Mwisho wa Daudi Ballali

Mwisho wa Daudi Ballali

balali.jpg

mnataka ni wasaliti wazazi wangu na walimu wangu walionifundisha na kujua ujinga na ukweli acheni porojo zenu kama gazeti mmehongwa nyie kuleni hizo pesa i tambueni jamii ya watanzania ya leo s yakuwaamini wandishi wa habari tena tushawastukia acheni porojo kama kafa kweli kwanini asije zikwa tz mmekaa mmeamua jenga kaburi ili kutuzuga eti acheni upuuzi wenu kuanzia mwandishi mpaka mhariri wa gazeti la mwananchi nimewadharau na sisomi tena taka taka zenu hizi bora niangalie bongo movie
 
It takes little intelligence to exhume the hidden agenda - the Balali death conspiracy. Who is interested in the story when, and why? Who planned and paid the cost for journalist's US trip and why? Is the journalist moral behavior above or below questionable integrity? Does Mwananchi have any interest in the story? What is the relationship between parties interested in the story and the newspaper? Something is heating up, and will soon come public.
Nimekuelewa ,kuna kitu hapa ..
 
Mwandishi weka na death certificates ili tujue mmeamua kumfuta balali kwenye list ya wanaishi
 
Mwandishi weka na death certificates ili tujue mmeamua kumfuta balali kwenye list ya wanaoishi
 
mnataka ni wasaliti wazazi wangu na walimu wangu walionifundisha na kujua ujinga na ukweli acheni porojo zenu kama gazeti mmehongwa nyie kuleni hizo pesa i tambueni jamii ya watanzania ya leo s yakuwaamini wandishi wa habari tena tushawastukia acheni porojo kama kafa kweli kwanini asije zikwa tz mmekaa mmeamua jenga kaburi ili kutuzuga eti acheni upuuzi wenu kuanzia mwandishi mpaka mhariri wa gazeti la mwananchi nimewadharau na sisomi tena taka taka zenu hizi bora niangalie bongo movie

hili gazeti mwananchi sasa limeanza kupoteza muelekeo.
 
Aseee cjawah ona uongo kama huu, yaan kama nchi hii wangekuwa hakuna kuuwana m ningefanya pravety investigation nikaja nauthibitisho, ila ss duuuuuuuuuuuu. Ngoja tuendelee kudanganywa
 
mnataka ni wasaliti wazazi wangu na walimu wangu walionifundisha na kujua ujinga na ukweli acheni porojo zenu kama gazeti mmehongwa nyie kuleni hizo pesa i tambueni jamii ya watanzania ya leo s yakuwaamini wandishi wa habari tena tushawastukia acheni porojo kama kafa kweli kwanini asije zikwa tz mmekaa mmeamua jenga kaburi ili kutuzuga eti acheni upuuzi wenu kuanzia mwandishi mpaka mhariri wa gazeti la mwananchi nimewadharau na sisomi tena taka taka zenu hizi bora niangalie bongo movie

Nimeisoma makala gazetini imeniacha na maswali mengi sana. Moyo wangu unagoma kushawishika kama kuna ukweli wowote.
 
Hivi watanzania lini tutaacha kuwa watu wa ajabu .... mmeambiwa mtu kafa maana yake amekufa. Marekani hakuna shortcuts za kijinga na usanii kama Tanzania ... eti ooh kumejengewa jina tu, tutajuaje aliyezikwa hapo ni yeye, kwa nini azikwa marekani, etc ..... Kwa kifupi waulizeni ndugu au marafiki zenu walioko marekani ni nini kinatokea mtu akifa, hata kifo cha kawaida hampati mwili mpaka uchunguzi ufanyike. Maziko yenyewe si bei rahisi ndio maana kuna watu wanachomwa moto kwa kushindwa kupata gharama za maziko. Wageni wengi tu huzikwa marekani kwa hiyo Balali hakuwa wa kwanza na wala hatakua wa mwisho kuzikwa marekani! labda ndio yalikua maamuzi yake na mke wake. kwenye maamuzi kama hayo ya maziko Marekani anasikilizwa mtu mwenye power of attorney, kwa hiyo hata mje jumuia nzima tunataka kwenda mzika Tanzania lakini mke wake akaamua azikwe marekani maana yake ni atazikwa marekani...mke wake angesema achomwe moto, angechomwa moto. MAREKANI HUENDESHWA KWA SHERIA HAKUNA SHORTCUTS ZISIZO NA CONSEQUENCES!
Tutajuaje hilo kaburi kwenye picha lipo Marekani? Haiwezekani wakachonga kaburi fake ili watuzuge?
 
Mwandishi alikuwa anafanya research au field? Alinadhani CCM wanaweza tengeneza kitu na wakaacha open sehemu zinazotiliwa shaka?hivi alitegemea kaburi halipo na wakati wamekuambia kafa?walijua utaenda tu je aliyezikwa ni yeye?na kaburi na fact ya ufo wake pekee?
 
huu sio uthibitisho. huwezi kusafiri amerika kutuletea picha ya kaburi tu tukuamini. tumia akili za mwanahabari anayeijua kazi yake.
Ni sawa na uambiwe wewe sio raia wa Tanzania alafu unakuja na picha ya makaburi ya babu zako kuonyesha walizikwa hapa nchini, aongeze supporting document zingine
 
Mungu kaiumba Tanzania na maajabu yake.....!!
 
