Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mkuu,
Mimi ninakuunga mkono 100% katika maoni yako hapo juu.
Ni jambo la kusikitisha kwa baadhi ya JF members kuona kuwa hii forum inapigania nchi yetu itawalie kwa kufuata misingi ya haki na utawala bora. Tunailalamikia serikali iliyoko madarakani kwa maovu na mabaya inayoyafanya na mengi kwa kuona ni kutofuatwa kwa utawala bora. Leo hii tunaacha katika kusimamia misingi thabiti ya kuifanya nchi hii iwe ni mahali pazuri kwa kila mwanajamii, tuaanza kuwa bias na kuonesha kuwa kelele zetu zote hazina malengo maalum zaidi ya kelele za chura ambazo hazimzuii mtu kuchota maji.
Leo kama unapata nafasi ya kurejea postings za baadhi ya wachangiaji humu katika threads tofauti lakini topics zinayofanana, utaona hakuna consistency, wachangiaji wanaangalia personalities badala ya issues.
Mengi kama anao ushahidi au vielelezo alipashwa kuviwasiliasha katika mamlaka husika na si vinginevyo, sasa inaoneka kuwa amefanya hivyo kwa maslahi binafsi na wala si ya watanzania kwani wote alowataja ni wafanyabiashara wakubwa na wengine ni mahasimu wake wa siku nyingi.

Ndugu hii sera na maoni yako yataweza tukifanilkiwa hapa tulipo. Wewe jiulize kagoda ipo wapi? Meremeta je?

Acha mambo haya, we are tired. Huu utawala bora umetushinda na wewe ndo unaupalilia. Dr. Slaa amewaambia yeye ndo anamiliki nyaraka za siri, nani mwenye moral support kumkamata? we are tired. Kama wewe unafaidika na utawala bora ni wewe na jitahidi katika hilo, mimi sitaki utawala bora.

AMANI WAKATI HAKUNA UTULIVU?
 
What I can't understand is why skin sensitivity only occurs when there is a big issue like this. So this means people should be afraid to speak out against criminals or other kind of law breakers if they are not black. Those people who first thought that naming this people are racist are theselves racists. kwa nini walivyo tajwa wasiseme ni watanzania? Kwa nini wame notice tofauti yao ya rangi haraka? If they said it then they also thought it. Tusiangalia race, gender, religion, height, wealth or anything else. Tukianza kuchambua mambo madogo mwisho tutaanza kusema oh huyu ni mfupi basi mnambagua kwa kumtaja au oh huyu ni mnene mnambagua. Why are people so easy to see the descriptions of peoples appearance when it comes to issues like this? I'm sure kuna mafisadi wengine lakini kama Mengi hana ushahidi nao afanyaje? Awataje tu na weusi ili mradi? WOTE WALIO TAJWA NI WANAUME KWA NINI WASISIME KABAGGUA WANAUME KWA SABABU LIST YAKE HAINA MWANAMKE HATA MMOJA? YEYE KASEMA ANA USHAHIDI NA HAO BASI MUAMBIENI ATOE USHAHIDI WAKE. MAANA ANGETAJA TU WATU KUTIMIZA DEMOGRAPHY YA NCHI MKAMUOMBA USHAHIDI AKASHINDWA KUTOA MGESEMAJE? I'M NOT SAYING ALIYO WATAJA WAMESHA HUKUMIWA LAKINI HE SAYS HE HAS EVIDENCE AT LEAST HEAR HIM OUT. KAMA KAWAONEA SI ITAKUJA KUONEKANA?
Kataja kama nani?? au kwa kuwa ana media house anayoimiliki kwa masilahi yake??

Rostam wala manji hawana tatizo lolote.. Tatizo ni mfumo wanaoutumia na kuwatumia wao ambao Mengi anaujua na kwa UNAFIKI WAKE HATUELEZI UKWELIII KUWA HAPA MCHAWI NI CCM NA VIONGOZI WAKE..

MEDIA YAKE KWA SASA KILA UOZO WA SERIKALI ILIYOPITA WANATUELEKEZA CHANZO NI BEN MKAPA!!!!! KWA NN UOZO WA SASA HAWATUAMBII JAKAYA KIKWETE NDO CHANZO KAMA KIONGOZI MKUUU?????

MENGI UNAFIKIII HAUTAMSAIDIAAAA WALA HUO SIO UZALENDO KWA TAIFA LAKEE....
 
Sophia Simba alipokuwa akimponda Mengi leo asubuhi ktk mahojiano na Marin Hassan alionyesha kusahau alichokariri.

