Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Well done Mwanafalsafa1. It is CCM that has been colluding with Rostam Aziz, Yusufu Manji, Jeetu Patel and Somaiya to milk the wananchi. CCM campaign funds come directly from money stolen through these named fisadis.

Kikulacho kii nguoni mwako. It is impossible to tackle corruption in Tanzania while CCM is still in power. The necessary first step is to consign the backers of these fisadis, that is CCM, to the opposition benches.
 
Tanzanians must rally behind anti-corruption crusaders to save the country



EDITOR
DAR ES SALAAM

THE war against corruption was taken a step further last week when IPP Executive Chairman Reginald Mengi publicly named five prominent personalities he alleged were the main ’sharks of corruption’ in the country.

Members of Parliament, human rights activists, and ordinary people rallied behind Mengi and saluted him for the audacity to name the high-profile corrupt elements.

We all know how the corruption cankerworm is tearing our country’s social fabric apart. We must agree that the situation has reached grave proportions and failure to put a stop to this vice will ultimately cause irreparable damage to any hopes of real economic progress this country may have ever had.

The situation is now so bad that if the current government continues to do nothing about bringing to justice the many corrupt elements in our midst, especially the more high-profile ones, it (the government) is in danger of being dismissed as a farce, both within and outside the country.

Suffice to say that the brazen thieving of public monies going on at practically all levels of government now even qualifies for a national state of emergency to be declared.
It is for this reason that we extend our strong support to Mengi and other like-minded Tanzanians who are in the forefront in the war against corruption.

However, it is surprising that there has emerged a group of people who use the media to try to defend these corruption sharks whose scandals have the potential of derailing the government.

It is high time the society in its entirety joined hands with all those spearheading the national fight against corruption so as to free our nation from the shackles of this vice, which is increasingly becoming an endemic.

The government, through its law enforcement organs, knows all those who have participated in various scams, despite the indifferent attitude it is maintaining.

It is instructive to note that in truly-developed societies where the rule of law is properly practiced, no violator of laws as those designed to prevent corruption is allowed to get away with it without any form of punishment or accountability.

Sadly, this is not quite so in our country. And it is a reality that can only be sending the wrong kind of signals to the outside world that, here in Tanzania, bribery and corruption are a way of life and we are not serious about the rule of law.

The national economy has lost billions upon billions of shillings through such endemic corruption.

And as a result - against the logic of its rich endowment in natural resources and its high developmental potential, this country has remained one of the most underdeveloped countries in the world, with three quarters of its population afflicted by grinding poverty and living on less than a dollar a day.

As a result of various policy failures that are largely attributable to corruption in the process of implementation, the majority of Tanzanians still to this day have little or no access to electricity or water - or even two good meals a day.

This has become a nation where a minority of individuals with direct access to its abundant natural resources appear to have commandeered its collective wealth and are now holding the rest of the citizenry to ransom.

The greatest hurdle to this country’s development remains to be corruption, and unless and until this cancerous disease gets the right cure, the majority of Tanzanians, and ultimately the nation as a whole - will continue to languish in poverty in the midst of plenty.
Time to act is now. Let’s all rally behind the true crusaders of the war against corruption.
 
This article is from THISDAY. The writer is tring to rally Tanzanians against mafisadi in my understanding.
 
Thats why we are here bro. If we don't love our country ourselves no one will do it for us, especially the fisadis.
 
Hapa tulipo tumefikia njia panda ni lazima tuwe na umoja wa hali ya juu ili kuwashinda mafisadi, na kama tukishindwa kufanya hivyo na kurudi yena madarakani basi tutajuta kwa miaka mingi ijayo na si ajabu nchi ikaingia katika matatizo makubwa zaidi kuliko ambayo tumekwisha yaona.
 
Kikulacho kii nguoni mwako. It is impossible to tackle corruption in Tanzania while CCM is still in power. The necessary first step is to consign the backers of these fisadis, that is CCM, to the opposition benches.

