Kwa ukuaji wa Mpira Tanzania sasa ni Wakati sahihi wa Rais Mstaafu Mwinyi Kufuta Kauli yake

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
482
969
Wasalam mabibi na mababu,

Ukweli usiopingika ni kuwa zama hizi Kumekuwa na mapinduzi makubwa sana hasa katika mchezo wa Mpira wa miguu, leo hii Tanzania ni fahari tunaona club mbili simba na Yanga zikipambana katika kufika hatua ya robo Fainali katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, ila ata timu za taifa kufuzu AFCON na WAFCON.

Kwa mafanikio haya ata kwa uchache tunastahili kujipongeza na Kujiona tumepiga hatua, bila shaka uenda tunashika Hadi namba moja kwa Afrika mashariki namna hamasa za mchezo zilivyoshika hatamu kwa Tanzania.

Sasa leo nimekumbuka miaka tisini 90` Rais Ali Hassan Mwinyi aliwahi kusema kuwa Tanzania katika michezo ni 'KICHWA CHA MWENDAWAZIMU' kutokana na kushindwa kupiga hatua zozote katika Michuano yoyote ile sisi ilikuwa hakuna hatua yoyote tunayopiga yani.

Sasa kwa mafanikio aya madogo nadhani n wakati sahihi mzee wetu Alhaj Ali Hassan Mwinyi Kufuta Kauli yake hii kuwa kwa sasa kwenye soka la Tanzania sio 'KICHWA CHA MWENDAWAZIMU TENA' ili kama ni Laana basi ifutike na tuzidi kufika Mbali zaidiii.
 
Kwa utakatifu upi?
 
Ondoa foreigners uone !!! Kama pale yanga ondoa wageni uone vilevile ssc
unafikiri kukuwa kwa mprira inatizamwa swala la wachezaji tu kuwa ni wachezaji wa ndani? Kuna mambo mengi ya kuangalia?kwanza uwezo wa wachezaji, timu kushiriki mashindano mbali mbali na kushinda, hali ya kifedha ya timu hii inaenda mpaka mishahara kwa wachezaji, marupurupu, jezi nakadhalika. Sasa hivi Simba na Yanga zimeweza kufanikisha hayo na kuitangaza au kuipeperusha vyema bendera yetu. Ukisema wachezaji ni wa nje, je timu za wenzetu kama Ulaya huko , Kina Ronaldo, Messi na wengine wanachezea vilabu vya nchi zao?
 
Back
Top Bottom