Mwisho wa Daudi Ballali

Mwisho wa Daudi Ballali

Upuuzi mtupu tutafanyana wajinga hadi lini?
Kwani kuwepo kwa kaburi lililoandikwa Ballali haimaanishi aliyezikwa humo ni yeye, kwa hili mnatufanya tuhisi kuna uchafu mwingi alifanya ambao serikari imeukalia . imeendelea

Tuko pamoja mkuu, huyo aliyeona kaburi ana uhakika gani kwamba kilichoko humo ndani ni mabaki ya mwili wa Balalli? Yaani jina tu juu ya kaburi ndio uthibitisho tosha kwamba Balali alizikwa hapo bila Watanzania wanwoishi huko kushuhudia? Kwa nini Watanzania wanaoishi huko hawakupewa nafasi ya kuuaga mwili au kuhudhuria mazishi?

Tiba
 
kweli akili ya kuambiwa changanya na yako. kaburi haliwezi kuwa uthibitisho wa mtu kufa.
Eti alitafuta kaburi bila mafanikio siku ya kwanza na ya pili na ya tatu ndipo alipowauliza wanaohusika kuangalia makaburi???? Kwa nini hakufanya hivyo tangu siku ya kwanza!!!!????
 
Mkazi wa Kijiji la Luganga, Wilaya ya Mufindi, Iringa, alikozaliwa Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali analazimika kutumia saa 32 kufika katika kaburi la kiongozi huyo lililopo eneo la Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

Ndugu wa Ballali (pichani) wanaweza kutaka kwenda kuona kaburi la ndugu yao, kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawakuwahi kupata fursa ya kumzika Gavana huyo ambaye alikuwa kiongozi wa juu kabisa wa taasisi kubwa inayosimamia masuala ya fedha na uchumi wa nchi.

Mwandishi wa gazeti hili alisafiri kwa saa 24 kutoka Dar es Salaam hadi Washington, Marekani ambako alithibitisha pasi na shaka kwamba Ballali alizikwa Mei 21, 2008 katika makaburi ya Gate of Heaven, baada ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake Maryland, Mei 16, mwaka huo.

Safari hiyo ya siku kumi, ilianza Alhamisi Juni 26, 2014 hadi Jumapili, Julai 6. Mwandishi wa habari hizi aliligundua kaburi hilo baada ya kwenda makaburi ya Gate of Heaven kwa siku tatu mfululizo.

Siku ya kwanza, mwenyeji wa mwandishi ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa alimfikisha katika makaburi hayo, lakini kaburi la Ballali halikuonekana na hata mwandishi alipokwenda siku ya pili peke yake, kaburi hilo pia halikuonekana kwa kutokana na ukubwa wa eneo hilo.

Siku ya tatu, Mwandishi wa Mwananchi alilazimika kuomba msaada wa Ofisi ya Makaburi ya Gate of Heaven, ambayo ilimsadia kuonyesha eneo lilipo kaburi hilo, hivyo kuwezesha kupata picha zake.

Kaburi lake liko katika msitari wa mwisho kabisa na Ukanda wa Kijani wa miti iliyozunguka makaburi ya Gate of Heaven, likiwa limeandikwa jina la kiongozi huyo, pamoja na maneno ya Kiingereza yanayosomeka “When the heart weep for what it has lost, the soul rejoices for what it has found”.

Maana ya maneno hayo ni kwamba “wakati moyo ukiomboleza kwa kile kilichopotea, roho hufurahi kwa kile kilichopatikana”. Kaburi hili limezungukwa na makaburi mengine kadhaa ambayo si ya Watanzania, kwani kwa haraka kutokana na mazingira yalivyokuwa, Mwandishi wa Mwananchi hakuweza kuona kaburi jingine lenye majina yenye asili au kuwa na mwelekeo wa asili ya Tanzania.