Absolutely. The only alternative we have right now is to send them packing.
 
Your analyis is simply a posture of where Tanzania stand. From the veil of ignorance the country is still unaware of what you are trying to say. I believe you have spoken out in un indiscibable attitude of positive mind and in a very historical and visionary way.
Tanzania is a country endowed with a strong respect of people regardless of their colour, religion race nd what ever a difference is . It is being absolutely silly not to tell the trueth because of being sensitive to skin color. Can't it be looked in the other way that Manji and Rostam Aziz arestaling our money simply because w are blak?? and i think Rostam and Manji hatre us. this is why they are stealing our money. they are also jelousy of our wealth. they are gready people who never get satsfied. They have stolen enough and now is the time to say stop and they should be rsposible!!!
jmbapani@yahoo.com
 
What I can't understand is why skin sensitivity only occurs when there is a big issue like this. So this means people should be afraid to speak out against criminals or other kind of law breakers if they are not black. Those people who first thought that naming this people are racist are theselves racists. kwa nini walivyo tajwa wasiseme ni watanzania? Kwa nini wame notice tofauti yao ya rangi haraka? If they said it then they also thought it. Tusiangalia race, gender, religion, height, wealth or anything else. Tukianza kuchambua mambo madogo mwisho tutaanza kusema oh huyu ni mfupi basi mnambagua kwa kumtaja au oh huyu ni mnene mnambagua. Why are people so easy to see the descriptions of peoples appearance when it comes to issues like this? I'm sure kuna mafisadi wengine lakini kama Mengi hana ushahidi nao afanyaje? Awataje tu na weusi ili mradi? WOTE WALIO TAJWA NI WANAUME KWA NINI WASISIME KABAGGUA WANAUME KWA SABABU LIST YAKE HAINA MWANAMKE HATA MMOJA? YEYE KASEMA ANA USHAHIDI NA HAO BASI MUAMBIENI ATOE USHAHIDI WAKE. MAANA ANGETAJA TU WATU KUTIMIZA DEMOGRAPHY YA NCHI MKAMUOMBA USHAHIDI AKASHINDWA KUTOA MGESEMAJE? I'M NOT SAYING ALIYO WATAJA WAMESHA HUKUMIWA LAKINI HE SAYS HE HAS EVIDENCE AT LEAST HEAR HIM OUT. KAMA KAWAONEA SI ITAKUJA KUONEKANA?
 
What I can't understand is why skin sensitivity only occurs when there is a big issue like this. So this means people should be afraid to speak out against criminals or other kind of law breakers if they are not black. Those people who first thought that naming this people are racist are theselves racists. kwa nini walivyo tajwa wasiseme ni watanzania? Kwa nini wame notice tofauti yao ya rangi haraka? If they said it then they also thought it. Tusiangalia race, gender, religion, height, wealth or anything else. Tukianza kuchambua mambo madogo mwisho tutaanza kusema oh huyu ni dark black kwanini atajwe na oh huyu ni light black kwa nini atajwe. Lets not look at unimportant issues. Sheria haina macho haiangalii mtu ukoje.

It beats me!
Rangi or no rangi... mwizi ni mwizi tu! Wahindi ni maji yaendayo kimya kimya lakini kina chake kinaua kwa jinsi kilivyo kirefu.WATAJWE TU hata kama itatafsiriwa ni ubaguzi.
 
It beats me!
Rangi or no rangi... mwizi ni mwizi tu! Wahindi ni maji yaendayo kimya kimya lakini kina chake kinaua kwa jinsi kilivyo kirefu.WATAJWE TU hata kama itatafsiriwa ni ubaguzi.

Kutumia rangi, dini au kabila fulani kubagua jamii fulani sio sifa ya "Great Thinker". Kuna wezi wengi ambao ni waafrika wenzetu.

Mengi alichemsha, huwezi kutoa hukumu kwa watu mbaya zaidi wengine wakiwa na kesi mahakamani zinaendelea! Kungekuwa na "rule of law" Mengi angekuwa tayari na kesi ya kujibu...lakini kwa sababu nchi hii inaendeshwa kisiasa basi Mengi na wengine kati ya aliowataja hawana wa kuwashika.
 