Nilishangaa sana kumuona Mheshimiwa anaongea kama vile yuko katika mipasho ya Kitchen Party!

Sasa tunajiuliza, JK anatumia kigezo gani kuwateua hawa Mawaziri wetu??? Tena waziri wa Utawala bora anayemhukumu Mengi kuwa "kawahukumu mafisadi" wakati yeye hapohapo anamhukumu Mengi! Mh. Simba kuwa waziri wa Utawala bora ndio anakuwa UNIVERSAL BAROMETER hapa TZ.

I get my fingers CROSSED!
 
Hivi ni nani anae kumbuka lini huyu chizi Mkuchika alisema neno la maana? Kesi kati ya Mengi na wafanya biashara wenzie inaingiliwa na serikali ili iweje? Rostam kama anaona mengi kamsema ovyo basi ana kila haki ya kufile lawsuit against Mengi.

Sasa hawa kina Simba sijui kuku wanalopokwa nini? I don't get kabisa kama hawa watu wanajua jurisprudence ya kazi yao.
 
Kataja kama nani?? au kwa kuwa ana media house anayoimiliki kwa masilahi yake??

Sasa ulitaka amiliki mwa maslahi ya nani?

Rostam wala manji hawana tatizo lolote..

Yaani, unaweza kusema hilo bila kupepesa macho? Yaani Rostam wala Manji hawana "TATIZO LOLOTE"?

Tatizo ni mfumo wanaoutumia na kuwatumia wao ambao Mengi anaujua na kwa UNAFIKI WAKE HATUELEZI UKWELIII KUWA HAPA MCHAWI NI CCM NA VIONGOZI WAKE..

Miongoni mwa viongozi wa CCM ni Rostam! halafu hili la kulaumu mfumo ni kujaribu kukwepesha kuwalaumu watu.. kwanini tusimlaumu Mungu tu!?

MEDIA YAKE KWA SASA KILA UOZO WA SERIKALI ILIYOPITA WANATUELEKEZA CHANZO NI BEN MKAPA!!!!! KWA NN UOZO WA SASA HAWATUAMBII JAKAYA KIKWETE NDO CHANZO KAMA KIONGOZI MKUUU?????

Kwani lazima uozo wa sasa chanzo chake kiwe Rais?

MENGI UNAFIKIII HAUTAMSAIDIAAAA WALA HUO SIO UZALENDO KWA TAIFA LAKEE....

Ni uzalendo kusema Rostam na Manji hawana "tatizo lolote"? Mzalendo ni nani basi?
 
Tuziachie mamlaka husika zifanye kazi ya kutoa hukumu na si vinginevyo.

Inaonekana kwako mamlaka "husika" za kutoa hukumu ni pamoja na mawaziri! Ungenipa moyo kuwa unajaribu kuwa fair kama ungepinga kitendo cha Mkuchika na Simba kumhukumu Mengi bila kumfikisha mahakamani au kumpa nafasi ya kujitetea! Hukufanya hivyo na hivyo kuthibitisha kuwa una maslahi zaidi ya kutaka haki itendeke kwa kila mhusika.

Mkuu mwanakijiji nadhani ndugu yetu anaitaji kuelimishwa...siasa aliyoiacha bongo those days sio inayoendelea hivi sasa.am sorry sijui wakati anaondoka nchini hata EPA aliisikia..well n Gud is a goodbr..ila nafikiri kama tungekuwa tunawaachia mamlaka hata
alipokuwa ATCL alikemea watu walioteuliwa na RAIS...Mbona akuiachia mamlaka kuhukumu makosa yanayotendeka........tu mmwombe mungu sana atupe ufahamu na busara hapo ndipo utakapoenda kujua jambo jema na baya......\
kila la kheri...mi kwa ushauri kama unaweza kutusaidia ungewasiliana na bibi SOPHIA LION THEN UWAAMBIE WATANGULIE MAHAKAMANA NA MKUCHIKA WAKE SISI TUTAKUWA NYUMA YAO...EMBU ANGALIENI WAZIRI MWENYE AKILI TIMAMU WA HABARI ANASEMA TUTAFUTA MIKANDA YA USHAHIDI KAMA KWELI ALISEMA...KWA NINI USIMUULIZE MKEO NYUMBANI ,KWA NIN ILIKUWA SIRI NA JANA USIKU WAMERUDIA NA KUKUSAIDIA UPATE MKANDA KAMILI ANGALIA KESHO USIKU TENA HOTUBA YA MENGI ..UUREKODI VYEMA....
HAYA MAPEPO SIJUI YAMETOKEA WAPI SERIKALINI.....TUKISEMA SERIKALI YA KUOMBEA MMMHHH...ANGALIENI VINAVYOWAPANDA MATOKEO YAKE WANAKIMBILIA TANGA ....NANI AMEKWAMBIA TANGA WANAPONYA VICHAA??

