bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 975
- 2,349
Dunia inatazama kwa mshangao: 👉Iran inaandamwa na vikwazo vya kila aina, wanasayansi wake wanauwawa kwa siri, na kuta za nyuklia zinalipuliwa na majasusi. Lakini upande wa pili, Kim Jong-un anafanya majaribio ya makombora ya kinyuklia mbele ya satelaiti za Marekani, na jibu pekee ni "tunaangalia hali ilivyo."
Kwanini Marekani hawezi kutoa vitisho vya kijeshi kwa North Korea kama anavyofanya kwa Iran? Hizi hapa ndio sababu:
👇
1. "The MAD Doctrine" (Mutually Assured Destruction)
Tofauti kubwa kati ya Iran na North Korea ni hatua ya uwezo wa kinyuklia.
Iran bado yuko kwenye hatua ya "kutaka." Marekani anajua akishambulia sasa, anaweza kuharibu mitambo kabla bomu halijakamilika.
North Korea: 👉Tayari ana vichwa vya nyuklia zaidi ya 50. Muhimu zaidi, ana teknolojia ya "Miniaturization"—uwezo wa kufanya bomu la nyuklia kuwa dogo kiasi cha kutoshea kwenye ncha ya kombora.
Deep Secret: North Korea amefanikiwa kutengeneza makombora ya Hwasong-18 yanayotumia mafuta magumu (Solid Fuel). Hii ina maana anaweza kurusha kombora ndani ya dakika 5 bila Marekani kuona maandalizi kwenye satelaiti. Ukimgusa, Washington inafutika kabla ndege za Marekani hazijatua Pyongyang.
2. Seoul: "Mji ulioshikiliwa Mateka" (Hostage City)
Kijiografia, mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul, upo umbali wa kilomita 50 tu kutoka mpaka wa North Korea.
Siri ya Kijeshi: Korea Kaskazini imeweka mizinga (Artillery) zaidi ya 10,000 kwenye milima ya mpakani. Mizinga hii haiitaji nyuklia; ikifyatuliwa kwa pamoja, inaweza kurusha makombora 250,000 kwa saa moja kuelekea Seoul.
Mtego: Marekani anajua kuwa dakika ya kwanza tu ya kumshambulia Kim, Seoul (mji wenye uchumi mkubwa na raia wa Marekani maelfu) utageuka kuwa "bahari ya moto." Marekani hayuko tayari kutoa kafara mshirika wake mkuu kiuchumi kwa ajili ya vita ambayo haina uhakika wa kushinda.
3. "The Underground Fortress" (Ngome ya Chini ya Ardhi)
Iran ina milima, lakini Korea Kaskazini ni nchi iliyojengwa chini ya ardhi.
Tangu miaka ya 1950, Korea Kaskazini imechimba maelfu ya mahandaki (tunnels) na kambi za kijeshi mita mamia chini ya milima ya miamba.
Hata Marekani atumie mabomu makubwa kiasi gani (Bunker Busters), hawezi kuharibu jeshi la North Korea kwa shambulio moja. Kim anaweza kuendesha nchi na jeshi lake kwa miezi kadhaa akiwa chini ya ardhi, huku akiendelea kurusha makombora. Hii inafanya uvamizi wa ardhini kuwa "ndoto ya mchana."
4. China: Mlinzi asiyeonekana
Iran ina marafiki, lakini North Korea ana "Kaka Mkubwa" ambaye ni China.
Kuna mkataba wa ulinzi kati ya China na North Korea (Sino-North Korean Mutual Aid and Cooperation Friendship Treaty). Ukimshambulia mmoja, umejishughulisha na mwingine.
China haitaki kuona North Korea ikianguka. Ikianguka, Korea itakuwa moja chini ya Marekani, na wanajeshi wa Marekani watapiga kambi mlangoni mwa China. Ili kuzuia hili, China itafanya kila kitu (hata kuingia vitani) kumlinda Kim. Marekani hawezi kujiingiza kwenye vita na China—hiyo ni sawa na mwisho wa ustaarabu wa binadamu.
5. Taifa la "Dini ya Jeshi" (Juche Ideology) 🎖️đź§
Tofauti na nchi nyingine, North Korea haina upinzani wa ndani. Watu wameandaliwa kisaikolojia tangu utotoni kuwa kiongozi wao ni Mungu na Marekani ni shetani.
Huwezi kutumia mbinu za "mapinduzi ya kiraia" (color revolutions) kama yanayojaribiwa Iran. Kila mwananchi ni mwanajeshi, na kila mwanajeshi yuko tayari kufa kwa ajili ya "Mwenyekiti." Hii inafanya gharama ya vita ya ardhini kuwa kubwa sana kiasi kwamba Marekani hawezi kuimudu.
Ujasusi unatuambia kuwa North Korea haihitaji kuwa na nguvu kuliko Marekani. Inahitaji tu kuwa na uwezo wa kumdhuru Marekani "kidogo" upande wa pili. Kama unaweza kumuua mbu kwa shida, na huyo mbu ana uwezo wa kukuambukiza malaria inayoweza kukuua, utamwacha tu aendelee na safari yake.
"Dunia haitawaliwi na haki, inatawaliwa na uwezo wa kusababisha maumivu. Iran anapambana ili asidhulumiwe, lakini Korea Kaskazini ameshajenga uwezo wa kulipiza kisasi ambacho hakuna nchi yoyote duniani iko tayari kukipokea."
Je, unadhani Kim Jong-un ni kiongozi mwenye akili sana (Genius) au ni mtu mwenye bahati tu ya kuwa na majirani wakubwa?