Mwitikio wa serikali na wananchi kusaidia wahanga wa milipuko ya Mbagala

Jasusi,
Lukuvi katamka nini Lukuviiiii? Nionyeshe Lukuvi katamka nini. Ha ahahahahahaha

Wala sijatetea au kukosoa alichofanya au kutofanya Lukuvi.

Yeyote yule anaejua alichotamka Lukuvi kuhusu kuzoeleka kelele za ndege na akiweke hapa neno kwa neno.

Nilimsikia akihohiwa na BBC nikamshangaa sana. Mwandishi wa BBC alimwuliza kuwa imeripotiwa watu kadhaa wamekuwa vziwi kwa sababu ya mabomu. Lukuvi alijibu kwa hamaki na haraka kuwa "huo ni uwongo!' Kama kiongozi, nadhani angejibu sijapta taarifa na kuahidi kufuatilia suala hilo na si kung'aka! Sasa Dilu habari za uhakika ni kweli kuwa kuna baadhi ya watu wameathiriwa na kuwa viziwi na kutoona vizuri sababu ya mabomu hayo. Ni vema asingejibu vile.
 
Okay, huyu jamaa ni mjinga na anastahili kutolewa hapo haraka sana.
Swali: Kazi hasa ya mkuu wa mkoa ni nini?
 
Hivi kuna ulazima wowote kuwa ukienda kutoa msaada kwa wahanda wa mabomu ya Mbagala lazima uvae mashati ya kijani? Je hili siyo janga la kitaifa kwani hawa wanaovaa nguo za kijani si ndiyo wanaojivuna kuwa hawana sera za kibaguzi? au ndo mnataka kutufanya tupumbazike na kuamini kuwa mnajali sana wakati Serikali mnayoiongoza ilitaarifiwa juu ya hatari ya uwezekano wa kulipuka mabomu hayo lakini ikakataa kutoa fedha za kuteketeza mabomu hayo!
 
Na Lukuvi akawataka wakazi wa Mbagala kuzoea milipuko kama wenzao wa Kipawa, wanaoishi jirani na Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, walivyozoea kelele za ndege.

Kwa hiyo hiyo ripoti ya kichwa cha habari si ya kweli? Mwandishi katunga?

Mtumeee! Yani concept ya reported speech na direct speech haileweki hata kwako Jasusi? Jasusi, hayo ni maneno ya mwandishi, siyo ya Lukuvi. Kumbe ndio maana press yetu inadumaa, tunaamini vitu kichwa kichwa?

Naomba tuwekee habari ya miungurumo ya ndege Kipawa kama alivyotamka Lukuvi neno kwa neno, na utoe chanzo unless ulikuwepo. Na kama ulikuwepo, ulimsikia kwa masikio yako, sema ulisikia lini, nini, wapi, saa ngapi.
 
Huwezi ukaripoti habari kuhusu kauli tata ya kiongozi bila kusema alitamka nini kwa maneno yake mwenyewe.

Yeyote yule anaejua alichokisema Lukuvi kuhusu kuzoeleka kwa milio ya ndege na akiweke hapa word for word.

Yale yale ya Makamba kumwambia Nape kuwa aliyoyafunda Duniani na mbinguni ameyagunga, halafu baadaye utetezi unakuja ooooh waandishi wameninukuu vibaya, oooooh ni kwa sababu mimi nimezoea mno kutumia maneno ya Bibilia. Upuuzi mtupu. Hebu ona Jese Jackson alivyonaswa akimsema Obama kwenye moja ya hotuba zake za kampeni ni nini alichokifanya kama siyo kuomba radhi. Sasa viongozi wetu hilo linakuwa gumu kweli kweli.