SOPHIA SIMBA MKUCHIKA MNAMUABISHA RAIS;SHAME ON YOU

ACHENI TAMAA ZISIZO NA MSINGI KAMA MNANUNULIWA HATA NA WAHINDI ;WATANZANIA WAMEAMUA KUAMKA WENYEWE HAWATAKI KUUZWA TENA....KAMA MMEKASIRIKA MKAFIE MBELE ;NA WEWE MKUCHIKA KAMA HUNA KITU CHA KUFANYA NA MKEO JARIBU UONE UTAKACHOPANDA ;KAMA UJAWA DECI YA PI,....ACHA KUTISHIA WATU KAMA MTOTO MDOGO...HII MIZEE ILISHASTAAFU IKASAHAULIKA KABISA KWENYE ULIMWENGU IMERUDISHWA BAADA YA KUPEWA FADHILA NA RAIS NA OLE WAKO KAMA USINGEKUWA MWANAJESHI UNGEFIA TANGA.....FANYA KAZI ZAKO INAVYOPASWA ....ACHA KUTISHIA WATANZANIA...COCROACH....

MODE TUNAOMBA HII IWE FUNDISHO IACHE IJITEGEMEE TUMECHOKA KUTISHANA KAMA MENDE KILA SIKU....BUNGENI WANATUTISHA HUYU WAZIRI UCHWARA MKUCHIKA ATUTISHE ...WA MAADILI NA STAREHE ZA ZIN..... ATUTISHE NAE.SHAME




Mfanyabiashara maarufu nchini, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi, serikali inamwona amefanya makosa kutangaza majina ya anaodai kuwa ni mafisadi papa.

* Waziri Sophia Simba asema Mengi kachemsha
*Mkuchika naye asema wanamchunguza


Ramadhan Semtawa na Leon Bahati


MAWAZIRI wawili, Sophia Simba na George Mkuchika jana walimshambulia mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi ambaye wiki iliyopita alitangaza majina ya wafanyabiashara watano wenye asili ya Kiasia, akisema ni mafisadi waliokubuhu.


Simba, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Mkuchika, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo walisema mfanyabiashara huyo wa jijini Dar es salaam "amechemsha".


Mengi alitangaza majina ya wafanyabiashara hao Alhamisi iliyopita akisema ni kati ya watu wasiozidi 10 ambao alidai wanaifilisi nchi na kutaka wadhibitiwe mapema kabla hawajaitingisha na kuiyumbisha nchi.


Hata hivyo, Mengi, ambaye alidai katika taarifa yake kuwa juhudi za Rais Jakaya Kikwete zinakwamishwa na watu hao, hakueleza jinsi watano hao wanavyoitafuna nchi zaidi ya kusema kuwa wanatorosha fedha wanazozipata 'kifisadi'.


Jana, kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam mawaziri hao wawili walitoa kauli za kumshambulia mwenyekiti huyo mtendaji wa makampuni ya IPP, kauli ambazo zinadokeza mtazamo wa serikali katika mjadala unaoendelea wa vita dhidi ya ufisadi na vinara wake.


Waziri Simba, ambaye wizara yake pia inawajibika katika vita dhidi ya ufisadi, alisema: "Kakosea... watoto wa mjini wanasema kachemsha."


Simba alitoa msimamo huo jijini Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kufungua semina ya wadau wa vyama vya siasa kuhusu namna ya kuiboresha Sheria ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995.


Simba alisema Mengi hana mamlaka hayo ya kutaja watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.


Kabla ya kujibu swali kuhusu kitendo cha Mengi, ambaye anamiliki televisheni ya ITV na kituo cha redio cha Radio One Stereo, kutaja majina ya watu hao aliowaita mafisadi papa, Simba alihoji: " Hapa kuna mtu wa ITV?."