Hizi tutaziona sana mpaka 2015 ipite. Kila gazeti ni kipindi cha kupiga hela.
 
Mkazi wa Kijiji la Luganga, Wilaya ya Mufindi, Iringa, alikozaliwa Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali analazimika kutumia saa 32 kufika katika kaburi la kiongozi huyo lililopo eneo la Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

Ndugu wa Ballali (pichani) wanaweza kutaka kwenda kuona kaburi la ndugu yao, kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawakuwahi kupata fursa ya kumzika Gavana huyo ambaye alikuwa kiongozi wa juu kabisa wa taasisi kubwa inayosimamia masuala ya fedha na uchumi wa nchi.

Mwandishi wa gazeti hili alisafiri kwa saa 24 kutoka Dar es Salaam hadi Washington, Marekani ambako alithibitisha pasi na shaka kwamba Ballali alizikwa Mei 21, 2008 katika makaburi ya Gate of Heaven, baada ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake Maryland, Mei 16, mwaka huo.

Safari hiyo ya siku kumi, ilianza Alhamisi Juni 26, 2014 hadi Jumapili, Julai 6. Mwandishi wa habari hizi aliligundua kaburi hilo baada ya kwenda makaburi ya Gate of Heaven kwa siku tatu mfululizo.

Siku ya kwanza, mwenyeji wa mwandishi ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa alimfikisha katika makaburi hayo, lakini kaburi la Ballali halikuonekana na hata mwandishi alipokwenda siku ya pili peke yake, kaburi hilo pia halikuonekana kwa kutokana na ukubwa wa eneo hilo.

Siku ya tatu, Mwandishi wa Mwananchi alilazimika kuomba msaada wa Ofisi ya Makaburi ya Gate of Heaven, ambayo ilimsadia kuonyesha eneo lilipo kaburi hilo, hivyo kuwezesha kupata picha zake.

Kaburi lake liko katika msitari wa mwisho kabisa na Ukanda wa Kijani wa miti iliyozunguka makaburi ya Gate of Heaven, likiwa limeandikwa jina la kiongozi huyo, pamoja na maneno ya Kiingereza yanayosomeka “When the heart weep for what it has lost, the soul rejoices for what it has found”.

Maana ya maneno hayo ni kwamba “wakati moyo ukiomboleza kwa kile kilichopotea, roho hufurahi kwa kile kilichopatikana”. Kaburi hili limezungukwa na makaburi mengine kadhaa ambayo si ya Watanzania, kwani kwa haraka kutokana na mazingira yalivyokuwa, Mwandishi wa Mwananchi hakuweza kuona kaburi jingine lenye majina yenye asili au kuwa na mwelekeo wa asili ya Tanzania.

Uthibitisho huu ni tofauti na hekaya za miaka nenda rudi zilizogubika kifo cha kiongozi huyo, ambaye tangu alipoondoka nchini kwenda Marekani Agosti 2007, hakuwahi kurejea na badala yake zilisikika taarifa za kuugua kwake, kifo chake na baadaye mazishi yake yaliyokuwa ya siri kubwa yakiwahusisha ndugu wa karibu pekee.

Kutokana na mazingira hayo, kumekuwapo na uvumi kwamba Ballali hakufa na pengine amefichwa kusikojulikana, madai yanayochagizwa na mtu aliyejitokeza katika mitandao wa kijamii ya Twitter na facebook, akidai kwamba yeye ni Ballali na kwamba hajafa, huku akisisitiza kuwa wakati ukiwadia ukweli utafahamika.

Mtu huyo asiyefahamika hadi sasa alianza kujitokeza Twitter, Oktoba Mosi, 2012 pale aliposema “Nitakutana na Rais Kikwete (Jakaya) na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani”. Mtu huyo alidai kwamba alikuja nchini Tanzania na kukaa karibu na Hoteli ya Hyatt Kempinski Kilimanjaro na baadaye kuondoka ghafla kwa kile alichokiita sababu za kiusalama.

Novemba 13 mwaka huo alituma ujumbe akisema:“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” akimaanisha kwamba niko Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, najisikia vizuri kuwa karibu na ofisi yangu ya zamani BoT.

Mtu huyo ambaye sasa tunaweza kuthibitisha kuwa ni feki amekuwa akiendelea kutuma ujumbe akijitambulisha kwa jina hilo la Ballali.

Ballali alifariki dunia kama ilivyotagazwa, lakini ilikuwaje akaenda safarini Washington, ugonjwa wake na hata kifo chake kilikuwaje? Je ndugu zake wanasemaje, safari ya kwenda Marekani ilikuwaje? Fuatilia mfululizo wa habari hii itakapoendelea kesho.

Source: Mwananchi

Naona kama wote hamjasoma hii story. wamesema inaendelea na keshio mbali.
 
Naona kama wote hamjasoma hii story. wamesema inaendelea na keshio mbali.

Kizazi cha sasa/leo ni wavivu sana kwenye kusoma. Kuna viongozi wengine pia nao ni wavivu kusoma pamoja na kuwa
na sifuri darasani (zero) ila wao wanataka madaraka tuu. Kusoma hapana....
 
Back
Top Bottom