Ndugu yangu PDidy,

Ahsante kwa maelezo yako japokuwa mengi haupo sahihi.

Lakini kama utakuwa umesoma maelezo yangu vizuri ni kwamba watanzania tunapigania kujenga nchi yenye misingi bora ya kidemokrasia na utawala bora. Sheria na taratibu zinazoweza kutuongoza zipo ila wengi wetu hatuamini katika hilo. Mimi sina kawaida ya kufumbia macho mambo yanafanywa nje ya utaratibu always nitasema hili hata kama wewe ni rafiki yangu mpenzi. Kinyume cha hapo nitakuwa sikutendei haki na ni mnafiki. Iko haja kwanza sisi wananchi tujiangalie ni kwa kiwango gani tuko tayari kuheshimu utawala wa sheria? endapo leo tunashabikia uvunjifu wa amani, je tunajiweka wapi katika safari ndefu ya kuifanya Tanzania ni mahali bora kwa jamii?
Endapo, unamtuhumu mtu amekwiba, wajibu wako ni kumfikisha katika vyombo vya sheria na wala si kuanza kumpiga...huo ndiyo utawala bora unaozingatia sheria. Kama Mengi aliona ana ushahidi wa kutosha hakuhitaji kuitisha press conference awadhalilishe watu ilihali akijua kuwa kwa kufanya hivyo si sahihi. Kama utakumbuka kuwa miaka kadhaa iliyopita Rev. Mtikila aliwaita wahindi magabacholi na kuwataka wananchi waende kuvamia maduka na kuiba, Mtikila alikamatwa pamoja na mambo mengine alishtakiwa kwa kosa la kuwaita wahindi wezi.
Muhimu katika thread hii ninachotaka kuwaasa watanzania kuwa mabadiliko ya kweli ya Tanzania si ya uongozi wa nchi bali ni kubadilika kwa mawazo ya watanzania waweze kufuata utawala wa sheria, vinginevyo mtayumbishwa kama anavyofanya Mengi, DECI, nk
Watanzania ni lazima wafike mahali kila mmoja aweze kuwa independent katika kufanya judgment kwa kuzingatia sheria halali za nchi. Hii itasaidia kutoa mwanga mkubwa wa kuleta maendeleo na mabadilko ya kisiasa na kiuchumi. Tutumie muda mwingi kuwa-impact watanzania namna nzuri ya kufanya maamuzi yakiwemo ya kupiga kura, kuanzisha na kuendesha communities zitakazokuwa na nguvu katika maeneo wanayoishi. si vyema tukapandikiza mbegu za chuki ambazo moto wake ukilipuka hakuna atakayeweza kuuzima na makovu yake kufutika. Jazba, Chuki, Fitna nk havitaisadia kuipeleka mbele Tanzania.
 
Naona mmesahau kuwa inabidi atetetee zile hela alizokuwa anatoa(honga) kwenye uchaguzi wa UWT.

Nyie mlifikiri zilitoka wapi?

JK amtoe huyu mama???!!!! hahahaaaaaa labda urais wake hauna ubia!
 
Maneno yako ni mazuri na yanaweza kuvutia lakini nyuma yake yanaficha ukweli ambao unataka kuusema. Tatizo lako ni Mengi kusema alichosema. Hujali alichosema Mkuchika au Sofia Simba ambao nao wamefanya kile kile ambacho Mengi anadaiwa kufanya.

Sasa kama kweli unataka watu wafuate sheria inabidi ulilie serikali na watumishi wake wawe wa kwanza kuonesha hiyo dhana ya utawala bora. Kama Mengi hawezi kumtuhumu mtu bila kuchukua hatua za kumfikisha kwenye vyombo vya haki inakuwaje kina Mkuchika wanaweza kumtuhumu mtu bila kufuata taratibu hiyo hiyo?

Hivi kweli unafikiri hata leo Mengi akikamatwa na kufikishwa mahakamani atatendewa haki wakati Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo (mwenye dhamana ya vyombo vya habari) keshatoa hukumu? Unafikiri anaweza kutendewa haki wakati waziri wa Utawala Bora ameshatoa hukumu yake?