Ngoja niwakumbushe kauli nyingine tata za Viongozi wetu:

Mathew Karesi aliwahi kuwaambia wapigakura wake wapange foleni ya ndoo ili azikojolea walipomtaka kutekeleza ahadi aliyowaahidi kuwatatulia tatizo la ukosefu wa maji. Lakini Wambulu hawana mchezo uchaguzi ulivyofika wakamtupilia mbali kama walivyomkata Marehemu Nyerere. Na Karesi alivyo pewa kitengo kingine kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akaenda kukumbana na tatemeko, acha nyumba zidodoke. Lakini yeye akaja na kejeli kuwa wanambeya hawajui kujenga nyumba, wanajenga nyumba ambazo hata kuku akichakura na kuipiga teke tu itaanguka

Basil Mramba naye katika kuhalalisha ulaji kwenye manunuzi ya ndege ya Rais ambayo kwa sasa inasemekana ni mbovu akatuambia hata kama ikilizimika kula majani wananchi wa Tanzania watakula, ilimradi ndege inunuliwe.

Marehemu Dito naye alivyofumaniwa na mke wa mtu akatuambia kwao Wazaramu kufumaniwa ni sifa mojawapo

Yele ya Mkuchika juzi kwenye kampeni za uchaguzi wa Busanda ya Wananchi kutoweza kuangalia taarifa za kwenye Runinga kwa sababu hawana umeme, kutoweza kununua magazeti kwa sababu hawana fedha.

Mwenye kukumbuka kauli nyingine aongezee
 
He is not std 7 leaver, c his profile: He is extraordinary~ remarkable~ astonishing Tanzanian. Within 4 years (1980-1983), he managed to do certificate in defence, form 5&6 and attended a 1? 2? year diploma course in Moscow. And 2001 he graduated at WIU. He is great!

Kwa nini NECTA wanaishia Chuo cha Ualimu Kange tu! kama mafuta yamewaishia si waongeze ili wachape mwendo na kuwafikia hawa kina Kajituliza Kasuku?
 
Yale yale ya Makamba kumwambia Nape kuwa aliyoyafunda Duniani na mbinguni ameyagunga, halafu baadaye utetezi unakuja ooooh waandishi wameninukuu vibaya, oooooh ni kwa sababu mimi nimezoea mno kutumia maneno ya Bibilia. Upuuzi mtupu. Hebu ona Jese Jackson alivyonaswa akimsema Obama kwenye moja ya hotuba zake za kampeni ni nini alichokifanya kama siyo kuomba radhi. Sasa viongozi wetu hilo linakuwa gumu kweli kweli.

Ngoja niwakumbushe kauli nyingine tata za Viongozi wetu:

Mathew Karesi aliwahi kuwaambia wapigakura wake wapange foleni ya ndoo ili azikojolea walipomtaka kutekeleza ahadi aliyowaahidi kuwatatulia tatizo la ukosefu wa maji. Lakini Wambulu hawana mchezo uchaguzi ulivyofika wakamtupilia mbali kama walivyomkata Marehemu Nyerere. Na Karesi alivyo pewa kitengo kingine kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akaenda kukumbana na tatemeko, acha nyumba zidodoke. Lakini yeye akaja na kejeli kuwa wanambeya hawajui kujenga nyumba, wanajenga nyumba ambazo hata kuku akichakura na kuipiga teke tu itaanguka

Basil Mramba naye katika kuhalalisha ulaji kwenye manunuzi ya ndege ya Rais ambayo kwa sasa inasemekana ni mbovu akatuambia hata kama ikilizimika kula majani wananchi wa Tanzania watakula, ilimradi ndege inunuliwe.

Marehemu Dito naye alivyofumaniwa na mke wa mtu akatuambia kwao Wazaramu kufumaniwa ni sifa mojawapo

Yele ya Mkuchika juzi kwenye kampeni za uchaguzi wa Busanda ya Wananchi kutoweza kuangalia taarifa za kwenye Runinga kwa sababu hawana umeme, kutoweza kununua magazeti kwa sababu hawana fedha.

Mwenye kukumbuka kauli nyingine aongezee

Lukuvi alisema nini? Direct quote (ile kauli iliyo kati ya " na ") iko wapi?
 
Lukuvi alisema nini? Direct quote ... iko wapi?

