Jamani, nahisi sifa moja kubwa ya kuwa mwanasiasa Tanzania ni uwezo uliopitiliza wa kuwa mnafiki. Sishangai serikali ikimgeuka Mengi. Ila katiba si inaruhusu mtu kutoa maoni yake na kama inaonekana kuna waliokosewa wampeleke mahakamani. Serikali kuwatetea hawa wafanyabiashara ambao wengi tunajua wanatudhulumu, ndio watakuwa wamechemsha
Kitu gani kizuri hapo?. Kwani wewe HUKUFIKIRI KUWA HAO WATU WANAWEZA KUMSHITAKI MENGI??
duh!
Wabongo zaidi ya uwajuavyo!
Mshikaji fikiria nje ya BOX. Aliyeibiwa nguo ni wananchi wa Tanzania. hao wananchi wanakuwa represented na POLISI (au kwa upana SERIKALI).
Sio kazi ya mwananchi kumfungulia mwananchi mwingine kosa la JINAI. Ni Polisi au ofisi ya DPP ndo ina mamlaka hayo.
Mengi hana mamlaka ya kuwapeleka mahakamani hao mafisadi kwa CRIMINAL CASE.
Jamani muwe mnauliza kwanza!
FP,
Sina hakika kama umejaribu kuelewa nilichomaanisha kwenye post yangu. Na pia sikuona sababu kwa nini usiniulieze (kama hukunielewa) badala ya kuamua kutoa conclusion yenye kuonesha dharau kwa maoni yangu ambayo hayakuhusu wewe na si lazima uyakubali.
Kwa kuwa tumekuwa tukisema kuwa tunahitaji siku moja hili suala lifike mahakamani, na Mengi mwenyewe alisema hivyo kwamba kama wanaona wameonewa waende mahakamani, huoni kuwa kwa maelezo hayo ya Waziri Simba jamaa wakienda mahakamni tutaipata ile fursa tuliyokuwa tunaitafuta siku nyingi? Kama huoni hiyo basi eleza jinsi unavyoona wewe na siyo kujaribu kushusha hadhi ya wenzio kwa kuwapandia mgongoni!
Hii approac ya hawa watuhumia kwenda mahakamani sijui inatoka wapi, kama kweli ni wezi wataenda mahakamani??
Naomba mtu anisaidie hivi mwananchi wa kawaida anawezi kumshtaki fisadi kama ana vithibitisho??
kwa hiyo tuamini kuwa ni jinai kwa mwananchi yeyote mwenye sifa kugombea uraisi??Tatizo Mengi bado anaonekana kama ana ajenda ya kisiasa, sidhani kama Serikali imejiridhisha na utetezi wake alioutoa siku za nyuma kuwa hana nia ya kugombea urais. Hadi hapo watawala watakapo amini kuwa Mengi ni Raia mwema, hata afanye jambo jema kiasi gani bado litapokelewa na wakubwa kuwa linalengo la kisiasa. I hope wananchi wengi wanamuelewa anachokipigania.
"Simba alisema Mengi hana mamlaka hayo ya kutaja watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi."
I need to be educated. Hivi zile kura za siri kwa ajili ya kuwataja watu tunaowashuku katika jamii kua ni wauaji wa maalbino, siyo kwamba tunawashutumu? I mean, if we are allowed to 'make' allegations in secret, why souldn't we be allowed to do that in public if I am not afraid??
kwa hiyo tuamini kuwa ni jinai kwa mwananchi yeyote mwenye sifa kugombea uraisi??
uhuni kweli huu
Ninapongeza kauli za serikali kwani watanzania wote tuna haki sawa na hakuna wa kumuhukumu mwengine pasi na mamlaka halali yaani mahakama. Kama Mengi ana ushahidi wa madai yake na ana vielelezo kwanini hakuviwasilisha katika mamlaka husika ili anaowatuhumu wachukuliwe hatua zipasazo? Hivi leo hii kila mtu anayemtuhumu mwenzie atinge maelezo amchafue kwa nia ya aliyechafuliwa aende mahakamani? Hakuna mantiki hata kidogo, watu wote wafuate sheria na utaratibu uliopo na si kutumia nafasi maalum kupindisha mambo.
Endapo serikali ingekaa kimya maana yake ina kubaliana na uendeshaji wa nchi bila ya kuzingatia utawala bora.
Serikali haipo kwa ajili ya wanyonge tu bali hata akina Mengi na Rostam. Ni vema basi ni lazima ikemee yale yote mabaya ikiwa ni pamoja na kauli za uchochezi, kuchukua sheria mikononi, ufisadi nk.
Serikali yetu iko imara wakati wote na iendelee kufanya kazi kwa faida ya wananchi wote bila ya kuwaonea aibu watu wachache kama Mengi wanaotaka kutimiza matakwa yao binafsi kwa mgongo wa mafisadi nk.
Tuziachie mamlaka husika zifanye kazi ya kutoa hukumu na si vinginevyo.
Kusema mtu ni fisadi kwa vitu ambavyo viko wazi sioni kama nitatizo. Kwani Mengi si mjinga wakutoka kichwa kichwa kwenda kwenye vyombo vya habari. Anajua kwani si mliona wakati anashitakiwa na Manji! Je manji aliendelea na kesi? Si alikacha kesi ikatupwa? Wakati mzee wa watu anaudhulia mahakamani kila siku.
Mbona hizi sheria zitumike kwa mengi je wakati wana mtandao wanajipamba kwa kuwachafua wenzao Salim mwarabu si mtanzania, Sumaye mwizi, Kikwete safi na Lowassa wake je mbona hamkusema? Sasa hivi sheria zifuate mkondo siyo?
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo maadili yalishaondolewa na hao hao ambao leo hii wamegeukwa walisahau nao kuwa wana uvundo. Alivyofanya ni sawa kama anatishwa asiseme? Kama akiona watu wanaiba na hakuna linalofanyika asiseme eti kwakuwa kuna sheria? Kwanini sheria ziliwekwa? Ili zifunjwa otherwise hakukuwa na haja ya kuwa nazo.
Sirikali makini haiachi kushughulikia ktk style iijuayo yenyewe aili muradi truth ina onekana, sidhani mama Sophy amekosea, maana kuikubali njia ya Mengi ni ku givein cheaply kwa sirikali kwa bwana Mengi na ndicho ambacho pengine alikitarajia, mimi naamini tayari sirikali iko kazini juu ya hao mapapa aliowataja Mengi, na wengine wako mahakamani tayari kabla Mengi kutoka na single yake.
Mama Simba yuko sahihi, acha dola ifanye kazi yake kama dola na kuweka miongozo kwa jamii ambamo ndugu Mengi anatokea, Mungu ibariki Tanzania, Hongera mama Simba kwa Job well done- tuachie home yetu ya Mengi vs Mapapa
Hebu tujikumbushe kidogo hii makala ya zamani kidogo ili tumfahamu huyu Manyerere na hapo itakuwa rahisi kumjadili:-
Huyu Manyerere anasema mengi amekuwa mahakama!!! Je naye amekuwa amekuwa Dr. wa vichaa kusema kuwa huyu mzee kachanganyikiwa?