Mwisho wa Daudi Ballali

Mwisho wa Daudi Ballali

Na haya yote siku moja yatakuwa wazi tu,watu hawa watakufa kweli.Mungu kaa nasi wananchi wa Tanzania.
 
Akitokea dodoma, Balali alipewa lifti kwenye ndege ya mkulu, akawekewa sumu!

Alipotoka hapo hakutaka maneno na bongo tena! Maana walikuwa wanamchekea chekea kumbe ndo wana mkili!

Akatimkia Marekani kutibiwa!

Watu walitumwa na serikali akawa hataki kuonana nao.Wengine wakidhani walitumwa kummalizia!

Ndo maana kuna wanao amini alifake kifo kwa usalama!
 
unacheza na siasa - aliemuua Tom Mboya alihukumiwa kifo lakini alionekana mitaa ya Cairo hadi kifo kilipomkuta kokote alikofia. Teknolojia ya sasa ina uwezo wa kupiga picha maiti iliyomo kaburini bila kuifukua - kwa nini mwandishi asije ingalao na kitu hicho cha kudanganyia
 
Yani mtu anasafiri all the way from Tz kwenda kuona kaburi, then anaamini baada ya kuona jina, mbona asingeanzia kwa funeral homes coz am sure kama kweli jamaa is dead there must be a funeral home which handled all the process from death mpaka anazikwa, and I am sure lazima wana picha pia. Weka hizo picha hapa from reliable sources otherwise I will always believe this dude is still well and kicking. Governor wa benki kuu anazikwa kinyemela hivyo, watu wa kawaida tu, they manage to transport bodies of their loved ones back home. Someone want me to believe familia ya governor wa benki kuu never had no resources to do so! Never in a million years
 
Mwamba wa kaskazini aliwaambia kuwa wakiendelea kumfuata fuata atamleta Balali akiwa hai
 
unacheza na siasa - aliemuua Tom Mboya alihukumiwa kifo lakini alionekana mitaa ya Cairo hadi kifo kilipomkuta kokote alikofia. Teknolojia ya sasa ina uwezo wa kupiga picha maiti iliyomo kaburini bila kuifukua - kwa nini mwandishi asije ingalao na kitu hicho cha kudanganyia

Uongo huu waambie watoto wako..technolojia gani inapiga mtu picha akiwa kaburini?acha mahekaya ya abunuwasi hayo
 
Hawa waandishi vilaza wana dharau sana, sijui katuonaje watanzania mwanaharamu wahed huyu mwandishi.
 
Wandishi wa TZ walivyokuwa wajinga na division four zao, usirudie kuandika ujinga kiasai hiki kama MCT haikukemei jamii itakukemea
 
balali.jpg

Mkazi wa Kijiji la Luganga, Wilaya ya Mufindi, Iringa, alikozaliwa Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali analazimika kutumia saa 32 kufika katika kaburi la kiongozi huyo lililopo eneo la Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

Ndugu wa Ballali wanaweza kutaka kwenda kuona kaburi la ndugu yao, kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawakuwahi kupata fursa ya kumzika Gavana huyo ambaye alikuwa kiongozi wa juu kabisa wa taasisi kubwa inayosimamia masuala ya fedha na uchumi wa nchi.

Mwandishi wa gazeti hili alisafiri kwa saa 24 kutoka Dar es Salaam hadi Washington, Marekani ambako alithibitisha pasi na shaka kwamba Ballali alizikwa Mei 21, 2008 katika makaburi ya Gate of Heaven, baada ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake Maryland, Mei 16, mwaka huo.

Safari hiyo ya siku kumi, ilianza Alhamisi Juni 26, 2014 hadi Jumapili, Julai 6. Mwandishi wa habari hizi aliligundua kaburi hilo baada ya kwenda makaburi ya Gate of Heaven kwa siku tatu mfululizo.

Siku ya kwanza, mwenyeji wa mwandishi ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa alimfikisha katika makaburi hayo, lakini kaburi la Ballali halikuonekana na hata mwandishi alipokwenda siku ya pili peke yake, kaburi hilo pia halikuonekana kwa kutokana na ukubwa wa eneo hilo.

Siku ya tatu, Mwandishi wa Mwananchi alilazimika kuomba msaada wa Ofisi ya Makaburi ya Gate of Heaven, ambayo ilimsadia kuonyesha eneo lilipo kaburi hilo, hivyo kuwezesha kupata picha zake.

Kaburi lake liko katika msitari wa mwisho kabisa na Ukanda wa Kijani wa miti iliyozunguka makaburi ya Gate of Heaven, likiwa limeandikwa jina la kiongozi huyo, pamoja na maneno ya Kiingereza yanayosomeka “When the heart weep for what it has lost, the soul rejoices for what it has found”.

