Mwitikio wa serikali na wananchi kusaidia wahanga wa milipuko ya Mbagala

Samahani,

Naomba kuuliza ukiwa una ka-kiosk kako, na umwemwajiri muuza ka-kiosk hako... akawa wateja wakinunua vitu akirudisha chenji arudisha zaidi kwa wateja wake... Na wateja wanachukua wanaendelea wanarudi na siku nyingine hivyo hivyo mpaka kaduka kako kanatereka...

Nani wakumfuata... muuza kiosk chako? au mteja?

I mean:
Muuza duka... ni mtumishi wa umma
Mteja ndio:... huyo RA


Rostam si mteja...! hana mfanano na mteja.. hatendi kama mteja.. mteja akijua amepewa chenji asiyostahili na akaamu kuibania anavuka mpaka wa mteja na kuwa .....
 
Pamoja na post zote... Lazima nisema RA has been amoung the most successfully and intelligent businessman in Tanzania.

Tungekuwa na wakina RA wengi Tanzania uchumi wa nchi ukiuwa imara na uwekezaji wetu kwenye nchi za Maziwa makuu na SADC ungekuwa mkubwa sana.

Angalia biashara anazozifanya, ndio zile wabongo waoga na wanadhani zinatakiwa kufanywa na makampuni ya Ulaya tu.

Issue ya Kasoro alizonazo kama anazo zinatokana na mfumo wenu wa kipumbavu... ni kazi kwenu kutumia Bunge kuziba mianya.

Nevertheless,,, tafuteni wanasiasa au watumishi wauma wanaomfaidisha huyo RA na sio RA.

Asubuhi njema, mchana mwema jioni njema na usiku mwema kutegemea ulipo

Anatuibia mabilioni na si ajabu trillioni halafu akitoa vilaki vichache mnamuona mtu wa maana sanaaa!!!!

Kagoda bilioni 40, Richmond/Dowans bilioni 200 na si ajabu kuna ufisadi mwingine ambao haujajulikana.

Hatutaki kabisa kuwa na akina mafisadi RA wengi hawa wachache tu Serikali inawaogopa kuwachukulia hatua pamoja na ushahidi wa kutosha wa ufisadi walioufanya na wanaoendelea kuufanya dhidi ya nchi yetu. Hebu tuondolee UPUUZI WAKO wa kuwapigia debe mafisadi!
 
Nafuta ajira kwa jamaa, ili nikaweke sawa mambo madogo madogo lakini biashara yetu itaimarika especially baada ya kukuwa na corporate governance... that is the only thing lacking in his group of companies...

Ngoja nimtafute... naomba contacts... naweza lamba dume...
 
Nafuta ajira kwa jamaa, ili nikaweke sawa mambo madogo madogo lakini biashara yetu itaimarika especially baada ya kukuwa na corporate governance... that is the only thing lacking in his group of companies...

Ngoja nimtafute... naomba contacts... naweza lamba dume...

namba yake ya simu ipo kwenye tovuti ya Bunge..
 
Ukisoma vizuri report ya CAG utagundua kwamba asilimia kubwa ya watumishi wa umma waliopo kwenye sehemu za manunuzi au wanaoidhinisha matumizi ya fedha ni wezi... kwa mfano kuna wizara moja imenunua photocopier 3 kwa mili karibia 60....

Ndio maana mimi naona ni uhuni kufikiria mtu mmoja.
 
Zungu Pule,

Kwa suala la rushwa huwezi kumpata RA, by the way he is smart, angekuwa mtu wa kuingia kichwa kichwa mungeshampeleka mahakamani,,, hamumpeleki kwa sababu gani?

Still admire the guy,,, anafanya biashara zenye akili! mengine ni uzembe wenu na serikali yenu... maana munapenda siasa sana.


.........KWA SABABU YA WATU KAMA NYINYI !!!:mad::mad::mad:
 
Nafuta ajira kwa jamaa, ili nikaweke sawa mambo madogo madogo lakini biashara yetu itaimarika especially baada ya kukuwa na corporate governance... that is the only thing lacking in his group of companies...

Ngoja nimtafute... naomba contacts... naweza lamba dume...

Rostam Abdulrasul Aziz
P.O. Box 11, Igunga,
Mob. +255 754 555555

I hope that helps, all the best..
 
Kasheshe,Mwanakijiji,..

..hivi Rostam Azizi ametokea wapi?

..ameanza na biashara ipi mpaka kujijenga kufikia hapo alipo?

..hivi sasa Rostam ana biashara gani halali, na zisizo halali?

..how much does he worth?
 
Kasheshe,Mwanakijiji,..

..hivi Rostam Azizi ametokea wapi?

..ameanza na biashara ipi mpaka kujijenga kufikia hapo alipo?

..hivi sasa Rostam ana biashara gani halali, na zisizo halali?

..how much does he worth?

Jamaa hana biashara haramu hata moja... labda hiyo ya New HCL... ambayo kidogo mambo hayajakaa sawa on corporate governance point of view... ingawa sio per se anatatizo maana hata makampuni ya umma mengine yana matatizo hayo hayo...

Mimi nafahamu kampuni la ujenzi ambalo linafanya vizuri kubwa na la uhakika...

Pili share za VodaCom Lazima zilimrusha juu sana... lakini mtu yeyote aliyeshika hela na alikuwa na elimu kama yeye wakati sisi wote tumelala lazima awe tajiri zaidi.

Hata Mheshimiwa Mengi, analia sana siku hizi kwa kuwa anabanwa kila mahali... sehemu tu ya ukakika kwake angalu ni Bonite huku kwingine everything tight... kinoma.
 
Ukisoma vizuri report ya CAG utagundua kwamba asilimia kubwa ya watumishi wa umma waliopo kwenye sehemu za manunuzi au wanaoidhinisha matumizi ya fedha ni wezi... kwa mfano kuna wizara moja imenunua photocopier 3 kwa mili karibia 60....

Ndio maana mimi naona ni uhuni kufikiria mtu mmoja.
Kweli, tunaibiwa sana humu kwenye maofisi ya umma... lakini kelele nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa wachache. Si ajabu waswahili walisema ... avumaye baharini...
 
Kasheshe,

..shares za Vodacom alinunua ngapi na kwa kiasi gani?

..pia kampuni yake ya ujenzi aliianzisha lini kwa mtaji kiasi gani, ilifanya projects zipi, na sasa anafanya project gani?
 
Kasheshe,

..shares za Vodacom alinunua ngapi na kwa kiasi gani?

..pia kampuni yake ya ujenzi aliianzisha lini kwa mtaji kiasi gani, ilifanya projects zipi, na sasa anafanya project gani?

It is now historical!!!
 
Ukisoma vizuri report ya CAG utagundua kwamba asilimia kubwa ya watumishi wa umma waliopo kwenye sehemu za manunuzi au wanaoidhinisha matumizi ya fedha ni wezi... kwa mfano kuna wizara moja imenunua photocopier 3 kwa mili karibia 60....

Ndio maana mimi naona ni uhuni kufikiria mtu mmoja.

Kusipokuwa na mkakati maalum wa kudhibiti ubadhirifu kwenye sekta ya umma, hususan sehemu ya manunuzi wimbo wa ufisadi utaendelea kurindima mpaka masikio yapasuke.
 
Leo nilikuwa nikisikiliza BBC, watu wakihojiwa kuhusu ahadi ya Serikali kuwasaidia na kuwalipa fidia wahanga wa mabomu yaliyolipuka mbagala. Baadhi ya wahanga wanalalamika hawajapata msaada wowote na wagawa misaada hao wamevaa nguo za kijana (baadaye akasema ni makada wa CCM). Hilo halikuwa tatizo kwangu kwani kwenye ajali kila mtu ana haki ya kusaidia na huo ndiyo Utanzania wetu.

Kilichonishangaza ni kw malalamiko ya wahanga kusema kuna agenda za kisiasa kwa priority, kwani wana CCM wanapewa kipaumbele zaidi katika misaada kama chakula. Siwezi kusema kuwa malalamiko haya huenda yana ukweli kwani hayajathibitishwa na makundi ya haki za binaadamu, ila kitendo cha malalamiko kama haya katika kipindi hiki yanaonesha ni jinsi gani nchi inapoanza kumomonyoka ki-mshikamano kutokana na siasa kuwekwa mbele kila sehemu.

