Mkuu wala tusimsingizie babu wa watu, tatizo letu ni usimba na yanga na pia maandalizi kiongozi.
Tunajisahau na kudhani tumeshapiga hatua tunajiweka class ambayo hatuko, tuache siasa ifanyike juhudi kuinua kiwango cha michezo, kwa sasa ni kama tunabahatisha kiongozi. Timu imejaa wavuta bangi, wasio na adabu, makocha wetu wamejaa siasa na kulalamika tu badala ya kutafuta njia za kubobea kwenye fani unategemea nini hapo.
Ushauri wa bure tu, tusahau habari za mashindano kwa sasa, serekali au sijui wadau watengeneze timu kwa miaka 3 au zaidi ndio tuanze kushindana, kwa sasa ni kupoteza muda na hela bure tu
Mzee Mwinyi alizungumzia uhalisia wa timu yetu. Hata ww pengine ungesema vivyo hivyo au zaidi yake. JK alijitahidi kadri yake, ikiwemo kumgharamia kocha na kuwaenzi wachezaji kwa hali na mali lakini wapi! Tatizo bado lipo, ina maana halijapata dawa? Hatuna wachezaji? Tatizo ni nini?Ni wakati sasa watanzania tumuombe rais huyu mstaafu afute kauli yake kuwa: "SISI NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU", maana kila mashindano tunaharibu. Yule mzee katulaani!
Mzee Mwinyi alizungumzia uhalisia wa timu yetu. Hata ww pengine ungesema vivyo hivyo au zaidi yake. JK alijitahidi kadri yake, ikiwemo kumgharamia kocha na kuwaenzi wachezaji kwa hali na mali lakini wapi! Tatizo bado lipo, ina maana halijapata dawa? Hatuna wachezaji? Tatizo ni nini?
Ni wakati sasa watanzania tumuombe rais huyu mstaafu afute kauli yake kuwa: "SISI NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU", maana kila mashindano tunaharibu. Yule mzee katulaani!
Pengine ni kwa kujua historia yetu ndo akatoa hiyo kauli. Unadhani mtu akisema TZ ni nchi ya ufisadi atakuwa amekosea? wala hahitaji kuondoa hiyo kauli yake, yuko sahihi na ukweli ndo huo. Ataendelea kuwa sahihi mpaka tutakapoondoa siasa kwenye mambo yanayohitaji utaalamu na umakini!