Baadaye alisema: "Sikilizeni, kwanza kitendo alichokifanya Mengi si sahihi, kakosea hawezi kuhukumu watu, mamlaka hayo anatoa wapi?"


Simba, huku akionekana kama mtu ambaye alikuwa akitafuta jukwaa kuzungumzia suala hilo, alisema Mengi amekosea kwa kuwa baadhi ya watu aliowataja wana kesi mahakamani.


"Anahukumu watu," alisema. "Kuna mtu kama Jeetu (Patel) ana kesi mahakamani (EPA), sasa unapokuja kusema ni fisadi wakati mahakama haijathibitisha, unakuwa na maana gani.


"Kwanza kwanini awatuhumu wafanyabiashara wenzake tu, ina maana si ana nia mbaya nao."


Alisema Mengi amechukua uamuzi huo kama vile serikali, wakati serikali ipo siku zote na imekuwa ikifanya kazi zake kwa umakini kwa kufuata misingi ya sheria.


"Serikali ipo na inafanya kazi kwa misingi ya sheria, sasa yeye kukaa na kutangaza watu nasema si sahihi kabisa. Mahakama pekee ndiyo inaweza kumtia mtu hatiani, lakini huwezi kuhukumu watu kama hakuna mamlaka."


Waziri Simba, ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), alisema Mengi hapaswi kutumia vyombo vyake vibaya.


"Asitumie vyombo vyake kufanya atakavyo yeye. Huwezi kukaa katika chombo chako na kuanza kuhukumu watu. Kila mtu akifanya hivyo itakuaje," alihoji.


Akiongea na Mwananchi baada ya kupata taarifa za kauli ya Simba, Mengi alisema: "Namuombea kwa Mwenyezi Mungu na kwa maskini wa Tanzania ili wamsamehe kwa sababu hajui anenalo."


Mengi hakutaka kuzungumza zaidi kuhusu hatua hiyo ya Mama Simba.


Naye Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali itamchukulia hatua za kisheria Mengi iwapo itabainika alikiuka taratibu na kanuni za nchi kwa kutangaza majina ya watu anaowatuhumu kwa ufisadi.


Mkuchika alisema jijini Dar es Salaam jana kwa sasa serikali inafanya uchunguzi juu ya suala hilo na itatumia mikanda ya video pamoja na maelezo ya kimaandishi aliyoyatoa Mengi siku alipokutana na waandishi wa habari.


"Tumekusudia kupata ule mkanda wa video, pia tusome maelezo yake ya kimaandishi... tukigundua kuna mahala ambapo sheria haikuzingatiwa, (Mengi) atachukuliwa hatua," alisema Mkuchika.


Mkuchika alisema serikali imepokea malalamiko mengi kutoka kwa watu wengi, wakishutumu hatua iliyochukuliwa na Mengi, ambaye pia anamiliki viwanda vya vinywaji.


Bila kutaka kuwataja majina, Mkuchika alisema miongoni mwa walalamikaji, wapo walioeleza kuwa vyombo vya habari vya mfanyabiashara huyo havikuwatendea haki watuhumiwa waliotajwa kuwa ni mafisadi wakuu.


Alisema ni kutokana na vyombo hivyo kuwataja majina watuhumiwa bila ya kuwapa fursa ya kujibu madai dhidi yao.


Waziri Mkuchika alipotakiwa kueleza siku ambayo uchunguzi huo utakamilika, alijibu wananchi wanapaswa kuwa watulivu kwa sababu serikali ikimaliza kuchunguza, itawatangazia yale waliyobaini.


Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miezi takribani mitatu kwa Mengi kuingia katika mvutano na serikali baada ya kuvutana mapema mwaka huu na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kutokana na kutangaza kuwa kuna mipango ya kumfilisi na kumuua.