Uthibitisho huu ni tofauti na hekaya za miaka nenda rudi zilizogubika kifo cha kiongozi huyo, ambaye tangu alipoondoka nchini kwenda Marekani Agosti 2007, hakuwahi kurejea na badala yake zilisikika taarifa za kuugua kwake, kifo chake na baadaye mazishi yake yaliyokuwa ya siri kubwa yakiwahusisha ndugu wa karibu pekee.

Kutokana na mazingira hayo, kumekuwapo na uvumi kwamba Ballali hakufa na pengine amefichwa kusikojulikana, madai yanayochagizwa na mtu aliyejitokeza katika mitandao wa kijamii ya Twitter na facebook, akidai kwamba yeye ni Ballali na kwamba hajafa, huku akisisitiza kuwa wakati ukiwadia ukweli utafahamika.

Mtu huyo asiyefahamika hadi sasa alianza kujitokeza Twitter, Oktoba Mosi, 2012 pale aliposema “Nitakutana na Rais Kikwete (Jakaya) na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani”. Mtu huyo alidai kwamba alikuja nchini Tanzania na kukaa karibu na Hoteli ya Hyatt Kempinski Kilimanjaro na baadaye kuondoka ghafla kwa kile alichokiita sababu za kiusalama.

Novemba 13 mwaka huo alituma ujumbe akisema:“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” akimaanisha kwamba niko Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, najisikia vizuri kuwa karibu na ofisi yangu ya zamani BoT.

Mtu huyo ambaye sasa tunaweza kuthibitisha kuwa ni feki amekuwa akiendelea kutuma ujumbe akijitambulisha kwa jina hilo la Ballali.

Ballali alifariki dunia kama ilivyotagazwa, lakini ilikuwaje akaenda safarini Washington, ugonjwa wake na hata kifo chake kilikuwaje? Je ndugu zake wanasemaje, safari ya kwenda Marekani ilikuwaje? Fuatilia mfululizo wa habari hii itakapoendelea kesho.

Source: Mwananchi

It takes little intelligence to exhume the hidden agenda - the Balali death conspiracy. Who is interested in the story when, and why? Who planned and paid the cost for journalist's US trip and why? Is the journalist moral behavior above or below questionable integrity? Does Mwananchi have any interest in the story? What is the relationship between parties interested in the story and the newspaper? Something is heating up, and will soon come public.
 
Kwamba mtu aliyekuwa na hadhi ya Gavana wa Benki Kuu anafariki Marekani halafu hata maofisa wa Ubalozi wetu,wawakilishi wetu katika mashirika makubwa ya kifedha yaliyoko US wote wanashindwa kuhudhuria hata kwa uchache wao?
Hata mchawi hakosi mtu wa kumzika na kuwadhibitishia watu kuwa huyo mtu kafa na kuzikwa.
Mwandishi kutueleza kaona kaburi limeandikwa jina eti ndio anakuja kutuambia ni habari za uchunguzi? Basi angeanzia uchunguzi wake katika historia ya matibabu,daktari aliye saini hati ya kifo na mengineyo angeonyesha kweli kafanya kazi.
Watu wangapi wanaokotwa wamekufa na majina yao hayafahamiki? Akizikwa na mkaamua kulipa jina hilo kaburi mfano MSALANI bin so and so hivyo itakuwa yule aliyepo humo ni huyo mwenye jina wakati MSALANI yupo Lumumba anaendelea kutupia post JF na anavuta mpango wake wa buk7 bila wasiwasi?


Sent from my iPad using JamiiForums

Kwi kwi Kwi kwi eti aliyekufa MSALANI wa Lumumba hahahahahaaa!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Kwi kwi Kwi kwi eti aliyekufa MSALANI wa Lumumba hahahahahaaa!!!!!

Mkuu nimetoa mfano tuu ili ueleweke. MSALANI tunaye hapa JF anapiga mzigo mwanzo mwisho hana hata mapumziko ya mwisho wa wiki wala likizo anasaka mshiko tuu. Chezea buk7 weye! Ha ha ha


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
mwanajeshi aliyemuuwa sethi fundikira naye tunaambiwa kazikwa na magereza dodoma bila familia kuwepo.

waambie bwana duuuu hongera bwana kwa kusema ukweli

We meandishi kilaza sana eti kisa kaburi lol! Kwenye tamthilia za kikorea, na Kifilipino tunaona makaburi inamaana ni ya kweli?