Unapotaka utawala wa sheria huchagui unasema Serikali ifuate sheria na wananchi wafuate sheria. Hapo uko neutral. Hadi sasa hujasema lolote kama Rostam alifanya vibaya kuzungumza na waandishi wa habari na kutoa tuhuma dhidi ya "wafanyabiashara" fulani?

Tatizo ninaloliona siyo kwamba mtu hajafuata sheria, bali tatizo mtu huyo ambaye unaona hajafuata sheria ni Mengi! Tell me I'm wrong.
 
Nchi imeuzwa , ingekuwa China........
Lakini subiri baada ya miaka mitano watajibu tu!
ndio maana nyaraka za serikali ni siri, wakati sisi tumeuzwa na hatujui, five years to come tutaambiwa ah mbona sehemu hiyo iliwekwa rehani etc etc
 
Hapa ndo pa kujua nani yuko upande upi?, badala wafatilie tuhuma wao wana dili na mtoa tuhuma? Serikali ndo itakuwa imechemsha big time, kujiingiza kuwatetea mafisadi, Ila wana sahau kwamba kuna nguvu kubwa ya umma nyuma ya wanao pambana na mafisadi! They want to see it, haya jaribuni kumgusa mzalendo Mengi!

My friend Rwabugiri, simple minds discuss people, we are still missing political leaders with great minds who will eventually discuss ideas and issues raised.
 
Jamani JF mnakosea (sio wote).

Mengi kataja mafisadi kama hapa tunavyo wataja. What is the problem?

Sofia Simba kila mtu anamuelewa; anatetea hela alizokuwa anahonga wakati wa uchaguzi UWT. Hata wewe ungetetea tu.

Niambieni lini Mkuchika au Sofia Simba waliongea kitu cha maana?

Kama Mengi kahukumu na yeye mbona anamhukumu Mengi?

JK, safisha nyumba. Kama ni fadhila ndugu yangu umeshalipa. Miaka minne inatosha kwa kulipa fadhila.

FP
 
huyo mama ni mbabaishaji,
hajui kuongea na huw anakurupuka sana
 
Ama kweli taifa hili limewekwa mfukoni na mafisadi. Kama Mengi alikosea kuwatuhumu wale watu ni wajibu wao wenyewe kukanusha au kumshtaki Mengi Mahakamani.
Ajabu ni pale Waziri wa serikali iliyohujumiwa na kuibiwa ndiye anasimama mbele ya kamera na kuwatetea wanaotuhumiwa kuiibia serikali hiyo hiyo anayoitumikia.
HUU NI WEHU WA KIWANGO CHA JUU KABISA.
 
Pamoja na kuchemsha, ameongea kitu kimoja kizuri sana, kwamba hawa watu wanaweza kumshitaki Mengi. Wengi wetu tumesubiri hilo ila naona halitokei. Kwa nini hawaendi kumshitaki Mengi? Ila kuonesha jinsi JK na serikali yake yote walivyotekwa na Mafisadi, magazeti yameripoti kuwa hata Mkuchika anataka kumjibu Mengi. Kwani kwenye hili suala la mafisadi papa serikali inahusikaje?
 
ndio maana nasema,mengi anafikiri kikwete mwenzake ...kumbe atamtosa...kila siku anajifanya kumpigia kikwete debe..sasa sofia simba huyo confidant na mwenza wa kikwete amemtosa......kikwete ni mnafiki....anamchekea mengi jono la pembe!!!
umenena kaka....

mengi ajidanganya tuu kwa kikwete..bora mkapa alimtosa live kumsaidia kwani mengia anapenda sana sifaaa..
 
Kwa nini Serikali inawajibia mafisadi???kwani wao wenyewe hawawezi kujibu??au hawazioni mahakama?kweli bora utawala .......SS ni bogus wa karne kwani hamumjui??ila watavuna walichopanda...time will tell.
 
Pamoja na kuchemsha, ameongea kitu kimoja kizuri sana, kwamba hawa watu wanaweza kumshitaki Mengi. Wengi wetu tumesubiri hilo ila naona halitokei. Kwa nini hawaendi kumshitaki Mengi? Ila kuonesha jinsi JK na serikali yake yote walivyotekwa na Mafisadi, magazeti yameripoti kuwa hata Mkuchika anataka kumjibu Mengi. Kwani kwenye hili suala la mafisadi papa serikali inahusikaje?

Kitu gani kizuri hapo?. Kwani wewe HUKUFIKIRI KUWA HAO WATU WANAWEZA KUMSHITAKI MENGI??

duh!

Wabongo zaidi ya uwajuavyo!
 
Back
Top Bottom