Mengi pia amewahi kujikuta katika malumbano na watendaji wa serikali hasa na waziri wa zamani wa nchi, ofisi ya rais (utawala bora), Wilson Masilingi alipotoa tuhuma kuwa suala la utoaji zabuni ya ununuzi wa hoteli ya Kilimanjaro, hivi sasa inajulikana kama Kilimanjaro Kempiski, kulikuwa na kitu alichokiita "mchezo mchafu".


Suala hilo liliamsha malumbano makali, lakini liliishia hewani.


Katika tuhuma za wiki iliyopita, Mengi aliwahusisha wafanyabiashara hao watano na kashfa za wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development (LLC) na uuzwaji wa jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF).


Mengi, ambaye kituo chake cha televisheni cha ITV kiliwahi kuendesha mchezo mkubwa wa bahati nasibu ya Jackpot Bingo, pia aliitaja Bahati Nasibu kuwa katika tuhuma hizo, pamoja na mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma.
 
Hatuwezi kukaa na miwaziri inayoendekeza njaa hata siku moja;;nyerere uko wapi...............nchi inauzwa na mawaziri babu;wasaidie hata kwa maombi uko uliko wasichomwe moto wa dunia......
 
Ninapongeza kauli za serikali kwani watanzania wote tuna haki sawa na hakuna wa kumuhukumu mwengine pasi na mamlaka halali yaani mahakama. Kama Mengi ana ushahidi wa madai yake na ana vielelezo kwanini hakuviwasilisha katika mamlaka husika ili anaowatuhumu wachukuliwe hatua zipasazo? Hivi leo hii kila mtu anayemtuhumu mwenzie atinge maelezo amchafue kwa nia ya aliyechafuliwa aende mahakamani? Hakuna mantiki hata kidogo, watu wote wafuate sheria na utaratibu uliopo na si kutumia nafasi maalum kupindisha mambo.


Mzee Mwanakijiji
Mzee Mwanakijiji is present!
JF Premium Member Join Date: Fri Mar 2006
Location: Kijijini
Posts: 14,460
Thanks: 8,472
Thanked 12,254 Times in 4,388 Posts
Rep Power: 55

Credits: 14,701,927,586


Re: Serikali yamgeuka Reginald Mengi kwa kauli ya mapapa wa ufisadi

--------------------------------------------------------------------------------

Quote: Pundamilia07
Ninapongeza kauli za serikali kwani watanzania wote tuna haki sawa na hakuna wa kumuhukumu mwengine pasi na mamlaka halali yaani mahakama.



sasa kama hili ni kweli (kitu ambacho unaonekana unakiamini), kuna tofauti gani ya ilichofanya serikali na alichofanya Mengi? Serikali (Mkuchika na Simba) wamemhukumu Mengi kuwa "amechemsha" na kuwa "amevunja sheria" wakati wao siyo mahakama! Kwa maneno mengine wamemuita Mhalifu bila ya kumfikisha mahakamani!

Au kwa vile ni "serikali" basi unaunga mkono kauli yao lakini ya Mengi huiungi mkono kwa sababu japo wote wamefanya kile kile (kutoa tuhuma dhidi ya mtu mwingine) la Mengi limekukera zaidi?


Quote:
Kama Mengi ana ushahidi wa madai yake na ana vielelezo kwanini hakuviwasilisha katika mamlaka husika ili anaowatuhumu wachukuliwe hatua zipasazo?

Swali hilo hilo linaulizwa kwa Simba na Mkuchika, kama wanajua Mengi kachemsha na kuwa kavunja sheria kwanini kuzungumzia hayo kwenye vyombo vya habari badala ya ushahidi walio nao kuupeleka kwenye vyombo husika ili achukuliwe hatua?

Quote:
Hivi leo hii kila mtu anayemtuhumu mwenzie atinge maelezo amchafue kwa nia ya aliyechafuliwa aende mahakamani? Hakuna mantiki hata kidogo, watu wote wafuate sheria na utaratibu uliopo na si kutumia nafasi maalum kupindisha mambo.

Je kanuni hii inamhusu Mengi tu (haimhusu Rostam au serikali maana wote wamewahi kutumia vyombo vya habari kutoa tuhuma nzito bila kwenda mahakamani?