Maana ya maneno hayo ni kwamba “wakati moyo ukiomboleza kwa kile kilichopotea, roho hufurahi kwa kile kilichopatikana”. Kaburi hili limezungukwa na makaburi mengine kadhaa ambayo si ya Watanzania, kwani kwa haraka kutokana na mazingira yalivyokuwa, Mwandishi wa Mwananchi hakuweza kuona kaburi jingine lenye majina yenye asili au kuwa na mwelekeo wa asili ya Tanzania.

Uthibitisho huu ni tofauti na hekaya za miaka nenda rudi zilizogubika kifo cha kiongozi huyo, ambaye tangu alipoondoka nchini kwenda Marekani Agosti 2007, hakuwahi kurejea na badala yake zilisikika taarifa za kuugua kwake, kifo chake na baadaye mazishi yake yaliyokuwa ya siri kubwa yakiwahusisha ndugu wa karibu pekee.

Kutokana na mazingira hayo, kumekuwapo na uvumi kwamba Ballali hakufa na pengine amefichwa kusikojulikana, madai yanayochagizwa na mtu aliyejitokeza katika mitandao wa kijamii ya Twitter na facebook, akidai kwamba yeye ni Ballali na kwamba hajafa, huku akisisitiza kuwa wakati ukiwadia ukweli utafahamika.

Mtu huyo asiyefahamika hadi sasa alianza kujitokeza Twitter, Oktoba Mosi, 2012 pale aliposema “Nitakutana na Rais Kikwete (Jakaya) na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani”. Mtu huyo alidai kwamba alikuja nchini Tanzania na kukaa karibu na Hoteli ya Hyatt Kempinski Kilimanjaro na baadaye kuondoka ghafla kwa kile alichokiita sababu za kiusalama.

Novemba 13 mwaka huo alituma ujumbe akisema:“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” akimaanisha kwamba niko Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, najisikia vizuri kuwa karibu na ofisi yangu ya zamani BoT.

Mtu huyo ambaye sasa tunaweza kuthibitisha kuwa ni feki amekuwa akiendelea kutuma ujumbe akijitambulisha kwa jina hilo la Ballali.

Ballali alifariki dunia kama ilivyotagazwa, lakini ilikuwaje akaenda safarini Washington, ugonjwa wake na hata kifo chake kilikuwaje? Je ndugu zake wanasemaje, safari ya kwenda Marekani ilikuwaje? Fuatilia mfululizo wa habari hii itakapoendelea kesho.

Source: Mwananchi

Hata hivyo sehemu ambapo picha imechukuliwa hapaonyeshi kuzungukwa na makaburi mengine,zaidi ya kibao tu hicho chenye maandishi ya kubandikwa
 
Hivi watanzania lini tutaacha kuwa watu wa ajabu .... mmeambiwa mtu kafa maana yake amekufa. Marekani hakuna shortcuts za kijinga na usanii kama Tanzania ... eti ooh kumejengewa jina tu, tutajuaje aliyezikwa hapo ni yeye, kwa nini azikwa marekani, etc ..... Kwa kifupi waulizeni ndugu au marafiki zenu walioko marekani ni nini kinatokea mtu akifa, hata kifo cha kawaida hampati mwili mpaka uchunguzi ufanyike. Maziko yenyewe si bei rahisi ndio maana kuna watu wanachomwa moto kwa kushindwa kupata gharama za maziko. Wageni wengi tu huzikwa marekani kwa hiyo Balali hakuwa wa kwanza na wala hatakua wa mwisho kuzikwa marekani! labda ndio yalikua maamuzi yake na mke wake. kwenye maamuzi kama hayo ya maziko Marekani anasikilizwa mtu mwenye power of attorney, kwa hiyo hata mje jumuia nzima tunataka kwenda mzika Tanzania lakini mke wake akaamua azikwe marekani maana yake ni atazikwa marekani...mke wake angesema achomwe moto, angechomwa moto. MAREKANI HUENDESHWA KWA SHERIA HAKUNA SHORTCUTS ZISIZO NA CONSEQUENCES!

Marekani hamna shortcut my azz.
 
mbona kwenye picha kwenye kaburi moja tu, au ballali ndio mtu wa mwisho kuzikwa hapo.
nmepata mashaka sana na uhandishi wako unaobase upande mmoja ,halafu unauita wa kichunguzi.

Ndugu NYANYADO ni kweli kabisa, mimi pia nimecheki hii picha kwa umakini kidogo nikastuka mbona kaburi moja tu? Hapo ndiyo tunamwomba mwandishi toleo linalokuja atueleze kinagaubaga.
 
Kwa ukubwa wa Gazeti la Mwanainchi sidhani kama picha ya kaburi ilipaswa kuonwa na wahusika kuwa inakidhi kiu ya Watanzania kwa ishu ilivyo na ukubwa wake.

