassa (Bepari) walitofautiana kifikra ila kisera juu ya Elimu walikuwa Sawa, UPE na Shule za Kata zinawakutanisha

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF

Ukisikia mchawi mpe sifa zake. Hili la Nyerere na Lowassa ni watu walioona mbali, kama si Nyerere kuanzisha UPE Taifa hili lilikuwa lizalishe wajinga wengi kwani idadi ya watu ilizidi kuoongezeka sana wakati ujenzi wa shule za primary zikiwa kidogo sana kukabiliana na idadi ya watu.

Nyerere kuchukua darasa la saba walio na weledi kidogo kufundisha wengine angalau wawafikie kiwango chao ili ilikuwa ni kufuta ujinga, lakini kwa sasa shule zimeboresha karibu kila kijiji kina shule yake.

Lowassa yeye kwa njia ile ile ya Nyerere alisisitiza elimu bure kwa wote kuanzia form one hadi form 4 mpaka sasa sera hiyo ndiyo inatumika kwa sasa na CCM. Lowassa alianzisha shule za kata akabezwa sana; sasa hivi shule hizo zimeanza kutoa Division One na zinafanya vizuri.

Siku hizi wanafunzi wa secondary uwezi kuwaona wakiaangaika kwenye mabasi, kila kata imejitahidi kuchagua wanafunzi wa eneo lao ambao ni day na wanatembea kwa miguu hadi shuleni kwao.

Hawa watu ni wakuheshimu sana kwa kuwa watupa mwanga.
 
Back
Top Bottom