Quote:
Endapo serikali ingekaa kimya maana yake ina kubaliana na uendeshaji wa nchi bila ya kuzingatia utawala bora.

Kwa kusema kwao wamethibitisha kuwa hawazingatii utawala bora!
Quote:
Serikali haipo kwa ajili ya wanyonge tu bali hata akina Mengi na Rostam. Ni vema basi ni lazima ikemee yale yote mabaya ikiwa ni pamoja na kauli za uchochezi, kuchukua sheria mikononi, ufisadi nk.

Inakuwaje kama serikali ndiyo mvunjaji sheria wa kwanza nchini? Nani ataiambia? Au kwako serikali haiwezi kufanya makosa?

Quote:
Serikali yetu iko imara wakati wote na iendelee kufanya kazi kwa faida ya wananchi wote bila ya kuwaonea aibu watu wachache kama Mengi wanaotaka kutimiza matakwa yao binafsi kwa mgongo wa mafisadi nk.

Na kwa wale wanaotaka kutumia migongo ya walalahoi na wapambanao na ufisadi ili kujijengeya himaya yao ya ufisadi na ambao wameiweka serikali mikononi mwao itakuwaje? Mbona siyo Simba wala Mkuchika aliyejitokeza kusema lolote wakati Rostam amezungumza na waandishi wa habari Mei mwaka jana?

Quote:
Tuziachie mamlaka husika zifanye kazi ya kutoa hukumu na si vinginevyo.

Inaonekana kwako mamlaka "husika" za kutoa hukumu ni pamoja na mawaziri! Ungenipa moyo kuwa unajaribu kuwa fair kama ungepinga kitendo cha Mkuchika na Simba kumhukumu Mengi bila kumfikisha mahakamani au kumpa nafasi ya kujitetea! Hukufanya hivyo na hivyo kuthibitisha kuwa una maslahi zaidi ya kutaka haki itendeke kwa kila mhusika.

Well, different strokes for different folks I guess.

HAPA NDIPO NINAPOIESHIMU JF; MKUU PUNDA SOMANYAKATI KAKA YANGU USIINGIE MKENGE KICHWA KICHWA KAMA MTIKILA.....
 
Kutumia rangi, dini au kabila fulani kubagua jamii fulani sio sifa ya "Great Thinker". Kuna wezi wengi ambao ni waafrika wenzetu.

Mengi alichemsha, huwezi kutoa hukumu kwa watu mbaya zaidi wengine wakiwa na kesi mahakamani zinaendelea! Kungekuwa na "rule of law" Mengi angekuwa tayari na kesi ya kujibu...lakini kwa sababu nchi hii inaendeshwa kisiasa basi Mengi na wengine kati ya aliowataja hawana wa kuwashika.

Mkuu,
Mimi ninakuunga mkono 100% katika maoni yako hapo juu.
Ni jambo la kusikitisha kwa baadhi ya JF members kuona kuwa hii forum inapigania nchi yetu itawalie kwa kufuata misingi ya haki na utawala bora. Tunailalamikia serikali iliyoko madarakani kwa maovu na mabaya inayoyafanya na mengi kwa kuona ni kutofuatwa kwa utawala bora. Leo hii tunaacha katika kusimamia misingi thabiti ya kuifanya nchi hii iwe ni mahali pazuri kwa kila mwanajamii, tuaanza kuwa bias na kuonesha kuwa kelele zetu zote hazina malengo maalum zaidi ya kelele za chura ambazo hazimzuii mtu kuchota maji.
Leo kama unapata nafasi ya kurejea postings za baadhi ya wachangiaji humu katika threads tofauti lakini topics zinayofanana, utaona hakuna consistency, wachangiaji wanaangalia personalities badala ya issues.
Mengi kama anao ushahidi au vielelezo alipashwa kuviwasiliasha katika mamlaka husika na si vinginevyo, sasa inaoneka kuwa amefanya hivyo kwa maslahi binafsi na wala si ya watanzania kwani wote alowataja ni wafanyabiashara wakubwa na wengine ni mahasimu wake wa siku nyingi.
 
