Mwisho wa kutumia Tiketi za Karatasi kwenye kivuko cha Magogoni - Kigamboni ni Tarehe 28 Februari 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,821
12,000
Salaam Wakuu,

Abiria wanaotumia kivuko cha Magogoni Kigamboni mnakumbushwa kwamba mwisho wa matumizi ya tiketi za karatasi kwenye kivuko hicho ni Tarehe 28 Februari 2022 hivyo abiria wote mnaombwa kununua kadi za N-CARD. Kadi hizo zinapatikana Kivukoni pande Zote mbili.

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), ilizindua mfumo mpya wa ukataji tiketi kwa njia ya kielektroniki utakaotumia kadi katika Kivuko cha Magogoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam 26 Mei, 2021

Akizungumza katika uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika tarehe 26 Mei, 2021 katika eneo la Kivukoni, Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle, alisema kuwa mfumo wa N-Card utasaidia kupunguza msongamano katika kivuko hicho, kutokana na kwamba unatoa huduma kwa haraka tofauti na mfumo uliokuwa ukitumika awali.

Aidha, alisema kuwa mfumo huo mpya unafanya kazi kwa kutumia teknolojia ambayo inamtaka abiria kuwa na kadi hiyo inayopatikana kwa gharama ya Sh.1000 na baada ya kununua ataweka fedha kupitia wakala wa N-Card au mitandao ya simu kuanzia kiwango cha Sh. 500 na kuendelea.

Abiria mwenye kadi yenye salio akifika kivukoni atagusisha kadi yake kwenye geti na kukatwa nauli stahiki ya Sh.200 na hatimaye kuweza kupita.

Maselle alifafanua kuwa tangu mfumo huo uanze umeonesha mafanikio makubwa hasa kuondoa tatizo la abiria kupanga foleni mbili ya kununua tiketi na ya kuruhusiwa kuingia eneo la kusubiri kivuko.

TEMESA imesimika mageti mawili pande zote mbili za vivuko na inatarajia kubadilisha mageti yote ya zamani na kuweka mapya ili kurahisisha huduma hiyo kufanyika kwa ufanisi zaidi.

“Napenda kuwatoa hofu wananchi hasa wale ambao ni wageni kuwa mifumo yote miwili itaendelea kutumika hadi hapo usimikaji wa mageti yote utakapokamilika”,amesisitiza Eng. Maselle. .

Kufuatia utaratibu huo abiria akipata changamoto yeyote ya kadi anaweza kuwasiliana na watoa huduma waliopo katika vivuko na pia kwa kupiga simu namba 0800 11 01 50 kwa msaada zaidi na huduma hiyo itakuwa bure.
 
Kwahiyo ndugu zetu wakija kutusalimia huku kigamboni na hawana kadi watavuka vipi kama tiketi za karatasi hakuna? Foleni ya jioni na asubuhi ni kitendawili kwenu, MV. KAZI mpaka kije kuzamisha watu ndio kitu mnasubiri? Alaf sikuhizi pesa mnakusanya bila tiketi utaskia 'wenye mia mbili piteni pale unampa yule mama' hizo pesa bila shaka mnazigawana. CCM ni laana
 
Salaam Wakuu

Abiria wanaotumia kivuko cha Magogoni Kigamboni mnakumbushwa kwamba mwisho wa matumizi ya tiketi za karatasi kwenye kivuko hicho ni Tarehe 28 Februari 2022 hivyo abiria wote mnaombwa kununua kadi za N-CARD. Kadi hizo zinapatikana Kivukoni pande Zote mbili.
Na sisi tutakaokwenda mara moja tu kuchumbia au kitoa mahali hizo kadi tutazifanyia nini baada ya hapo maana Honemuni tutafanyia Londani.
 
Kwahiyo ndugu zetu wakija kutusalimia huku kigamboni na hawana kadi watavuka vipi kama tiketi za karatasi hakuna? Foleni ya jioni na asubuhi ni kitendawili kwenu, MV. KAZI mpaka kije kuzamisha watu ndio kitu mnasubiri? Alaf sikuhizi pesa mnakusanya bila tiketi utaskia 'wenye mia mbili piteni pale unampa yule mama' hizo pesa bila shaka mnazigawana. CCM ni laana
Wanajipimia kwa urefu wa kamba yao.
 
Na sisi tutakaokwenda mara moja tu kuchumbia au kitoa mahali hizo kadi tutazifanyia nini baada ya hapo maana Honemuni tutafanyia Londani.
Sijui hua yanawaza vipi haya majamaa, mtu katoka mkoani vijijini huko na furushi lake la nguo kafika kivukoni saa sita usiku na hana kadi anataka kuvuka. Watu weusi sisi ni kitendawili
 
Hii nchi ya ajabu sana.
Kuna siku wametujaza kwenye kale kajumba kuna mmama akazimia mule hakuna hewa kidogo akate moto, tumekaa zaidi ya nusu saa vivuko vyote vipo upande wa pili na hakuna meli inayo pita. Kuna jamaa walimlazimisha kutoa gari yake kivukoni ili gari ya kiongozi iingie avuke kwanza. Mimi mngeniua CCM nyie
 
Back
Top Bottom