Naona sasa propaganda na conspiracy theories zimetawala baina ya Marekani na eneo zima la Peninsula ya Korea. Tangu ile vita ya Korea 1953, baada ya Babu yake Kim Jong Un, aliyekuwa muanzilishi wa taifa la Korea kaskazini ( Kim il Sun), na baadaye mwanae (Kim Jong il) Kuwekuwa na Mvutano wa moja kwa moja baina ya kusin na kaskazini, huku mgogoro huu ukipaliliwa na marekani kupitia propaganda zake kama democracy, human rights, the interview nk....
Baada ya Vita ya pili ya dunia (WWII) Korea iligawanywa na kuwa matafa huru mawilii , huku Marekani wakileta ustaarabu wa kimagharibi eneo la Kusini (USA na washirika wake walikuwa wanawakilisha komandi ya UN) na USSR wakieneza utaarabu wa kijamaa eneo la kaskazini. Baada ya muda mfupi tuu mwaka 1951 Korea mbili zikaingia vitani huku, kusini ikisaidiwa na Marekani na washirika wake zaidi ya nchi 60 na Kaskazini ikisaidiwa na USSR, China na baadhi ya nchi za kijamaa kama Hungary, Mongolia , Czech na Bulgaria..
Matokeo ya vita ikawa Kaskazini wakashinda na kuongeza eneo lao kuvuka 38 parallel. Huu ulikuwa ni moja ya ushindi mkubwa wa USSR dhidi ya USA kipindi cha vita baridi. Na ni moja kati ya vita ambayo USA walishindwa vibaya (vita nyingine ni ile ya Vietnam na wachambuzi wengine pia wanasema mgogoro wa Syria baada ya urusi kuingia) . Rais wa USA wa kipindi hicho (Harry S Truman) akaamua kusema sio vita bali ni "police in action" ili kuficha ukweli wa mambo ingawa walituma vikosi vya kijeshi wala siyo masheriff (police wa majimbo).
Baada ya mwaka 1953 vita iliisha huku USA akipata kuistaarabisha Korea kusini na kufanya mission impossible kwa kuistaarabisha Korea kaskazini. Hakukuwa na mkataba wa amani zaidi ya demilitary demarcation zone (DMZ)kati ya Korea kusini na kaskazini, hii imepelekea mataifa haya mawili kuishi kwa uhasama wa hali ya juu.
Sasa kwa suala la kufanya mazoezi eneo la peninsula ya Korea upande wa kusini ya hiyo DMZ ndiyo inatishia usalama wa upande wa kaskazini (Korea) hivyo Kim Jong Un anaitishia marekani kuwa anajibu kwa kutumia makobora ya nyuklia kuishambulia USA na Korea kusini. Anasema atatumia intercontinental ballistic missiles(ICBM) na cruise missiles ili kulibda utaifa wao dhidi ya uvamizi wa USA na Korea kusini, maana anaamini mazoezi hayo ni uvamizi wa taifa lake na ikumbukwe kuwa USA tayari ameweka mfumo wa kinga ya makombora eneo kusini ya DMZ ili kuilinda korea kusini.
ingawa naweza sema hii hali ya sasa kweli ni mbaya sana na inaweza leta vita kubwa ila tujue kuwa tangu mwaka 1953 hadi sasa hawajawahi pigana zaidi ya vita ya mdomo na viingozi wote wawili wa Korea naweza waita Warmongers. kwanini nawaita hivi? kila siku Korea kusini wanaweka vipaza sauti karibu na mpaka wa Korea kaskazini na kutoa propaganda zao kuwa wanauwezo mkubwa kijeshi na watawavamia Korea kaskazini. tukija upande wa kaskazini nao ni hivyo hi yo kilasiku Kim anatoa propaganda zake Mara wanauwezo mkubwa kijeshi wana A-bomb wana H-Bomb nk..... ila hawapigani. Mara kwa Mara USA anafanya mazoezi ya kijeshi na Korea kusini, na Korea kaskazini anatoa vitisho ila mwisho wasiku wote kimnya.
Siwezi sema kuwa ni propaganda tuu, na kwamba vita haiwezi tokea, bali tutambue kuwa vita haiwezi tokea bila propaganda, maana propaganda inapokomaa basi watu wanaingia vitani. Na ikitokea vita katika eneo la Korea peninsula basi itakuwa vita kubwa maana kuna uhasama wa muda mrefu sana yani tangu WWII na kunauwezekano wa kutumia silaha hatari za kinyuklia na kuhusisha mataifa makubwa ie. Urusi na china upande wa Kaskazini na USA na NATO yake upande wa kusini.
Urusi na china watatoa support kwa Korea kaskazini kwa kuwa eneo la peninsula ya Korea ni muhimu kwa usalama wa hay a mataifa mawili , ni eneo muhimu katika Geopolitics za mataifa haya.
My take: naona hapa kuna conspiracy theories tuu na wanafanya mambo yao kwakujua kile wanachokitaka ili kuandaa mpango mpya wa ulimwengu. Hivi inakuwaje K. kusini na K. kaskazini kuwa na uhasama wakati wana viwanda vya uzalishaji vya pamoja mpakani? sasa vinaendeshwaje? mbali na hayo kuna wakati wanandugu wanavuka mpaka kusalimiana? zaidi sana wanamkakati wa kuungana, na hii inashangaza sana maana wote wanaridhia kuungana.
Mwisho: Naona matatizo na migogoro mingi inatengenezwa na mataifa yenye nguvu. Kipindi cha vita baridi kilibadili geopolitics za wakati ule na pia bado kinaendelea kubadili wakati huu, ingawa USA ndiye anayeshape global geopolitics kwa sasa na anapelekea kuleta machafuko mengi na huku akiendeleza sera za kipindi cha vita baridi ndo maana hata baada ya kusambaratika kwa Warsaw pact ya soviet union yeye hajavunja NATO, na ikiwa NATO ilianzishwa kwa lengo la kulinda mataifa ya magharibi dhidi ya vitisho vya soviet union.