Tuziachie mamlaka husika zifanye kazi ya kutoa hukumu na si vinginevyo.

Inaonekana kwako mamlaka "husika" za kutoa hukumu ni pamoja na mawaziri! Ungenipa moyo kuwa unajaribu kuwa fair kama ungepinga kitendo cha Mkuchika na Simba kumhukumu Mengi bila kumfikisha mahakamani au kumpa nafasi ya kujitetea! Hukufanya hivyo na hivyo kuthibitisha kuwa una maslahi zaidi ya kutaka haki itendeke kwa kila mhusika.

Mkuu mwanakijiji nadhani ndugu yetu anaitaji kuelimishwa...siasa aliyoiacha bongo those days sio inayoendelea hivi sasa.am sorry sijui wakati anaondoka nchini hata EPA aliisikia..well n Gud is a goodbr..ila nafikiri kama tungekuwa tunawaachia mamlaka hata
alipokuwa ATCL alikemea watu walioteuliwa na RAIS...Mbona akuiachia mamlaka kuhukumu makosa yanayotendeka........tu mmwombe mungu sana atupe ufahamu na busara hapo ndipo utakapoenda kujua jambo jema na baya......\
kila la kheri...mi kwa ushauri kama unaweza kutusaidia ungewasiliana na bibi SOPHIA LION THEN UWAAMBIE WATANGULIE MAHAKAMANA NA MKUCHIKA WAKE SISI TUTAKUWA NYUMA YAO...EMBU ANGALIENI WAZIRI MWENYE AKILI TIMAMU WA HABARI ANASEMA TUTAFUTA MIKANDA YA USHAHIDI KAMA KWELI ALISEMA...KWA NINI USIMUULIZE MKEO NYUMBANI ,KWA NIN ILIKUWA SIRI NA JANA USIKU WAMERUDIA NA KUKUSAIDIA UPATE MKANDA KAMILI ANGALIA KESHO USIKU TENA HOTUBA YA MENGI ..UUREKODI VYEMA....
HAYA MAPEPO SIJUI YAMETOKEA WAPI SERIKALINI.....TUKISEMA SERIKALI YA KUOMBEA MMMHHH...ANGALIENI VINAVYOWAPANDA MATOKEO YAKE WANAKIMBILIA TANGA ....NANI AMEKWAMBIA TANGA WANAPONYA VICHAA??
 
Angalia hawa mawaziri walivyo vichaa wakati wakigombea uwt mengi alipitishwa sufuria na kuchanga hela nzuri tu kwa mema .sas ahivi ameanza kujisikia anakaribia kiti cha ikuluu...sasa na salma aseme nini mama,angalia tu usimrudi mwenzi bi salma mtoto wa mjini yule aongei maramoja....maneno machache kazi kubwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Pumbavu zaoooooooooooo kabisa .....mi ndipo ninapoona hata ze utamu tunaitaji kuwaweleta humu walete heshimu kwa machizi kama hawa.....msifikiri mtu na akili zake kaenda kupeleka picha ya rais ze utamu kuna mambo yamemfika kooni...wacha usipime...atubariki uchafu ule lakini upumbafu kama wa hawa mawaziri ndio unapelekea na yeye kuwepo kwenye kapu la waliooza.....rais lini utaelimika lini utaisikiliza jf????
Moto watauona mwaka huu.....kufa hawatakufa....
 
