Mwisho wa Google assistant inaondolewa kwenye simu za Android

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,322
Reaction score
2,694
Baada ya miaka karibu 10 ya kuwasaidia mamilioni ya watumiaji duniani, Google Assistant anaondoka rasmi kwenye simu za Android.

🤖 Kuanzia sasa, Google anabadilisha kila kitu kwa kumleta Gemini AI kuwa msaidizi mpya wa simu. Hii ina maana kuwa ukisema "Hey Google", badala ya Google Assistant utafunguliwa Gemini.

3_20260806_091155_0002.png
2_20260806_091155_0001.png


🔥 Gemini anakuja na uwezo mkubwa zaidi wa AI ikiwemo:
✅ Kujibu maswali kwa akili zaidi.
✅ Kusaidia kuandika, kutafsiri na kufanya utafiti.
✅ Kufanya mazungumzo ya kawaida kama binadamu. ✅ Kuendelea kufanya kazi za kila siku kama kuweka alarm, timer na mengine mengi.

6_20260806_091155_0005.png


📅 Mabadiliko haya yataanza kutolewa rasmi kuanzia Septemba 4, 2026 kwa simu zinazokidhi vigezo, na yatafika kwa watumiaji hatua kwa hatua.

💬 Je, wewe ungemchagua nani? Google Assistant au Gemini? Tuambie maoni yako kwenye c
omments. 👇
 
Hiyo technology ninayo ila siitumii, labda sio ya kila mtu
 
Kujifunza kifaransa kupitia AI...nafikiri shule tutafata vyeti tu
 
Mimi huwa inanisaidia sana , nishatengeneza logo kwa kuikomand tu , mikataba ya tenda, n.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom