Ilianza Babylonian empire ikapita
ikaja Medo-Persian empire ikapita
ikaja Greece empire ikapita
ikaja Roman empire ikapita.
baadaye ikaja UK kama world super power, baada ya WWII ikapita.
ikaja marekani na USSR na kua mwanzo wa wababe wawili kuibuka (bipolar powers) , USSR ikaanguka kipindi cha vita baridi, ikawa mwisho wa bipolar power, na hapo ndipo Marekani ikawa world superpower, wakaiita majina mengi kama American Hegemony, Kiranja mkuu wa dunia, msemaji wa mwisho katika masuala yote hata UN ipo chini yake na haiwezi sema kitu dhidi yake.
Kwa hali iliyopo naona Russia wanaangaika kurudisha bipolar power, sasa sijui nani ataweza kuondoa American hegemony. maana hadi sasa America ndio wanaongoza dunia kiuchumi na kijeshi. China wanaonyesha jitihada kuipiku America kiuchumi huku Russia wanaonyesha juhudi kuipiku America kijesha.
Ingawa naona itakuwa ngumu kuangusha American supremacy kwakuwa imeweka mizizi kupitia dollar economy nk... pia kupitia washirika wake wa NATO.