Haa hahaa aaaaaa Blue Ray, yani kuna mambo fulani tuko nyumba Wabongo. Hatujali facts and specifics.

You know what baffles me though? Direct quotation sio foreign concept, utotoni ukimshtaki mtoto wa jirani utadaiwa specifics. Mamaaa, Madenge mchokozi; Kakufanya nini Madenge? Kanitukana; Kasemajeee?

Yeyote anaejua alichotamka Lukuvi kuhusu kelele za ndege na akiweke hapa neno kwa neno! Ha hahaaaa aaa
 
Mtumeee! Yani concept ya reported speech na direct speech haileweki hata kwako Jasusi? Jasusi, hayo ni maneno ya mwandishi, siyo ya Lukuvi. Kumbe ndio maana press yetu inadumaa, tunaamini vitu kichwa kichwa?

Naomba tuwekee habari ya miungurumo ya ndege Kipawa kama alivyotamka Lukuvi neno kwa neno, na utoe chanzo unless ulikuwepo. Na kama ulikuwepo, ulimsikia kwa masikio yako, sema ulisikia lini, nini, wapi, saa ngapi.

Dilunga,
Ningependa kuamini kuwa huyu mwandishi wa habari hakutunga hii stori ingawa haina direct quote. Sikuwepo lakini nawapa waandishi the benefit of the doubt, na fact kwamba sasa ni siku zaidi ya moja Lukuvi hajakanusha kuwa amekuwa misquoted. That's all
 
Yaani bada ya matatizo yote ya waandishi wa habari wa kibongo wewe bado unawapa the benefit of the doubt tu?
 
Duuuh check na wageni walivyojaa...

Currently Active Users Viewing This Thread: 21 (3 members and 18 guests)
Tusker Bariiiidi, Lole Gwakisa, Recta

Tusker, isijali mkuu. Suala la mkuu wa mkoa kwa ar es salaam ni nyeti sana.Mkuu wa mkoa wa Dar ni mtu very powerful kuliko mawaziri wengi sana.
Hatakiwi kuwa kichwa cha mwenda wazimu, mtu wa kujifunzia kazi hapa.
Na Dar kuna kila aina ya mtu kuanzia machinga,changudoa,Mabalozi wa Nje hadi Rais wa Jamhuri.
 
Dilunga,
Ningependa kuamini kuwa huyu mwandishi wa habari hakutunga hii stori ingawa haina direct quote. Sikuwepo lakini nawapa waandishi the benefit of the doubt, na fact kwamba sasa ni siku zaidi ya moja Lukuvi hajakanusha kuwa amekuwa misquoted. That's all

Utasemaje akanushe "amekuwa misquoted" wakati hajawa quoted? Wapi kawa quoted? Ha hahahaaaa

"Ungependa kuamini"? Unasemaje? Ungependa kuamini, kwa hiyo huamini. Hata wewe huamini! One thing about you Jasusi ni kwamba uko very civil, most of the times. Hapa unakiri kwamba hujui kilichosemwa. Aksante.

Here is the thing Mkuu Jasusi. Hatusemi mwandishi kaota ndoto. Kuna kitu kinaitwa interpretation, kingine kinaitwa distortion, kingine embellishment. Ndio maana watu hudai quotes. Usinitafsirie, nipe quotes.

Unawapa waandishi "benefit of the doubt"? Ma tabloid ya Bongo kila siku wanatolewa nishai na Rostam kotini? Rostam of all people. Na sio lazima ukanushe ndio iwe uongo. Wengine hukaa kimya unasikia jaji kamkanushia.

Sisemi habari ni uongo, nasema anaejua alichotamka Lukuvi kuhusu kelele za ndege na akiweke neno kwa neno.
 
Sasa hapa mimi siasa za kitanzania ndio zinapokera, Huyu Lukuvi ni mbunge halafu huyu huyu Lukuvi ni mkuu wa mkoa wa dar es salaam. Dar ni mkoa mgumu sana kwanini Vasco asingemchagua mtu ambaye angekuwa committed na hii kazi, na kuna hule msemo mshika mawili...
 