Na kama sikosei mmeandika kuwa siku kwanza kufika makaburini, kaburi halikukutwa.....Marekani ninavyoamini ni kuwa wapo makini kwa kuratibu shughuli zao, so sielewi unawezaje kutembelea sehemu maarufu/ya kihistoria bila kuona ulichokusudia ?

Unaweza kumpeleka Mtalii Serengeti, aliyetoka mbali kote kwa hamu ya kumuona Chui, mkazunguka siku nzima na kwa bahati mbaya mkashindwa kumuona Chui....je na kaburi ni vivyo hivyo ?

Ewe "Mtalii" uliridhika vipi kutokuona kaburi siku ya kwanza ? Je ulipata mashaka yoyote kwa kulipata kaburi baadae ? nakushauri baada ya mwezi mmoja rudi tena kwa kushtukiza kama utaliona...then wape muda kama ulivyofanya awali....ukirudi utaliona.
 
We ulitakaje?? Achukue mifupa afanya DNA?? Yeye ni muandishi kaishia hapo

Huyu kama kweli alifanya kilichoandikwa, basi alikuwa mpuuzi. Alifanya kazi isiyokuwa yake. Mwandishi wa habari hatoi uthibitisho wa kifo cha mtu. Ndo maana aliishia kupiga picha.
 
Hivi watanzania lini tutaacha kuwa watu wa ajabu .... mmeambiwa mtu kafa maana yake amekufa. Marekani hakuna shortcuts za kijinga na usanii kama Tanzania ... eti ooh kumejengewa jina tu, tutajuaje aliyezikwa hapo ni yeye, kwa nini azikwa marekani, etc ..... Kwa kifupi waulizeni ndugu au marafiki zenu walioko marekani ni nini kinatokea mtu akifa, hata kifo cha kawaida hampati mwili mpaka uchunguzi ufanyike. Maziko yenyewe si bei rahisi ndio maana kuna watu wanachomwa moto kwa kushindwa kupata gharama za maziko. Wageni wengi tu huzikwa marekani kwa hiyo Balali hakuwa wa kwanza na wala hatakua wa mwisho kuzikwa marekani! labda ndio yalikua maamuzi yake na mke wake. kwenye maamuzi kama hayo ya maziko Marekani anasikilizwa mtu mwenye power of attorney, kwa hiyo hata mje jumuia nzima tunataka kwenda mzika Tanzania lakini mke wake akaamua azikwe marekani maana yake ni atazikwa marekani...mke wake angesema achomwe moto, angechomwa moto. MAREKANI HUENDESHWA KWA SHERIA HAKUNA SHORTCUTS ZISIZO NA CONSEQUENCES!

Nadhani hayo ungelenga kwa mwandishi husika, hii stori yake ndio inatuambia Marekani kuna shortcuts...hebu mkemee aache hizo.

Alafu kabla ya kupanic, ungefanya kwanza utafiti ni kwa nini Watanzania wanahitaji uthibitisho wa kifo cha Balali, badala ya kuja na stori mreeeeeeeeefu.
 
huyu mwandishi kasafiri kwenda Amerika kwa gharama za nani?ili amletee nani uthibitisho?kwa lengo gani?.Ebu acheni umburura kutuona watz wote ni wa shule za kata!!
 
Nadhani hayo ungelenga kwa mwandishi husika, hii stori yake ndio inatuambia Marekani kuna shortcuts...hebu mkemee aache hizo.

Alafu kabla ya kupanic, ungefanya kwanza utafiti ni kwa nini Watanzania wanahitaji uthibitisho wa kifo cha Balali, badala ya kuja na stori mreeeeeeeeefu.

kazi kweli kweli ... naelewa sana jinsi hiki kifo kilivyoleta kutokueleweka katika jamii kwa sababu kila jambo au ufisadi uliotokea alisingiziwa yeye as if mfumo wote wa pesa ulikua unafanywa na mtu mmoja na hakuna jinsi ya kutrace wengine ... haya ni maajabu ya dunia .... mwandishi kakwambia kaburi liko wapi ... wewe kama una maslahi marefu na kifo chake unaruhusiwa kwenda pale kujiridhisha, unaweza ukaomba kibali cha mahakama ili ufukue na kufanya hizo DNA tests kama unataka!

kwa kifupi watanzania wafanye juhudi za kuweka utawala tofauti utakao fanya uchunguzi na kuchukulia hatua wote waliohusika na ufisadi mbali mbali nchini maana hata mimi naamini kuna wengi tu bado wanadunda mitaani waliofanya huu ufisadi!
 
Tutajuaje hilo kaburi kwenye picha lipo Marekani? Haiwezekani wakachonga kaburi fake ili watuzuge?

Back
Top Bottom