Matarajio yangu ni kwamba Serikali itatekeleza yale iliyoahidi kwa wahanga bila kujali wanapeperusha bendera gani nje ya nyumba zao. Kwani mabomu hayo yalipolipuka hayakuchagua itikadi badi yalimuathiri kila mtanzania aliyekuwa karibu au mwenye bahati mbaya.

Watu walioathirika kutokana na milipuko ya mabomu kwenye ghala la silaha katika kitongoji cha Mbagala nje kidogo ya Dar Es Salaam, bado wanasubiri misaada iwafikie.
Serikali ya Tanzania imeahidi kulipa fidia kwa watu wote walioathirika na milipuko hiyo, ambayo ilijeruhi mamia ya watu na kuua 20 juma lililopita.
Lakini baadhi ya wakazi wa maeneo hayo bado hawajapata msaada wa kutoksha wa malazi na chakula kwa mujibu wa Vicky Ntetema. Serikali imeunda tume ya kuchunguza chanzo cha mlipuko huo.
Wakati baadhi ya familia zikiwa zimepokea msaada wa dharura yakiwemo mahema, magodoro na chakula, watu walioko umbali wa kilometa moja kutoka eneo la tukio wanalazimika kulala kwenye mabaki ya nyumba zao zilizobomoka.
Tukio hilo lilizua hofu miongoni mwa wakazi wa Dar Es Salaam wakifikiri kumetokea shambulio jingine la kigaidi kama ilivyokuwa katika ubalozi wa Marekani mwaka 1998 jijini Dar Es Salaam.

Source: BBCSwahili.com | Habari | Milipuko Tanzania: Misaada yachelewa

unaweza kusikiliza hapa http://www.bbc.co.uk/mediaselector/check/swahili/meta/tx/swahili_1530?size=au&bgc=003399&lang=sw&nbram=1&nbwm=1
 
Last edited:
Fisadi kawaida anakuwa na roho mbaya. Sio tu anapenda kujilimbikizia kila kitu lakini pia hapendi hata kidogo kuona mwingine zaidi yake anakipata nafuu. Kwao maisha bora ni kwa kila fisadi. Inawauma kuona mwanachama wa cuf pale mbagala akisaidiwa na serikali. Wamechukua magodoro ya msaada wamepeleka kwenye gesti zao. Hio ndio tabia ya fisadi. Msitegemee awe fair hata siku moja.

Kinachonishangaza mimi ni kwamba tunaambiwa nyumba 750 zimeteketezwa na mabomu ilhali watu 23 tu ndio waliofariki! Wanajeshi waliokufa ni sita tu tena miili yao imeokotwa kwenye mto. Pale kwenye ghala la silaha palipolipuka inamaana hapakuwa na mtu au ndio hio miili ilirushwa hadi mtoni? Kuna watoto mpaka leo wazazi wao hawajajitokeza kuja kuwachukua na wanaonekana kwenye tv kila siku, kulikoni? Tutadanganyana mpaka lini kuhusu hii idadi ya waliopoteza maisha katika hili tukio. Ni mzembe gani huyo anayelindwa hivi? Tunaficha ukweli ili wakubwa waendelee kula hata wakivurunda.
 
Inashangaza! Tatizo njaaaaaa ...Tanzania walioelimika na wasio elimu wote njaaaaaaaaa. Wafanyafa mambo bila kuona message gani inatuma...bado tuko nyuma saaaaana kisiasa!!
 
...Kinachonishangaza mimi ni kwamba tunaambiwa nyumba 750 zimeteketezwa na mabomu ilhali watu 23 tu ndio waliofariki! Wanajeshi waliokufa ni sita tu tena miili yao imeokotwa kwenye mto. Pale kwenye ghala la silaha palipolipuka inamaana hapakuwa na mtu au ndio hio miili ilirushwa hadi mtoni? Kuna watoto mpaka leo wazazi wao hawajajitokeza kuja kuwachukua na wanaonekana kwenye tv kila siku, kulikoni? Tutadanganyana mpaka lini kuhusu hii idadi ya waliopoteza maisha katika hili tukio. Ni mzembe gani huyo anayelindwa hivi? Tunaficha ukweli ili wakubwa waendelee kula hata wakivurunda.
ni kwamba mabaki ya skeletons yaliyookotwa kwenye ghala la kambi ndiyo yaliyothibitisha kuwa wanajeshi watano walikufa hivyo si mtoni kama ulivyoquote. ila kuhusu mtoni ni kwamba watoto wengi wameripotiwa na mashuhuda kuwa wamezama humo na mkuu wa mkoa amesema kazi ya utafutaji inaendelea.
kinachonishangaza mie ni kwamba wanaficha idadi halisi ya waliokufa maana kama watu wengi hawaonekani tena watu wazima ina maana hawana utashi tena na wamekufa mbona hawasemi hivyo? kuna kituo kimoja cha TV ktk taarifa yake ya habari kilisema kwamba imegundulika kuwa wahanga waliokusanyika ktk makambi maalum si wote ni wahanga kwa kigezo kwamba hawatoi ushirikiano ktk kuwatambua wao na ndugu zao ...this is another crap.
 