Mkuu,
Mimi ninakuunga mkono 100% katika maoni yako hapo juu.
Ni jambo la kusikitisha kwa baadhi ya JF members kuona kuwa hii forum inapigania nchi yetu itawalie kwa kufuata misingi ya haki na utawala bora. Tunailalamikia serikali iliyoko madarakani kwa maovu na mabaya inayoyafanya na mengi kwa kuona ni kutofuatwa kwa utawala bora. Leo hii tunaacha katika kusimamia misingi thabiti ya kuifanya nchi hii iwe ni mahali pazuri kwa kila mwanajamii, tuaanza kuwa bias na kuonesha kuwa kelele zetu zote hazina malengo maalum zaidi ya kelele za chura ambazo hazimzuii mtu kuchota maji.
Leo kama unapata nafasi ya kurejea postings za baadhi ya wachangiaji humu katika threads tofauti lakini topics zinayofanana, utaona hakuna consistency, wachangiaji wanaangalia personalities badala ya issues.
Mengi kama anao ushahidi au vielelezo alipashwa kuviwasiliasha katika mamlaka husika na si vinginevyo, sasa inaoneka kuwa amefanya hivyo kwa maslahi binafsi na wala si ya watanzania kwani wote alowataja ni wafanyabiashara wakubwa na wengine ni mahasimu wake wa siku nyingi.

I can't argue with you mkuu because you make a good point. I am against discrimination in any shape, form or manner be it racism, sexism, tribalism, religionism etc. but don't you think we should at least hear that evidence that Mengi claims to have? The mannerism in which he used in this case is wrong but since the cat is out of the bag why don't we just hear what he claims to know? Instead ya kujigawa kati ya wanaozani Mengi mzalendo halisi na wanaoona Mengi ana agenda zake kwa nini tusidai atoe huo ushahidi wake tujue moja? Akisha toa huo ushahidi ndiyo tutajua nia haswa ya Mengi. Mengi is not above the law but neither are the mentioned people. If he really has the evidence let the authorities ask him to give it & deal with the matter according to the laws of the country. I am tryin to be unbiase the best I can here so mimi naona ili kujibu maswali yote haya Mengi atoe ushahidi anaodai kuwa nao halafu sheria ichukue mkondo wake. Maana kama kuwataja hao watu ambao ni innocent untill proven guilty kashawataja kwa hiyo hamna maana kubishana kama njia aliyo tumia ni sahihi au la. kilicho baki atoe ushahidi wake kama una basis sheria ifuate kama mzee mzima aliji ropokea tu basi na sheria uchukue mkondo wake. Jamani wana JF mnaonaje? I think thats fair but its only my opinion.
 
Last edited:
Mkuu,
Mimi ninakuunga mkono 100% katika maoni yako hapo juu.
Ni jambo la kusikitisha kwa baadhi ya JF members kuona kuwa hii forum inapigania nchi yetu itawalie kwa kufuata misingi ya haki na utawala bora. Tunailalamikia serikali iliyoko madarakani kwa maovu na mabaya inayoyafanya na mengi kwa kuona ni kutofuatwa kwa utawala bora. Leo hii tunaacha katika kusimamia misingi thabiti ya kuifanya nchi hii iwe ni mahali pazuri kwa kila mwanajamii, tuaanza kuwa bias na kuonesha kuwa kelele zetu zote hazina malengo maalum zaidi ya kelele za chura ambazo hazimzuii mtu kuchota maji.
Leo kama unapata nafasi ya kurejea postings za baadhi ya wachangiaji humu katika threads tofauti lakini topics zinayofanana, utaona hakuna consistency, wachangiaji wanaangalia personalities badala ya issues.
Mengi kama anao ushahidi au vielelezo alipashwa kuviwasiliasha katika mamlaka husika na si vinginevyo, sasa inaoneka kuwa amefanya hivyo kwa maslahi binafsi na wala si ya watanzania kwani wote alowataja ni wafanyabiashara wakubwa na wengine ni mahasimu wake wa siku nyingi.

Kukaa kimya kwao ina maana ni ukweli, na kama si kwelil wamshtaki maana shutuma hizo ni kubwa. Nadhani Mengi ana ushahidi kwa aliowasema na kama ulivyosema, '' ni wafanyabiashara wakubwa na wengine ni mahasimu wake siku nyingi''. Anawajua vizuri.
 
Back
Top Bottom