Lukuvi hana lolote.

Zamani kidogo miaka ya 90 nilikuwa nafanya kazi na dada mmoja ambaye aliwahi kusoma chuo cha uhazili Tabora. Akawa anashangaa kwamba Lukuvi alikuwa amejipenyeza na kukubalika kwenye siasa. Kwa mujibu wa huyo dada Lukuvi alikuwa ni jamaa aliyekuwa kuwa anafahamika sana hasa kwa kufukuzia kina dada wa uhazili wakati akisoma chuo cha ualimu Tabora. Ni mwalimu wa Grade A (shule ya msingi).

Kilichotokea baada ya pale alifanya kazi mikoa ya kusini (Masasi kama sikosei) kama mwalimu wa shule ya msingi. Ni huko alikojihusishwa na mambo ya chipukizi wakati ule, walikiwatumia watoto wa shule kuimba nyimbo za halaiki. Akawa mwepesi kujipendekeza kwa makada na mambo kama hayo.

Hizo qualifications zingine ndo zile za kuungaunga mitaani. Hazina kichwa wala miguu. Matokeo yake ni hayo. Anadhani kuwa maisha ya watanzania ni rahisi kuyachezea kama anavyotaka kwa vile tu amebahatika kupanda katika medani za siasa bila kuhangaika kusoma kwamba kama wengine.
 
Lukuvi inabidi atengenezewe thread yake peke yake...yale madudu aliyozungumza kwenye msiba wa IDDI NYUNDO nikajua kuwa kazi tunayo watu wa Dar

Lukuvi kazi waliyompa ni kubwa mno ukilinganisha na kisomo chake; ni darasa la saba ingawa ana cheti cha degree cha kugushi!! Historia ya utendaji wake toka alivyokuwa umoja wa vijana wa CCM ni ya utatanishi; mnakumbuka mradi wa mabasi ya shule ya watoto wa Dar? Lukuvi alikuwa mmoja wa watu waliohusika moja kwa moja kuufilisi mradi ule. Mtu kama huyo mnategemea atakuwa kiongozi wa maendeleo; kazi anayoimudu huyu bwana ni ile ya kusindikiza na kupokea viongozi pale kiwanja cha ndege tu!!
 
Lukuvi naye ni kama Mabomu ya Mbagala... yameanza kulipuka moja baada ya jingine.... alianza na kauli za Kipawa... (Msiniombe quote tafadhali) Boooooooom!! na bado ataendelea kulipuka.

Lukuvi kama kambi za jeshi zilizowazingira wakazi wa jiji la Dar Es Salaam apaswa kufutwa kazi....Hana alijualo huyu. Mkoa ni mkubwa kuliko akili yake...

Miye nikitazama Tivii akianza kuongea Lukuvi tu, naizima...
 
aisee nimecheka sana
 
Sasa hapa mimi siasa za kitanzania ndio zinapokera, Huyu Lukuvi ni mbunge halafu huyu huyu Lukuvi ni mkuu wa mkoa wa dar es salaam. Dar ni mkoa mgumu sana kwanini Vasco asingemchagua mtu ambaye angekuwa committed na hii kazi, na kuna hule msemo mshika mawili...

Lyampinga msemo huu kama utakumbuka vizuri aliutumia mwanafunzi wa shule ya msingi Mkoani manyara kumwuuliza Lowasa wakati ule akiwa PM juu ya kukinzana kwake na hali halisi ilivyo kwa baadhi ya viongozi wa serikali na kwenye CCm. Inasemekana mtoto huyo alipata usumbufu wa hali ya juu toka kwa jamaa wa UwT kwa tuhuma kwamba alitumwa kuuliza swali hilo na wapinzani. Yaani hata pale kizani cha nchi hii kinapoonekana kinajaribu kuconceptualize na kuchanganua mambo kinakandamizwa na kulazimishwa kubakia na fikra duni
 
Mkuu kama sikosei ni wa Ukerewe Mwanza
 
Back
Top Bottom