Balali yupo hai na anaendelea kula bata kama kawaida CCM acheni kutufanya wapumbavu tusiyojuwa kitu.

Mazoea mabaya maana eti hata sokoine alikufa baada ya gari 'kuseleleka' na baadaye kugongana na Dumisani Dube na baadaye Dube kuachiwa na kutokomea SA!
 
Inaonekana huyu mwandishi hata akilikuta kaburi lenye jina lake na picha yake ataamini kuwa alishafariki...!Yani yeye anachohitaji kuthibitisha mauti ni jina halisi tu kwenye kaburi,basi!
 
Picha ya kaburi hujaiona?

Picha ya kabur haimaanishi kama aliezikwa ni David balali au la,hiyo ni kama picha ya kuigiza tu ila balal yupo hai(serikali haikutoa sababu yoyote ya kutokumzika kwao mtu mkubwa kama balal halafu mazishi yake yawe ya siri,msiba gan unaofichwafichwa?


If your not right...go left,,
 
Nisabau zipi zilizoifanya serikali ya magamba kuamua kumzika huko ughaibuni?
 
ManDla Jr, Huyu mwandishi wa magaze ameshapata kiinua mgongo chake na sasa anatuletea blah blah zisizokuwa na mpango. Kwa vile anataka kujaza nafasi kny gazeti lake aendelee kuchapisha hiyo story yake ya Alinacha, akidhani sisi wote ni wajinga kama Maccm.
Hali yetu ya maisha imepondeka partly kwa ajili ya fedha za EPA ambazo Balali na CCM walituibia kutoka BOT.
Balali hajafa, na hili linathibitishwa na nduguze waliopo Mafinga, Iringa ambao wengi wao ni wanaccm!

Machozi yananibubujika ndugu zangu,wapi watumwa wa Lumumba?
 
Last edited by a moderator:
kweli akili ya kuambiwa changanya na yako. kaburi haliwezi kuwa uthibitisho wa mtu kufa.

Kama serikali iliweza kurudisha mabaki ya wanajeshi toka msumbiji na kwenda kuyazika tena pale naliendele Mtwara,basi na mabaki ya gavana yaletwe.
 
Ukitaka kujua huu ni uongo usio na shaka mi pale mwandishi anaposema eti alitumia siku mbili kutafuta bila mafanikio ila siku ya tatu ndo akakumbuka kwenda kwa mamlaka inayohusika wamsaidie..hivi kwa jinsi mwandishi alivodiscribe ukubwa wa ilo eneo sidhani kama mtu alieko katika mission kama hiyo tena kwa safari zaidi ya masaa 30 kutafuta ukweli eti angeanza kuangaika kutafuta ilo kaburi bila kushilikisha wausika.. nadhani mwadishi anajaribu kutengeneza na kuulemba uongo wake uwe mlefu na jua toleo lijalo litanunulika vya kutosh kwa sababu ya huu uongo.

Hakuna marefu yasiyo na ncha,na kila lenye mwanzo lina mwisho.
 
Tuko pamoja mkuu, huyo aliyeona kaburi ana uhakika gani kwamba kilichoko humo ndani ni mabaki ya mwili wa Balalli? Yaani jina tu juu ya kaburi ndio uthibitisho tosha kwamba Balali alizikwa hapo bila Watanzania wanwoishi huko kushuhudia? Kwa nini Watanzania wanaoishi huko hawakupewa nafasi ya kuuaga mwili au kuhudhuria mazishi?

Tiba

ha ulitaka wamfukue aone hizi gongo za slaa ni majanga kwa taifa
 
Ujinga mwingine bana.
Buku7 hebu danganyaneni wenyewe kwa wenyewe.
Mbona mnajishtukia nani kawauliza au mmeona balali ameshachoka maisha ya kujificha sasa mnamtisha ili arudi dark
 
Back
Top Bottom