Hivi huu mshikamano ambao sasaunadaiwa uko hatarini kubomoka ni maneno ya siasa ama kweli ulikuwepo?

Hakuna kinachobomoka, kitokeacho ni ari ya Watanzania kueleza maoni yao bila hofu.


Kuweka siasa kwenye kila kitu ni sawa tu kama kuna hoja ya msingi pem,beni yake.

CCM iliingiza siasa kila mahali , mpaka leo bado inag'ang'ania kulazimisha siasa kila Mahali.

CCM inatumia wanajeshi wa JWTZ,POLISI na usalama wa Taifa kama watumiavyo kitengo cha umoja wa Vijana wa CCM.
Huku si kuingiza siasa kila mahali?

CCM wanaitumia jumuia ya Wafanyakazi wa Tanzania kama jumuia ya CCM.
Huu nao si uchuro wa kuingiza siasa za kiCCM vichwani mwa wafanyakazi wote

CCM wanatumia BOT kama ghala la fedha za CCM.


Sioni tatizo kwa mtanzania yeote kutumia jambo lolote apendalo kisiasa, tatizo nionalo ni mtu kutumia jambo fulani kisiasa na kutumia nafasi yake katika jamii kulazimisha watu wengine watumie jambo lile kwa namna aitakayo yeye.
 
Jana nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari ya Luninga. Moja wapo ya habari nilizozisikia ni ile ya Wananchi ambao siyo Wahanga wa milipuko ya mabomu kujichomeka kwenye kuhitaji kupewa misaada ya maafa hayo. Sehemu ya taarifa hiyo ilieleza kuwa mfano kuna mtu ana nyumba yake Mbagala lakini yeye anaishi Kimara; lakini wakati wa kugawa misaada na yeye anaingia kwenye foleni akitaka apatiwe misaada hiyo.

Hapa ndipo niliona kuna somo mojawapo kwa serikali juu ya umuhimu wa kuwa na kumbukumbu zinazowahusu raia wake (nani ni nani?, anaishi wapi?, anafanya nini?, n.k.), lakini hakuna utaratibu wa aina hiyo; kwa nini watu wasiione hiyo kuwa fursa ya kuichuna serikali ambayo kwa kiasi kikubwa huwa haiwajali Raia wake. Mfano mimi nimehamia Dodoma karibu mwaka wa tatu sasa, lakini sijamwona mjumbe wa Mtaa wala nani akija kunifuata walau kwa ajili ya kunisajili. Lanini watu wa Kanisa tayari walishanisajili kwenye Jumuia Ndogondogo na kunipatia na Uongozi. Kwa nini Serikali yetu inashindwa kuweka utaratibu ambao utawezesha taarifa kama hizi kupatikana.
 
Wasalamu wanaJF.

Mimi napata tabu sana na jinsi vyombo vingi vya habari vinavyopotosha umma juu ya neno Mhanga! Nijuavyo mimi Mhanga ni mtu anayejitolea uhai wake kwasababu fulani kama jamaa zetu Palestina, sasa waliopata Ajali ama wale waliolipukiwa na Mabomu kwa bahati mbaya au kutokana na uzembe wa wahusika fulani tutawaitaje wahanga!!? Mi nadhani neno linalistahili ni Wa-athirika! Au mnasemaje?

Naomba mnisaidie ndugu zangu kiswahili nadhani kinanipa tabu.
 
Back
Top Bottom